Kesi ya Mbowe na wenzake: Makomandoo 'wanaonewa'

Kesi ya Mbowe na wenzake: Makomandoo 'wanaonewa'

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,137
Reaction score
17,908
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi kuendelea kufuatilia kesi inayomkabili Mbowe na wenzake watatu. Leo sikuweza kwenda kwakuwa ninatarajia kusafiri hivi punde. Nimemsikia na kumuona Luteni Denis Urio akitoa ushahidi wake. Nimemsikiliza kwa makini na kwa kutaka kumuelewa. Ameeleza mengi kumhusu Mbowe na wenzake watatu walio mahakamani na mmoja ambaye hayuko mahakamani: Komando Lijenje.

Luteni Denis Urio, akitajwa na ACP Kingai na wengine, ndiye kiini cha kesi ya Mbowe. Ndiye mtoa-taarifa wa kwanza kuhusu njama za kutenda makosa ya jina: ugaidi na kudhuru viongozi wa kiserikali. Luteni Urio ndiye anayedai kupeleka taarifa za uhalifu wa kijinai kwa DCI na hata mengine kufuata baada ya hapo. Leo anaendelea kutoa ushahidi wake mahakamani. Mimi siusubiri ushahidi wa leo. Wa jana unanitosha na kunitisha.

Luteni Urio amepasua jipu namna alivyowatafuta na kuwapata makomandoo wanne:Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Lijenje. Kila mmoja alikuwa kwenye harakati zake za kimaisha. Harakati halali zisizo na dalali. Alikuwa kipambana kivyake ili kujikimu na kutunza familia yake. Huyu huku, huyu kule. Hii ni baada ya kuwakuta kilichowakuta jeshini (ukweli wanaujua wao wenyewe na Mungu wao).

Wakatafutwa. Wakataarifiwa kuwa kuna kazi ya ulinzi. Wakashawishiwa kuikubali. Wakakubali. Wakapewa na pesa ya kusafiria na kujikimu. Wakaenda mahali pa kupata kazi. Waliambiwa waseme kinachoendelea huko na wakawa wanasema ( mmoja alikuwepo Dar na akasema kinachoendelea). Kama vijana wenye nguvu na maarifa, waliambiwa kuhusu kazi. Wakaitamani na kuikubali kwakuwa kwao ulinzi ni jambo la kawaida. Wakaenda.

Walipokuwa huko walipoambiwa waende, wakavamiwa na kukamatwa kwa kutaka kutenda ugaidi na kudhuru viongozi. La haula! Hayo yalitokea wapi tena? Je, Luteni Denis Urio aliwatengenezea wenzake kesi labda kwa visasi vyao binafsi wakiwa jeshini? Je, iweje waliotafutwa na kuambiwa waende walikokwenda kwa kazi ya ulinzi waende halafu wakakamatwe hukohuko walikoambiwa waende? Hawa makomandoo watatu waliopo mahakamani na ambaye anatafutwa 'hawana kosa lolote'.

Nani angeacha kuifuata ajira ikiwa ana nguvu, maarifa, ujuzi na shida ya ajira husika? Wasibagazwe kwa harakati zao za kimaisha.

Wasiojulikana sasa wamejulikana!?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (safarini kwenda Dodoma)
 
Kama alitokuwa anasema Urio ni ukweli... Basi Urio ni mshenzi sana. Wenzake walikuwa wanapambana na hali zao, yeye anaenda kuwaingiza kwenye matatizo makubwa.
Unaweza kukuta Urio na Mbowe wana jambo lao.

Ogopa sana Machame.....Ole imekula kwake!
 
mtu mbaya kabisa hapa ni mbowe ndiyo amewasababishia shida makomandoo unafikiri bila hao makomandoo kuja kwenda kwa mbowe dhamira ovu ya mbowe isingejulikana na walikamatwa mapema ili mbowe asije akatenda uovu wake
 
hata hao makomandoo wenyewe pia wana matatizo, wanajua kabisa kwamba hiyo kazi waliyopewa si halali kwanini walikubali kuifanya wakati walishaonywa na Urio kwamba wale walishakua na kiapo kwaiyo kama kazi itakuwa ni ya uhalifu waachane nayo?
 
Huyu jamaa ametenda dhambi mbaya sana. Sijui kama wenzake watakuja kumsahau achilia mbali kumsamehe. Yaani unaharibu maisha ya wenzako wasio na hatia hivihivi. So sad!
 
Baada ya kuona amekuwa mwenyekiti wa kudumu Mboe aliamua kukigeuza chama kama kampuni yake binafsi na kuanza kukitumia chama kama kichaka cha kupanga mipango ya kihalifu dhidi ya Serikli/nchi.
tulimshauri mara kadhaa ang'atuke lkn aliye diriki kugombea nafasi hiyo aligeuka kuwa adui wake!! kumbe alikuwa na agenda za kimafia dhidi ya serikali.
sasa yamemkuta.
 
Wewe ni mburundi hata usijue yanayoendelea kisutu ?
 
mtu mbaya kabisa hapa ni mbowe ndiyo amewasababishia shida makomandoo unafikiri bila hao makomandoo kuja kwenda kwa mbowe dhamira ovu ya mbowe isingejulikana na walikamatwa mapema ili mbowe asije akatenda uovu wake
mmh,sijui kwa nini usiende mahakamani kuthibitisha hiyo nia ovu ya mbowe maana kwa maneno yako inaonekana wewe una uthibitisho ambao mahakama inahangaika kuupata. okoa muda wa mahakama na fedha za watz nenda kathibitishe tuachane na hili jambo tuendelee na mengine
 
hata hao makomandoo wenyewe pia wana matatizo, wanajua kabisa kwamba hiyo kazi waliyopewa si halali kwanini walikubali kuifanya wakati walishaonywa na Urio kwamba wale walishakua na kiapo kwaiyo kama kazi itakuwa ni ya uhalifu waachane nayo?
Hivo umesikiliza hiyo kesi, Urio anasema hawa watu aliwatafuta kwa kazi ya ulinzi so ugaidi. Wao walijua wanaenda kufanya kazi ya kumlinda mbowe. Sasa kosa lao hapo ni lipi
 
Back
Top Bottom