KESI YA MAUAJI: Utetezi wa Elizabeth Michael (Lulu) ndani ya mahakama kuu

KESI YA MAUAJI: Utetezi wa Elizabeth Michael (Lulu) ndani ya mahakama kuu

Nikiwa coco beach,meseji zilianza kusambaa zikiniuliza kwamba kanumba kafa......zilisambaaje? Ulijuaje kwamba meseji zinasambaa?
Je marafiki zake alioenda nao kwa Kanumba waliondoka muda gan?,kama sikosei kwenye utetezi wake amedai alikuwa na mtoko wa usiku na baadhi ya ya marafiki zake
 
Yulee Wakili wa serikali naona hana mpango wa Lulu afungwe maana kwa jinsi lulu alivyojitetea Alitakiwaa apigwee maswalii ya kutoshaa ya kumkabaa koo lakini mambo yameenda so smooth... Wamauachie mtoto wa watu tuu japo kiuhalisia unaona kabisa Mama kanumba ataumia maana haki kama vile haijatandekaa...
 
Nauliza tu je alikuwa ameanza mapenzi na hajafikisha miaka 18 na serikali inaliacha hilo?Kuna kitu lulu anaficha na kitamsumbua mpaka aingie kaburini,anaujua ukweli na hapa hausemi.Amefundishwa nn cha kusema.
 
Kweli Jela ni kwa Masikini tu na sio vinginevyo....
Yaani kesi ya Lulu ni kama vile yupo Location, kameza Scripts vyema huyu mtoto.

LEO NIMETAZAMA movie ya NERIA niseme wazi KILE kipengele cha Mahakama kimekaa kiuhalisia kuliko uhalisia wa KESI YA LULU.
Mahakama zetu HAZIJAWAHI KUWA HURU.
Zikiminya Wapinzani - Zinanangwa kweli kweli...Zikiminya Wanyonge -Zimetenda Haki
 
Huyo wakili **** kweli, so hayo kaona ndo maswali y kuuliza kweli, hiyo hongo imemzuzua wakili, hiv n lin mahakama zetu zitakuwa na justice???
 
Sawa, inawezekana muongo, lakini muongo kuhusu nini?

Inawezekana alikuwa na leseni ya bandia, akasema alikuwa na leseni, akajishtukia leseni haikuwa halali, akachomoa, akadanganya kuhusu leseni.

Hilo halimaanishi kadanganya kuhusu kuua.

Kwamba kakataa alikuwa namahusiano na Komba inawezekana anadanganya, huyu mtoto mdogo, Komba mtu mzima alikuwa na mkewe na watoto wakubwa kuliko Lulu. Sasa msichana kama Lulu akikataa ukweli kwamba alikuwa na uhusiano na jibaba inawezekana anadanganya, lakini je, kudanganya kuhusu uhusiano huo kunamaanisha kwamba yeye ni muuaji?

Ningeona contradiction ina nguvu zaidi kama ingeweza kuhusishwa moja kwamoja na kesi ya mauaji, siyo habari za kumharibia character tu. Mtu yeyote ukimuweka katika microscope utakuta mapungufu, huyu ana mchepuko, huyu hajalipa kodi, huyu anampiga mkewe, huyu mlevi mbwa, lakini, kama tunazungumzia kesi ya mauaji, kitu muhimu ni ushahidi wa kesi ya mauaji, si hizi habari nyingine. Unless zinaingia moja kwa moja katika kesi ya mauaji.

Kama Kanumba angefariki katika ajali ya gari ambalo Lulu alikuwa anaendesha, hapo habari za leseni ya Lulu ingekuwa very relevant.

Lakini haikuwa ajali ya gari, suala la leseni ya Lulu linakuja vipi? Sisemi kwamba halihusiki, inawezekana linahusika (sijafuatilia kesi kwa karibu). Ningependa kujua tu, linahusikaje?

Ukimchukua mtu yeyote na kuanza kumdai risiti za nguo zake zote alizonunua katika miak 10 iliyopita, utakuta kuna nguo kibao hana risiti.

Je, hilo linatosha kusema huyu ni mkwepa kodi na hivyo anaweza kuua tu?
Swali la kuendesha gari lilikuwa too technical to understand.

Swali lililofuata ilikuwa "kanumba alipokuwa anakukimbiza taulo halikuanguka?"
Concentration ya lulu ikawa imeng'ang'ania kwenye umri ndipo alipoligoliwanya.

Ilikuwa inatafutwa kauli thabiti ya Lulu ili mahakama ijue ni kivipi michakato ya mule ndani ilisababisha kanumba afe bila Lulu kukusudia!

Na kweli majibu yake yameonyesha kuwa kanumba alianguka!

Mwanguko unaonekana kuwa ni baada ya kupigwa chenga ya maudhi na Lulu, baba wa watu akaangukia uchogo ndio ikawa kwaheri!
Kwa muktadha huo ni kweli kuwa Lulu alipompiga chenga kanumba hakukusudia aanguke afe.

LULU AMEUA BILA KUKUSUDIA KUUA.

RIP KANUMBA.
 
We unasoma sheria za wapi?
huyo ulomjibu kajaribu kuelezea kitu kinaitwa Mitigating Factor...sasa wewe usichoolewa hapo ni kitu gani.na ameeleza mtizamo wake kuwa kutokana na hiyo principle ya mitigation anaweza kupunguziwa adhabu.

All in all,kwa mujibu wa sheria za Tanzania under 18 hawezi kupatiwa adhabu sawa kama adult kwa kosa lolote lile...na kinachoangaliwa ni wakati tukio linatokea alikuwa na umri gani,kama alikuwa ni mtoto atakuwa na haki zote za kimahakama/proceedings kama mtoto,this is basing on principle of the best interest of the child.

Unachemka!

Wanafunzi wa mchovu Kabudi nyinyi!

Lulu hakuwa mtoto wakati anaua, kama anavyotuhumiwa.

Hilo lilishakataliwa mahakamani kwenye pre-trial motions.
 
Unachemka!

Wanafunzi wa mchovu Kabudi nyinyi!

Lulu hakuwa mtoto wakati anaua, kama anavyotuhumiwa.

Hilo lilishakataliwa mahakamani kwenye pre-trial petitions.
Hata angekuwa chini ya miaka 18,bado sheria haimpi kinga,knga ni miaka 10 na mtoto wa kiume hawezi kuadhibiwa kwa kubaka akiwa chini ya miaka 12.
 
Mkuu ujue Maimartha wa Jesse anakimbiza 45 so usimfananishe kbs na bibie Joanah...
Mkuu sijamfananisha, nimemuuliza tu, umri wake kama Lulu au kama Maimartha?[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji124] [emoji125] [emoji125] [emoji377] [emoji377] [emoji377]
 
Back
Top Bottom