Wakuu, nikili kuwa nmefuatilia kwa karibu Sana kesi ya m/kiti wa CHADEMA Mh. Freeman Mbowe na wenzake toka ianze mpaka Leo, kipindi chote hicho nlikua naelewa kilichokuwa kikiendelea na namna ambavyo safu zote ( yaani upande wa mashtaka na upande wa utetezi walivyotupa taswira ya mambo).
Lakini Leo, baada ya wakili msomi Peter Kibatala kumaliza kumhoji mshitakiwa Adamoo na Jaji kumpa uskani wakili wa serikali (mashtaka), kwa kweli nmetoka kapa, nadhan hata mshtakiwa mwenyewe alikua haelewi maswali ndo maana alikua anaomba yarudiwe, Jaji nae vivyo hivyo!
Kwa kuwa tunazidiana uwezo wa kufikiri, je , Wenzangu mmemuelewa wakili wa serikali alikua anauliza Nini?
Kama uliipata picha ya ndugu wakili, tujuzane hapa tafadhar!