KESI YA MAUAJI: Utetezi wa Elizabeth Michael (Lulu) ndani ya mahakama kuu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
=> "Nilipofika kwa marehemu 'Kanumba' nilimkuta yupo kwenye dressing table, nilikaa kitandani kwa kuwa hapa kuwa na sehemu ya kukaa"- Lulu

=> "Nilikuwa nataka kutoka ila marehemu 'Kanumba' alinikataza, alikuwa hataki nitoke na marafiki zangu"- Lulu

=> Mara nyingi marehemu alikuwa ananipiga kila akilewa na sio kwa akili zake"- Lulu

=> Marehemu nilipomwambia natoka na marafiki zangu alinikimbiza na taulo na mimi nilikuwa naogopa kupigwa"-Lulu

=> "Alipoona simu yangu inaita akahisi ni simu ya mwanaume akasema kwanini naongea na simu ya mwanaume mbele yake?"

=> Marehemu akaingia uvunguni akatoa panga akasema leo nakuua huku akinipiga na panga kwenye mapaja" - Lulu

=> "Nilipoona hivyo ananikimbiza na taulo nilitoka nikakimbilia chooni na kupiga kelele - Lulu

=> "Marehemu alianguka mwenyewe na kujigonga kwa nguvu na kuinuka sehemu nyingine alikuwa kama anatapatapa - Lulu

=> "Baada ya muda mchache nilisikia kishindo kama mtu anafungua mlango - Lulu

=> "Nilimkuta amelala, nilihisi amejifanyisha nikaanza kumwambia kuwa wakija watu nitawambia kila kitu ulivyonipiga na panga"

=> "Nilimwambia Seth kuwa Kanumba amedondoka na akajaribu kumuamsha hakuamka akasema anaenda kumuita daktari" -Lulu

=> "Alivyosema anaenda kumuita daktari nikasema na mimi naondoka nikiogopa anaweza akaamka akaanza kunipiga - Lulu

=> "Niliondoka nikawasha gari kuelekea Coco Beach, Huko Coco Beach hakukuwa na kitu nilienda tu kutuliza akili - Lulu

=> "Nilivyofika Coco Beach SMS zilianza kusambaa kuniuliza kuwa nasikia Kanumba amefariki - Lulu

=> "Nikachukua simu nikampigia kidume 'rafiki yake Kanumba' kumuuliza Kanumba yupo hospitali gani? nije kumuona-Lulu

=> "Akaniambia wewe usije hospitali, niambie uko wapi tuonane Bamaga? "- Lulu

=> "Tulivyokutana Bamaga alikuwa kama anataka kuongea na mimi ghafla wakaja askari kunikamata - Lulu

=> "Na kunipeleka Oysterbay polisi, Nilipofika Oysterbay nilikuta watu wengi sana niliyemtambua ni Ray- Lulu

=> "Nilijua Kanumba amefariki nikiwa polisi"- Lulu

=> "Nilipomkuta Ray Oysterbay polisi nikajua Kanumba amekamatwa kwasababu ya makelele niliyokuwa nayapiga kule nikajua watu walisikia" - Lulu

=> "Kwa namna yoyote ile mimi sijasababisha kifo cha Kanumba, na mimi ndiye nilieshambuliwa na marehemu " - Lulu

=> ....kutokana na umbile langu nilikuwa mdogo na alikuwa na uwezo wa kufanya chochote kwenye mwili wangu kwa sababu yeye ndo alikuwa na silaha

Maswali kutoka kwa wakili wa serikali


=> Wakili wa Serikali = Wewe na Kanumba mlianza mahusiano kwa muda gani?
= "KWA MIEZI MINNE" - Lulu

=> Wakili wa Serikali "Inamaana Kanumba alikukimbiza na taulo mpk nje halikuanguka?"
= Jibu "NDIO ALINIKIMBIZA AKIWA PEKU NA TAULO" - Lulu


Chanzo: BONGO 5

====================================

 
Kwa utetezi huu inaonyesha kiasi fulani ali plan kama self defence fulani.
 
Hivi mtu unayempenda unaku.tia kila siku kaanguka ghafla ndugu yake anasema namtafuta Dr aje ww unaweza kweli ukaenda coco kula upepo. Huyu dogo ahojiwe vzuri.
Noma sana..
 
ila hapo pa kutoka kuwasha gari kwenda coco pana mushkeli
Mushkeli uko wap, kumbuka alikua tayar kakimbilia kujificha chooni. Mtu kaanguka unaskia kishindo. Halafu unaambiwa mtu ghafla anaumwa ngoja aje daktari, hujui anaumwa nn kwa kiasi gan, na mnaugomvi. Ungekua ni ww umefanikiwa kuchoropoka chooni utabaki ndani unamsubir tena daktari na huna uhakika kama kwel anaumwa au atazinduka ghafla.

Issue ya kwamba alienda Coco sio issue hata. Coco kuna club na sehem za refreshment (sio alienda kukaa kwenye mchanga wa bahari au kuogelea). Wenyewe walitaka aende wap sasa?

In my case I honestly buy her statements. Ni logical kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…