Barua hii kumhusu Komando Ling'wenya itakuwa imeutafsiri uwanja mzima rasmi kabisa kwa jinsi ulivyo.
Hakuna kisichofahamika tena. Hii ni vita kamili.
Vita vya haki dhidi ya dhuluma. Vita vya wanaoyathamini maisha ya akina Luteni Urio, Moses Lijenje na wenzao, dhidi ya wabinafsi waliopitiliza.
"Vita ni vita Mura!"
Tumesikia "mahakamani si kwa mama zetu." Bila shaka "mahakamani ni kwa mama zao." Wao kumbe pia ni mawakili wa mahakama.
Zimeombwa tu, Movement Order (MO), Station Diary (SD) na Occurrence Book (OB) kwa ajili ya kumkagua D/C Msemwa. kimeumana! Hakuna kuwaachia hawa.
"Waombeni pia na ma CCTV recordings njia yote RAU - Moshi - Arusha - Dar - Mbweni. Pia data kama hizo tokea makampuni ya simu."
Ipelekwe miito ya kuwaita wote na vyote vinavyoweza kusaidia kuthibitisha lolote. Asiachwe mtu au kitu tafadhali.
Iwe ni Hangaya, Sirro, Urio, Ahadi, Chungulu, Sabaya, Lijenje, nk. Tuonane Kizimbani. Vigezo na masharti yakizingatiwa.
Wanahofia nini nyendo za D/C Msemwa kuhakikiwa?
Si kwa sababu kuwa: "the guilty are always afraid?"
--------
Kesi ya Mbowe: Kwa minajili ya haki Mbivu na Mbichi zote zianikwe