Jambo la kupongezwa kuona mawakili wa utetezi wakipambana vilivyo kuona haki za washitakiwa haziporwi.
Hata hivyo inashangaza ni kwa motisha gani upande wa mashtaka kupambana kikuku kuona ikiwezekana washitakiwa hawapati haki zao.
Faulo za upande wa mashtaka ziko nyingi na ziko wazi:
1. Kwenye shauri la Adamoo wakiwa wameahidi kuleta shahidi wao mwingine, walifunga sehemu yao ya ushahidi ghafla asubuhi asubuhi. Hatua hii ikawawekea shinikizo utetezi kuanza bila kutarajia na (labda) bila kujiandaa kikamilifu.
2. Leo wakiwa pia wameahidi kuleta shahidi, wamefika mahakamani wakiwa wamechelewa na ghafla bila kutarajiwa wakafunga sehemu yao ya ushahidi. Kama #1 wakawaweka upande wa utetezi katika kuendelea na kesi.
3. Si mara moja, wakiamua hupoteza muda ili kesi iahirishwe kwa maslahi yao. Wamefanya hivyo pia leo.
4. Wao hukomaa kweli kweli ili kuingiza exhibits zozote hata kama ni zenye utata mtupu.
5. Wameonekana kukomaa pia kuzuia kata kata Ling'wenya asiwasilishe chochote kinachoweza kumsaidia katika lolote analoshtakiwa.
Hali hii kibinadamu inashangaza na kutia kichefu chefu. Hasa ikizingatiwa kuwa wanafanya hivi kinadharia kwa niaba yetu.
Izingatiwe Ling'wenya ni komando aliyelitumikia taifa hili na hawa jamaa ni watu wanaokula kodi zetu mahotelini pasipokuwa na ridhaa zetu:
Hivi kwani, hawapo mawakili wa serikali Dar? Au hizi per diem ni sehemu ya motisha huo?
Au hawa ndugu wana ahadi fulani fulani zenye kufungua fursa zaidi kwao?
Walisema kua uyaone: "haki za watu zinapogeuka kuwa bidhaa kama nyanya tu, gengeni."
Utetezi: "Kwa mustakabala huu chonde chonde, hakuna kimwangalia nyani usoni."
Ushahidi wa kisayansi ni takwa la msingi wala si ombi tena. Jiwe moja lisibakie juu ya jingine.
---------
Kesi ya Mbowe: Madai Mahakamani yathibitishwe Kisayansi