Kesi ya Mbowe na wanasheria wa Tigo na Airtel ikumbushe wenye mamlaka kutunza siri za wateja ni muhimu kujenga sekta imara ya benki na mawasiliano

kama wewe sio Gaidi unaogopa nini??!!
 
Hata mimi nimeshangazwa sana. Kwa wenzetu, ni lazima kuwepo na amri ya mahakama. Yani uchunguzi umefikia mahali ambapo mahakama inaona ni sahihi taarifa hizo zikatolewa. Lakini hapa kwetu ni polisi tu akiamua anapewa hizo taarifa. What a stupid country.
 
kama wewe sio Gaidi unaogopa nini?
magaidi ndio watakao ogopa maana wana tumia vibaya mawasiliano.
 
Aiseee pole kama ndiyo unajua leo,wengi kuongea mambo ya siri/Madili wanatumia whatsapp call au Facebook call.....Mwendazake alienda mbali hadi kurekodi maongezi na kusoma meseji za watu aliowatarget.
 
Sheria inasema taarifa inaweza kutolewa kama mtumiaji wa simu anatuhumiwa kutenda kosa fulani. Lakini uthibitisho uliotolewa leo ni kwamba polisi hawaelezi hata sababu, na tigo hata hawaulizi taarifa inahitajika kwa sababu gani.
Kaka km unacho kile kielelezo cha barua kutoka polisi kwenda tigo tuwekee km hawakutoa sababu maana wakili wa utetezi alisema visisomwe ila aongozwe tu kwa kuwa vitachukua muda mrefu
 
Sheria inasema taarifa inaweza kutolewa kama mtumiaji wa simu anatuhumiwa kutenda kosa fulani. Lakini uthibitisho uliotolewa leo ni kwamba polisi hawaelezi hata sababu, na tigo hata hawaulizi taarifa inahitajika kwa sababu gani.
Hili ndio tatizo na weakness ya huyo shahidi aliodhihirisha leo mahakamani. Pili alipaswa ashirikishe uongozi wa kampuni katika kudisclose customer's infos.
Labda aliwekwa TIGO na mfumo kwa kazi maalumu who knows.?
 
TIGO WAMEPELEKA MTU FAMBA, AMEHARIBU IMAGE YA TIGO.....TIGO MLIPENI CHEQUE YAKE AONDOKE....AMECHAFUA
 
Hao watu (mamlaka) wanaopewa taarifa ni kwa mujibu wa sheria zilizopo.
Kuna mamlaka hazinyimwi hizo taarifa
sheria zipo zinazi guide hivyo vitu
 
Hao unadhani wanajielewa basi
 
Ina maaana hata kina nape na januari na kinana hawakulijua hilo
 

ni upuuzi kiwango 1000% kudhani kwamba mtandao utaheshimu faragha za mjinga mmoja dhidi ya serikali,hakuna nchi ya hivi,haipo.
zipo policy kati yako,mtandao,na serikali kama utatu mtakatifu katika biashara,lakini kuna policy kati ya mtandao na serikali.

wewe mkuu ukiua,ukahitajika ushahidi kutoka katika simu,polisi ambao ni sehemu ya serikali wana mamlaka ya kwenda tigo au kwingine wakapewa mkeka wote wa mawasiliano yako,na huwezi kuja hapa unalalamikia faragha kwamba umesalitiwa na mtandao husika,maana utaonekana kichaa.

hao wahanga unaojaribu kuwataja ni kundi hili hili la kwako wanaoamini kutumia mitandao kuna ngao sababu ya sera ya faragha kutoka mtandao husika,unapiga majungu mkuu wa nchi kwenye simu[emoji1787][emoji23][emoji1787].

melo mwenyewe labda sababu hawezi kukwambia kakabidhi nini kwa kazi zipi,ndio maana unaandika hapa,vinginevyo angeeshakula ban saa hizi usijue hata jf iliishakuwepo.
 

mambo hayako namna hiyo.

amri ya mahakama haiko mitandaoni huko,kasome sheria mpya ya uhalifu wa mtandao.
watu walilalamika mamlaka kushushwa chini mpaka kwa wakuu wa vituo tu.
 
mambo hayako namna hiyo.

amri ya mahakama haiko mitandaoni huko,kasome sheria mpya ya uhalifu wa mtandao.
watu walilalamika mamlaka kushushwa chini mpaka kwa wakuu wa vituo tu.
Haujui kitu fanya uchambuzi wa kina utajua
 
kama wewe sio Gaidi unaogopa nini?
magaidi ndio watakao ogopa maana wana tumia vibaya mawasiliano.
Faragha ya mtu siyo uhalifu tu. Au kwako, hata serikali au kampuni wakisema hii ni confidential au classified information, basi ni ugaidi?
 
Makampuni mengi ya simu yana bahati ya kufanya kazi katika nchi zenye watu wengi wajinga ila ingekuwa kwenye nchi zilizoendelea leo tigo hisa zao zingeshuka tu kumbe kwao suala la privacy siyo kipaumbele chao kbsa kwa mteja wao shame on them
 
Kuna sehemu anasema wao mtu yeyote akipata barua toka Polisi kuhusu kuchunguzwa kwa mtu hawaangalii chochote.
Hii tunaita ufanyaji wa kazi wa mazoea. Bila kuzingatia kanuni na Taratibu za kampuni yao zilizopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…