Fundi Madirisha
Senior Member
- Jun 30, 2020
- 184
- 988
Katika jambo kubwa ambalo nafikiri wengi hawaliongelei na hawataki kulielewa huenda labda ni makusudi waone kuna kitu gani mwishoni ni kuhusu mwenendo mzima wa kesi ya Ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa taifa wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe. Kuna mtego mwingine mkubwa kwenye hii kesi na watakaoumia zaidi ni CCM na serikali wanayoongoza. Kwa viongozi wenye kutazama mbali zaidi wangeachana na hii kesi, mwisho wake si mzuri.
Kiukweli kabisa majibu yeyote yale kwenye hukumu ya kesi hii hayataiacha CCM na serikali yake salama kisiasa, labda watolewe kafara watu wachache waliofungua hii kesi ili kuweka balance kwenye mitazamo ya Watanzania.
Maana Mbowe mpaka sasa kila mtanzania hata asiyependa anajua kua alikamatwa kwa sababu ya kongamano la kudai katiba mpya, kwahiyo hata akifungwa ni katiba mpya ndiyo itakayomfanya na siyo ugaidi maana mpaka sasa ushahidi unaotolewa mahakamani unajikanganya na hata hisia za ugaidi hakuna.
Kwahiyo, itaamka ari mpya ya watu kudai katiba mpya na hawataogopa wataona ni bora nao waende jela kama Mbowe, hili vuguvugu litawagawa sana watanzania na hawatazielewa mamlaka. wakifuta mashtaka watakaolaumiwa ni Polisi na serikali kwa ubambikiziaji kesi na itaonekana kwamba suala la katiba mpya ni la msingi ndiyo maana Wanawasumbua wapinzani, kwenye hili atakayepewa umaarufu ni Mbowe na chama chake.
Bado hata Mhe Mbowe akishinda kesi hii itaonekana ni ya uongo na kubambikiwa na kuamsha hasira za wananchi na kuichukia serikali yao. Kwa vyovyote vile matokeo yeyote ya maamuzi ya kesi hii si mazuri, huu mtego ni mbaya labda itafutwe namna nzuri ya kulimaliza bila kuathiri upande wowote. Sasa inaonekana kua taifa liko kwenye mgogoro wa kikatiba kwa sura ya nje na ndani.
Huu mtego kwa Mbowe anahangaishwa kwa sababu ya kudai katiba mpya ni kitu ambacho hakikuwepk tangu nchi hii ipate Uhuru, ngumu sana kuingia akilini kumshtaki kwa tuhuma za ugaidi mtu ambaye hana rekodi zozote za kushiriki mauaji au kitendo chochote cha utovu wa nidhamu. Kwanza ni dhambi mbele za Mungu Mola maana atashusha laana kwa watawala na wahusika wengine.
Kuna wanaodhani kuwa kesi ya Mbowe ingeweza kuzima vuguvugu la madai ya katiba mpya ambayo ina maslahi kwa watanzania wote lakini wamesahau kua kutajwa tajwa kwa hii kesi ndiyo kunachochea neno Katiba Mpya kutajwa sana maana ndivyo inavyo hukuliwa kua Mbowe ana kesi kwa sababu ya kudai katiba mpya na ugaidi juu yake ni vitu vya kufikirika.
Hii kesi ni mtego mkubwa sana kwenye uwajibikaji wa kusimamia shughuli za maendeleo nchini, suala la kisiasa halimalizwi kwa kumweka mtu jela, alikaa sana jela Rais Hichilema wa Zambia, kina Raila Odinga, kina Hayati Mandela kwa kesi za uongo na kutunga lakini walitoka.
Naishauri CCM na serikali watambue kua CHADEMA wana wanachama zaidi ya milioni 8 kwa takwimu zao, hii idadi si ndogo wapime madhara yanayoweza kuwakumba baadaye.