Kesi ya Mbowe na wenzake inaanika hadi 'mambo ya siri za nchi'. DPP hujachelewa kuifuta


Kwenye katiba mpya tuongezee hili:

"Mambo ya siri za serikali dhidi yetu hatuyataki."

Kuendeleza haya ya siri za Baraza la mawaziri ndiyo yaliyotufikisha huku.

Hivi serikali kama ni yetu inakuwa je na siri dhidi yetu?

Simon Sirro:

"Tunawataka Moses Lijenje na Luteni Urio wakiwa hai kutokea mikononi mwako."

Vivyo hivyo itatupa Ben Azory Mawazo na utatwambia waliaomuru, kuratibu na kutekeleza shambulizi la Lissu.
 
Ngoja inyeshe tujue panapovuja. Kumbe polisi wamepewa madaraka mpaka ya kutesa makomandoo wa JWTZ ? Wallahi sikujua...
 
Kwenye hili suala la kuwepo wanajeshi vituo vya polisi hata mimi limenistua,na huyo shahidi anasema hao wenzie nao walikamatwa kwa kesi hizo hizo za ugaidi,kulitokea nini huko jeshini?!

Yule shahidi anasema aliona Luteni Urio akiteswa na wanajeshi wa special forces(aliokuwa nao kambi moja so anawajua) pamoja na polisi kwenye magari mabovu pale Tazara police.
Na mimi nimeamini kabisa ushahidi huu maana sidhani kama wanajeshi wangeweza kukamatwa na kushughulikiwa bila kuhusisha wajeda wenzao.Sasa nini kilitokea huko jeshini?
Kuna nini pia kwa wanaostaafu huko jeshini?

Pili,ni kwanini kesi hii imeachwa wazi hivi huku inaonekana kama inakwenda kureveal vitu vizito dhidi ya serikali ambavyo si busara kuviweka hadharani?
Naamini kabisa tiss wangetaka iwe kimya kimya wasingeshindwa kwa mvua kwa jua na hii kesi isingekuwepo kabisa in the first place,lazima ingefutwa kama ni Mbowe na Chadema wangetafuta namna nyingine ya kudeal nao.

Hii kesi naishangaa sana.
Kuna smokescreen gani hapa?!
 
Yaani DPP afute kesi kisha magaidi watoke nje waendelee na njama zao haramu za kupanga mikakati ya kuhatarisha Amani ya nchi yetu??!!
 
wenye akili zao hawewezi kuamini maneno ya uongo ya Ligwenya/ Adamoo, huyo ni mtuhumiwa wa Ugaidi anaye daiwa kumtumikia mtuhumiwa Mbowe.
kama walidhani wanaweza kupoteza amani yetu ya Tz basi wajue amani ya Tz lazima ilindwe kwa gharama yoyote ile.
Mbona wewe umeshahakikisha tayari wakati wote ni watuhumiwa?
 
Hili halina shida, ndio kiu
wenye akili zao hawewezi kuamini maneno ya uongo ya Ligwenya/ Adamoo, huyo ni mtuhumiwa wa Ugaidi anaye daiwa kumtumikia mtuhumiwa Mbowe.
kama walidhani wanaweza kupoteza amani yetu ya Tz basi wajue amani ya Tz lazima ilindwe kwa gharama yoyote ile.
Ila kwa huu ushahidi wa polisi kuna ndoto ya hiki unachokisema kutokea?
 
inawezekana kuna mambo ya ndani sana inapofika issue ya wanajeshi wengi kuhusishwa hata kuteswa kwenye vituo vya polisi...Hawa wanajeshi wanaingia kwenye kesi ya Mbowe, na kama kweli ni hivyo,Je Mbowe na jeshi uhusiano wao kwanini ulikuwa mkubwa kiasi hicho...

Simtetei yeyote hapa najaribu kuwaza kwa upana kidogo kulingana na mtoa mada hapo juu...
 
Hili halina shida, ndio kiu Ila kwa huu ushahidi wa polisi kuna ndoto ya hiki unachokisema kutokea?
Mimi sijui, Jamuhuri ndio inajua zaidi.
wewe endelea kusikiliza kesi mpaka mwisho wake.
sikiliza hadi shahidi wa mwisho.
hadi wa mwisho.
hadi wa mwisho.
hadi wa mwisho.
 
kichwani zimo? wewe ni mjinga na una akili.
 
Mbona wewe umeshahakikisha tayari wakati wote ni watuhumiwa?
angalia vizuri juu ya comment nimesema mtuhumiwa/watuhumiwa.
bado ni watuhumiwa.
tuache kelele mingi, ngoma bado mbichi sana.
ndio kwanza trela picha lenyewe halijaaanza
 
inaonesha serikali hawakujua kibatala anaweza akachimba mashitaka na kupelekea uzalishaji wakesi ndogo ndani yakubwa
 
Mbowe na wenzake maji ya shingo, sasa wanatapatapa.
walidhani kuchezea amani ya nchi ni masihara!! ebo!!
Daaaa Ama kweli duniani Kuna vioja
Gwajima njoo uchukue msukule huku Kwa maombezi ya wiki la ufufuo na uzima katika jina la Yesu wa Nazareth
Amina!
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Na mara mara nyingi moto huanzia chini kupanda juu
 
Amani ya nchi yoyote ile hulindwa kama mboni ya jicho.
sasa ole wake ujaribu kuchezea amani ya nchi utajuta!!!
unaweza kuchezea kitambi chako au kidevu chako lkn kamwe usijaribu kuchezea AMNI ya Nchi.
 
Na wote waliokamatwa na kuteswa ni kj 92,special force (makomandoo tupu)
Kingai na Mahita hiiiiiiiiiiii!
Samahani. Jamani niulize hawa akina Adamoo, Lingwenye, na Moses WALIKUWA WANAJESHI au ni WANAJESHI. Kwa maana WALIFUKUZWA JESHINI au WAPO JESHINI HADI LEO?
 
Amani ya nchi yoyote ile hulindwa kama mboni ya jicho.
sasa ole wake ujaribu kuchezea amani ya nchi utajuta!!!
unaweza kuchezea kitambi chako au kidevu chako lkn kamwe usijaribu kuchezea AMNI ya Nchi.
Unapata tabu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…