Nasikia watu wakitolea mfano nchi kama Ethiopia ambao wana madege mengi kutuzidi, flyovers zaidi na bwawa kubwa zaidi. Of course huenda mgogoro wao unachochewa na kusisitiza ujenzi wa bwawa na Misri wakawaambia "tutaona".
Kikubwa ni kwamba mfumo wa utoaji haki kupitia mahakama ni mzuri sana hasa ukishaaminiwa na watu wa kawaida, lakini ikitokea watu wakakata tamaa nao ni lazima wapate suluhisho la kupata haki kwa njia yoyote ...iwe ya kimya kimya au kwa kupiga makelele.
Kesi nyingi walizohukumiwa wapinzani watu waliona wazi kuwa ni uonevu na hata walivyokata rufaa baadae (japokuwa unaweza kudahni ni katika mahakama zilezile) hukumu zilibatilishwa. Rais wa sasa alipoingia madarakani alisema wazi wazi kuwa ubambikaji wa kesi ni wa kiwango cha juu sana. Kibaya zaidiile misemo ya "hatuna haja ya kuendelea na kesi" inaonekana kawaida lakini tusubiri matokeo yake
Ukiangalia Kenya mfano Willy Mutunga ni mwanaharakati wa kawaida kwa sasa baada ya kuwa Chief Justice, kwa hiyo na aliyepo sasa anajua atakuwa benchi kwa mujibu wa sheria. Haihitaji kumlamba mtu viatu bali kutendea haki walichokuwekea hapo.