Kesi ya Mbowe: Kwa minajili ya haki Mbivu na Mbichi zote zianikwe

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kesi ndogo ya Mohammed Ling'wenya iwe nafasi ya kuzianika mbivu na mbichi zote hadharani.

IMG_20211126_052052_232.jpg

Iliyodhaniwa nia njema (ya kusaka haki tu) kuwapo japo kidogo, imeshadhihirika kuwa haipo. Si jaji si mashtaka haonekani anayewaelewa.

Kwa maana hiyo hapa sasa inabidi kieleweke. Kumwangalia nyani usoni hakupo tena.

Beberu anasema "do or die."

Kama mashtaka wanavyotumia muda kama wanavyotaka wao, hakuna haja ya haraka. Kila hoja ni lazima kuzingatiwa:

1. Kila ushahidi unaoweza kupatikana ni lazima uwasilishwe.
2. Kila anayetajwa na apandishwe kizimbani kuisaidia mahakama kutenda haki.
3. Vyote vyenye kusaidia kuthibitisha lolote e.g CCTV na rekodi tokea makampuni ya simu ziletwe mahakamani.

IMG_20211126_052207_347.jpg

Mohammed Ling'wenya ni mwana halisi wa nchi hii mwenye kustahili haki zake zote.

Mnyonge mnyongeni lakini haki zake mpeni.

-------
Kesi ya Mbowe: Madai Mahakamani yathibitishwe Kisayansi
 
Leo ni leo....
Mtobesya
Kibatala
Mallya.
Mh.Mbowe..
DPP
Mh.Jaji
Kesi Sheria(precedent)
IGP

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Akitajwa mtu hapa aitwe kizimbani. Si Urio, hangaya, Lijenje, Siro nk.

Ni Ahadi Alex, Chuma Chungulu, Mosses Lijenje, Dennis Urio nk zege hakuna kulala. Wapande kizimbani.

Si Movement Order (MO), Station Diary (SD), Occurrence Book (OB), Report Book (RB), nk ikiombwa ya popote na ije mahakamani.

Hapa kama ni kuumana mazima na iwe hivyo.
 
Mimi kila niksikiliza maneno ya utetezi. Hasa wa jana. Mwili unasismka juu ya matendo ya watu tuliowamini wangefanya nchi yangu kuwa Nchi yenye ustarabu wa kuwango cha juu. Kuna watumishi Wamekua wasaliti wa wananchi kw kiwango cha kutisha! Nmeamini huko Magerzani kuna Vilio na Mioyo ya watu imejaa majonzi sana!
 
Asante sana ujumbe umefika

Ni Ahadi Alex, Chuma Chungulu, Mosses Lijenje, Dennis Urio, nk zege hakuna kulala. Waletwe wapande kizimbani.

Kama vipi kiumane jumla lieleweke moja.
 
Mimi kila niksikiliza maneno ya utetezi. Hasa wa jana. Mwili unasismka juu ya matendo ya watu tuliowamini wangefanya nchi yangu kuwa Nchi yenye ustarabu wa kuwango cha juu..kuna watumishi Wamekua wasaliti wa wananchi kw kiwango cha kutisha!! Nmeamini huko Magerzani kuna Vilio na Mioyo ya watu imejaa majonzi sana!!

Inataka uwe zaidi ya ibilisi kujaribu kuyapita haki kina Lijenje, Urio, Adamoo, Bwire au Ling'wenya.

Makosa ya Urio nini hadi kupokea kichapo kufikia kulia kwa kuwatafutia kazi waliokuwa wakihitaji kazi ya halali?

Makosa ya wahitaji kazi ya halali ni yapi?

Utawala huu:

IMG_20211119_091739_123.jpg

Wajitathmini sana kwa kweli.
 
Mtu alielitumikia taifa kwa level hiyo leo haki zake zinachezewa hovyo kwasababu tu aliamua kutafuta mkate wake kwa njia nyingine baada ya kufukuzwa kazi jeshini, hii inaacha maswali mengi kwa wale walioko huko wakati huu.
 
Jiwe aliharibu sana nchi hii ndio maana nature iliona aondoke hata kabla ya kumaliza term ya pili kutokana na mambo haya ya hovyo aliyokuwa anaya-engineer.

Mateso waliyopitia akina Ling'wenya na wenzake ni chuki na hasira zake kuona makomando wanamlinda mtu toka chama pinzani tena CHADEMA. Naamini alijiapaza "haiwezekani wamlinde Mbowe huku wamepewa training kwa gharama za serikali" kama tu alivyowahi ng'aka kwa watu fulani kuwa mshahara wanaopokea na hata magari wanayotumia ni serikali hivyo itakuwa ni jambo la ajabu akiona/sikia wamemtangaza mpinzani kashinda uchaguzi.

Mashitaka haya na ushahidi unaotolewa ni wa kuunga unga sana kwa gundi ili tu kumzuia Mbowe asiendelee na harakati zake za kudai katiba mpya ndio maana wameibuka na kesi hii uchwara mwaka huu hali kuna watu wamekuwa ndani toka June 2020 kwa sababu za kuambatana na mpinzani, Mbowe.

Mimi ni CCM ila sipendezwi na haya yaliyofanywa dhidi ya walinzi wetu hata kama walishatoka jeshini ila bado wana nafasi kubwa sana ya kuisaidia nchi katika maswala ya ulinzi na usalama. Ila pia si vyema kuwaonea wale tunaotofautiana nao kimawazo na kiidikadi.
 
Mimi kila niksikiliza maneno ya utetezi. Hasa wa jana. Mwili unasismka juu ya matendo ya watu tuliowamini wangefanya nchi yangu kuwa Nchi yenye ustarabu wa kuwango cha juu..kuna watumishi Wamekua wasaliti wa wananchi kw kiwango cha kutisha!! Nmeamini huko Magerzani kuna Vilio na Mioyo ya watu imejaa majonzi sana!!
Huko Mahabusu watu wanateswa sana,haswa wakijua unatoka familia inapesa,wanakutesa ili uwahonge wasikutese,Kama kuna anaye bisha,ajitokeze,tumpe shahidi nyingi sana
 
Hii ccm bhana,utafikiri wao wataishi milele

Wamelewa madaraka, wanajiona wamefika, wamesahau mpanda ngazi hushuka:

IMG_20211119_091739_123.jpg

Hangaya, Majaliwa, Mpango - hawawezi kukwepa lawama kwa dhuluma zilizo kithiri magerezani, polisi, mahakamani na kwenye taasisi zao zote.
 
Huko Mahabusu watu wanateswa sana,haswa wakijua unatoka familia inapesa,wanakutesa ili uwahonge wasikutese,Kama kuna anaye bisha,ajitokeze,tumpe shahidi nyingi sana

Tupaze sauti kuukataa udhwalimu huu kwa vitendo.

Viongozi waliopo madarakani wanazikwepa vipi lawama hizi?

Cc: Samia, Majaliwa, Mpango
 
Mtu alielitumikia taifa kwa level hiyo leo haki zake zinachezewa hovyo kwasababu tu aliamua kutafuta mkate wake kwa njia nyingine baada ya kufukuzwa kazi jeshini, hii inaacha maswali mengi kwa wale walioko huko wakati huu.

Hii haikubaliki. Hiki ni cha kuumana mazima hapa hapa.
 
Jiwe aliharibu sana nchi hii ndio maana nature iliona aondoke hata kabla ya kumaliza term ya pili kutokana na mambo haya ya hovyo aliyokuwa anaya-engineer.
Mateso waliyopitia akina Ling'wenya na wenzake ni chuki na hasira zake kuona makomando wanamlinda mtu toka chama pinzani tena CHADEMA. Naamini alijiapaza "haiwezekani wamlinde Mbowe huku wamepewa training kwa gharama za serikali" kama tu alivyowahi ng'aka kwa watu fulani kuwa mshahara wanaopokea na hata magari wanayotumia ni serikali hivyo itakuwa ni jambo la ajabu akiona/sikia wamemtangaza mpinzani kashinda uchaguzi.
Mashitaka haya na ushahidi unaotolewa ni wa kuunga unga sana kwa gundi ili tu kumzuia Mbowe asiendelee na harakati zake za kudai katiba mpya ndio maana wameibuka na kesi hii uchwara mwaka huu hali kuna watu wamekuwa ndani toka June 2020 kwa sababu za kuambatana na mpinzani, Mbowe.
Mimi ni CCM ila sipendezwi na haya yaliyofanywa dhidi ya walinzi wetu hata kama walishatoka jeshini ila bado wana nafasi kubwa sana ya kuisaidia nchi katika maswala ya ulinzi na usalama. Ila pia si vyema kuwaonea wale tunaotofautiana nao kimawazo na kiidikadi.

Kwamba hata Samia anayaona haya yakiendelea na anaona sawa?

Ajue kuwa hata pesa zetu zinazotumika hovyo kwenye kesi hii kama posho tunadhani zingeweza kutumika vyema zaidi kwingine.

Ni vyema ajue hatufurahishwi unyama huu uliopitiliza kwa binadamu wenzetu.

Ajue kuwa yapo mawazo ya kuwa Lijenje na hata Urio wanaweza kuwa wameuliwa.

Ajue kuwa yote haya hayakubaliki.
 
Haki huliinua taifa

Kuna mijamaa imedhamiria kwa ubinafsi wao kuichafua hii nchi. Mijamaa hiyo imo kwenye sufuria hili:

IMG_20211119_091739_123.jpg

Pana haja ya kuwakabili hawa hadharani kuwafahamisha kuwa sasa imetosha.
 
Jiwe aliharibu sana nchi hii ndio maana nature iliona aondoke hata kabla ya kumaliza term ya pili kutokana na mambo haya ya hovyo aliyokuwa anaya-engineer.
Mateso waliyopitia akina Ling'wenya na wenzake ni chuki na hasira zake kuona makomando wanamlinda mtu toka chama pinzani tena CHADEMA. Naamini alijiapaza "haiwezekani wamlinde Mbowe huku wamepewa training kwa gharama za serikali" kama tu alivyowahi ng'aka kwa watu fulani kuwa mshahara wanaopokea na hata magari wanayotumia ni serikali hivyo itakuwa ni jambo la ajabu akiona/sikia wamemtangaza mpinzani kashinda uchaguzi.
Mashitaka haya na ushahidi unaotolewa ni wa kuunga unga sana kwa gundi ili tu kumzuia Mbowe asiendelee na harakati zake za kudai katiba mpya ndio maana wameibuka na kesi hii uchwara mwaka huu hali kuna watu wamekuwa ndani toka June 2020 kwa sababu za kuambatana na mpinzani, Mbowe.
Mimi ni CCM ila sipendezwi na haya yaliyofanywa dhidi ya walinzi wetu hata kama walishatoka jeshini ila bado wana nafasi kubwa sana ya kuisaidia nchi katika maswala ya ulinzi na usalama. Ila pia si vyema kuwaonea wale tunaotofautiana nao kimawazo na kiidikadi.
Namshukuru Mungu wetu Kwa amani aliyotujalia na utulivu wa jeshi letu,maana kuna majeshi ya nchi zingine hapa hapa Africa,makomandoo wangewafuata wenzao hao akina Adamoo,na wenzake na kuwachukua hapo hapo mahakamani mchana kweupe,bila kujali walitokaje jeshini.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom