Kesi ya Mbowe: Mahakamani kunapozidi Kumong'onyoka

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kesi ya Mbowe imekuja na mengi.

Mahakamani kulikofikiriwa kuwa ndiko kimbilio, hilo haipo tena:

Your browser is not able to display this video.


Tulianza kuzuiliwa kwenda mahakamani kunakopaswa kuwa mahala pa wazi.

Your browser is not able to display this video.


Ikaja kuzuiliwa kuingia mahakamani. Kuzuiliwa kuingia na simu. Sasa kuna kufungiana mahakamani.

Yote hayo kinyume cha sheria.

Kinara wa kuingilia mhimili huu ni kama anavyoonekana. Huyu bwana ambaye leo anaaminiwa kwa kila shitaka lake mahakamani.

Haki zipi ziendelee kutegemewa kutokea mahakamani?
 
Kujaa mahakamani hakutomsaidia Mbowe kushinda kesi yake ,waacheni wanasheria wamsaidie nao baada ya kumsaidia wanafanya maigizo na mikogo siku inatoka hukumu vilio vitatawala mahakamani ,ukiwa na kesi mahakamani jua kuna mstari mdogo sana unakutenganisha ww ,jela na uraiani .
 
Ndo maana kuna magereza, Sabaya hakuwahi kiwaza iko siku atakuwa anaugua vidonda vya tumbo akiwa nyuma ya nondo, leo anaweza kulia familia ya mbowe na wana chedema kesho ukalia wewe. Dunia inazunguka aliyeona mchana wa leo kuna posibility kubwa ya kuuona usiku wa leo pia.
Ni suala la kujipa hekima tu,
 

Akikuelewa usiache kutuletea mrejesho
 
Wewe unaogopa jela?
 
Binadamu tunajisahau sana!
 
Mimi sijaelewa ila ninachosikia ni maneno tu yanayotamkwa pasipo mpangilio ya "ana kosa gani", " "katibu wetu..." nk nk...

Ungetusaidia sana ambao hatukuwepo kwa kufanya narration ya tukio zima step by step in summary yaani;

# Lilianzaje

#Likaendeleaje

#Ikawaje na

#Na mwisho/hitimisho ikawa nini...

Lakini hii video clip pekee haitoi picha kamili ya tukio kwa mtu ambaye hakuwepo pale...
 

Nchi ngumu sana hii mjomba.

Mtu kukusanyia yote unayoonekana kuyahitaji mbona ni zaidi ya kumtaka kujaribu kumkamata Simba mkia?

Hata hivyo in a nutshell iko hivi:

Baada ya mahakama kuahirishwa, mamwela wakawahi na kufunga mlango wa kutoka kwenye chumba cha mahakama, ili watu wasitoke kwenda kumuaga Freeman Mbowe.

Baada ya kina Mbowe kuondoka ndipo makuda wakarejea kuja kuufungua mlango. Makabiliano ndipo yalipojiri.

Unayosikia ni kuwa askari Magereza anamueleza John Mnyika, "tutakubeba."

Mnyika naye anajibu, “siogopi kubebwa, nibebe hata sasa kama unadhani naogopa”

Hadi hapo nadhani panakupa picha kamili ya mazingira mazima tuliyomo.
 
YES, umeeleweka. Na nimeelewa vyema..

Asante sana
 
Kwani kufuatilia kesi hii ni kosa??? Je watu wakijaa Mahakamani wataizuia ishindwe kuyatekeleza shughuli zake kisheria??

Kwanini mnapenda mambo ya gizani???
 

Tulioko nje tunapata wakati mgumu sana kutangaza Tanzania kwasababu ya kesi za kijinga jinga hivi. Kila mtu anaona huu ujinga ambao kwa nchi hata zambia tu! Umepitwa na wakati. Siku hizi nchi zina ringia maendeleo na demokrasia sio mambo ambayo hayamnufaishi mtu yeyote.
 

Wadanganyika wasichokiona ni kuwa Zanzibar wao wamekuwa wamoja. Kina Jussa waliovunjwa mabega hayo yalikuwa zamani.

Huko hakuna ugaidi wala nini wanavutia wawekezaji na wadanganyika wataijenga Zanzibar hadi waote vibiongo.

Si kina Jussa tu, hata Seif na rais JMT mzanzibari ngoma ilikuwa inogile.



Zanzibar sasa ndiyo Chatto.

Mwinyi njia moja rais JMT 2030. Kijiti kitoke vipi Zanzibar?
 
Kwamba Askari magereza nayeye anakamata watu siku hizi? Nimependa ulisema wakuda wakafunga mlango
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…