Kesi ya Mbowe: Mahakamani kunapozidi Kumong'onyoka

Naona safari yetu inazidi kuwa ndefu kila kunapokucha, wameshindwa hoja, wameshindwa kutafsiri sheria, sasa wameamua kuwa wababe, nani wakuwazuia na huu ubabe wao?

Wao wana marungu, magereza, maji ya kuwasha, mabomu ya machozi, majaji, mahakama, kufungiwa mahakamani kama kuku, na ikibidi risasi za moto kama walivyomfanyia Mbowe pale Kinondoni Mkwajuni, ila Mungu akamnusuru.

Nikiangalia hii hali kwa undani, kumbe sisi ni mateka; tunatawaliwa na serikali ya CCM, hatuna pa kukimbilia, hatuna marungu, mabomu ya machozi, majaji, na mahakama zetu kama wao, tumaini letu limebaki wapi? au tuendelee kuishi kwa matumaini tukiamini iko siku?

Naona wameshatuzoea hatuna chakuwafanya zaidi ya kulalamika mitandaoni, ndio maana wanazidi kukandamiza haki za wengine kwa makusudi ili waendelee kujinufaisha kwa maslahi yao, tunaitwa taifa la kidemokrasia ya vyama vingi bila ya uhalisia wowote, kwani wao hawataki kushindwa.
 
Tunalo lundo la vyuo chini ya TCU lakini kimekosekana hata chuo cha VETA kikamtunuku walau kasatifiketi Kipanya, badala yake wanagawa PhD na uprofesa kama njugu kwa wasiostahili kabisa. Mmoja miaka kadhaa iliyopita alipewa uprofesa lakini hata yeye anaona aibu kuitwa prifesa.
 
Pole sana, "Haki sio tuu ni lazima itendeke, bali pia ionekane inatendeka".
 
Wanasheria wake ndio wanampigilia msumari wapiga deal hao
 

Mkuu hakipo kisichojulikana:

Tuutambue mzizi wa machungu yetu nchini

Hali kadhalika tufanye je? Yapo masomo ya kutosha pia:

Katiba Mpya: Kulikoni Makamanda na ndugu Wananchi Kusita Sita?

Machinga wanapotoa Somo, Makamanda tunakwama Wapi?
 
Inasikitisha na kuudhi sana ukiona huu udhalimu unaozidi kukithiri nchini.



 
Tunapoelekea itazuiliwa kuingia wala kuripoti kinachoendelea mahakamani, hakuna mtu anaependa kuaibika.
 
Hivi hamna kazi ya kufanya nyie CHADEMA
 
Inasikitisha na kuudhi sana ukiona huu udhalimu unaozidi kukithiri nchini.

View attachment 2001123

Zanzibar behind the scene yaonesha wameelewana kutucheza shere na kukishikilia kijiti kwa kadri itakavyowezekana.



Jussa ni kama unavyomwona hapo. Huyo alivunjwa bega.

Usishangae hapa wadanganyika tutaijenga Zanzibar sasa hadi tutoke vibiongo. Chatto sasa ni Zanzibar. Kazi na iendelee.

Usishangae hapa kuna kijiti kinapigiwa mahesabu si kabla ya 2040.

Usishangae hata Seif angekuwapo na rais wa JMT mzanzibari hali ingekuwa hivi hivi.

Kwao wanaongea maridhiano kwetu je?
 
Halafu eti tuna mtu kakaa hapo anajiita CJ, Rubbish!
 
Hata chief Hangaya, Majaliwa na Mh. Mpango hawadhani hala hala zinaweza kuwahusu.

Nani aijuaye kesho? Kwanini kama binadamu tusitendeane haki na usawa tu?
Nitakapokuwa rais mwaka 2035 kolikoli nao mahakamani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…