Kesi ya Mbowe na wenzake inaitesa Serikali, inawatesa viongozi wa vyama na Serikali na inatutesa raia wema kuliko inavyomtesa Mbowe na wenzake

Utaliamsha lakini watu watapigwa mapanga vichwa na viwili wili vitatenganishwa. huwajui ccm wewe. Wana nguvu nyingine nje ya chama cha siasa.
 
Umeandika vyema sana sana, kwa uweledi mkubwa na hisia za ndani sana kiongozi. Kiroho sana mkubwa....
 
Naona umelikamilisha andiko lako kwa maono ya kidini. Kwa mtazamo wangu ambaye sina chama cha siasa na kwa kutazama historia ya Tanzania iliyoheshimika katika mataifa, pia nikitazama sifa za viongozi 3 walioiletea sifa Tanzania yaani Mwalimu, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa naona walikuwa na sifa mbili muhimu: 1.Intelligence Quotient (I Q) zao zilikuwa za juu.
2. Emotional Quotient ( EQ) zao pia zilikuwa kubwa.
Kwa sifa hizo 2 haingewachukua muda kugundua au kusikia sauti ya wengi kuwa Tanzania inakoelekea siyo sahihi kwamba tutesane, tupigane risasi au tuibiane kura za wananchi sisi kwa sisi! Haihitaji akili kubwa. Iweje hii hali iruhusiwe kuendelea hata kwa juma moja!? Hii kweli ni Tanzania iliyoshinda vita ya Idd Amin. Kweli Watanzania tumesahau ule mshikamano wetu ambao hata majasusi tuliwavurumisha? Siasa ni sawa na Klabu za mpira mithili ya Simba na Yanga. Siku ambayo Klabu bingwa itaanza kuwafunga jela na kuwatafutia simu wachezaji wa timu pinzani Timu ya Taifa ya mpira wetu itakuwa ni timu ya taifa kweli? Kiongozi ye yote wa taifa ni mlezi wa taifa zima, hivi hili jambo linahitaji sheikh au Bishop kumweleza Rais? Yeye mwenyewe hata bila ushauri hawezi kuliona kuwa tuendavyo siyo sahihi!?
 
Na Mbowe anaweza kuondolewa akaokolewa mtu na Mungu huyo huyo .
Historia ya tangu na enzi inaonyesha kwamba Mungu ana kawaida ya kuwaondoa wanaoddhulumu. Kwa hio katika hili jiulize ni nani anaedhulumu? Kama ni Mbowe ndie anaedhulumu basi ni kweli kwamba Mungu ndie atakaemuondoa. Ila kama ni kinyume chake basi elewa kwamba Mungu anajuwa ya siri na ya dhahiri na hana upendeleo na wala hana chama!
 
Utaliamsha lakini watu watapigwa mapanga vichwa na viwili wili vitatenganishwa. huwajui ccm wewe. Wana nguvu nyingine nje ya chama cha siasa.
Wananchi wa Sudan waliweza. Serikali ya Bashir ilikuwa ni kitu kimoja na jeshi lkn wananchi waliamua na wakaweza kumuondosha Bashir.

Labda tuseme tu muamko wa watanzania bado uko chini mno. Wanadhani Mbowe anayapiyia yote haya kwa faida ya familia yake
 
Mimi ni Stuxnet Wala Sina uhusiano na huyo gentamicin OD. Muache gentamicin OD mwenyewe akuhakikishie Wala sijawahi kupambana na Numbisa.

Nina mawazo yangu huru yanayojitegemea
 
Kwa iyo Maalim Seif alimvulumu nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…