Nasema kwa kulazimisha kwa sababu Kila mtu anajua Mbowe sio Gaidi.
Kingai anajua,
Mahita anajua,
Jaji Siyami anajua,
IGP anajua CCM wanajua,
Mashehe,Mapadri,wachungaji mitume na manabii wanajua.
Watu wengi makini wanajua Mbowe sio Gaidi.
Kama ni kweli alitaka "kumdhuru" Sabaya Basi huo sio Ugaidi bali ni uhalifu wa Kawaida kabisa,ingefaa ashitakiwe kwa kosa la kutaka kumdhuru au kumuua Sabaya lakini sio Ugaidi.
Ugaidi ni kosa kubwa mno hapa Duniani na lina Sheria zake namna ya kutambua kuwa kosa hili ni Ugaidi ama kosa hili ni uhalifu wa Kawaida.
Ugaidi una hukumu kali Sana.
Tazama hili,
Mabalozi wa nchi za magharibi mara baada tu ya Serikali kumtangaza Mbowe kuwa anashitakiwa kwa kosa la kutaka kufanya Ugaidi,wamekua wakihudhuria mahakamani mara kadhaa,
Mbowe sio Mzungu,sio Marekani,sio Mjerumani wala sio mswidishi,sasa ni nini kinachowapeleka mahakamani?
Hebu jiulize hili,uliwahi lini na wapi mabalozi wa nchi kubwa hizo wakienda Mahakama za nchi walizokaribiahwa kusikiliza Kesi?
Je wameenda kusikiliza Kesi ya Sabaya?
Je walienda kusikiliza Kesi iliyokua inamkabili Mbowe na wenzake baada ya kifo cha Akwilina?
Je walienda kusikiliza Kesi ya Zombe?
Au uliiwaona wakienda kusikiliza Kesi ya milionea yule wa Arusha aliyeuawa kwa kupigwa risasi?.
Je unadhani wanampenda sana Mbowe na chadema na akina Adamoo?
Iko hivi,Wamarekani na wazungu wa West ni waathirika wakubwa wa mambo ya ugaidi,hivyo wamefanya tafiti nyingi Sana za kijasusi juu ya ugaidi,wanajua network zote za magaidi hapa Duniani.
Hatuji tu hao wanaoenda mahakamani ni watu wa aina gani,Kati ya hao kuna Watu Wa FBI,CIA,Mossad,MI6 na mashirika mengine.
Wenzetu hawachukulii mambo kwa wepesi au kipuuzi.
Wenzetu ukitamka tu neno Gaidi,masikio yao na macho yao yako wazi masaa 24 kujua nani Gaidi na nani sio.ndio maana Kesi hii wameipa kipaumbele kikubwa Sana.
Watakua wamefuatilia na kujua kabisa Kesi hii imetengenezwa kwa chuki za kisiasa na malengo yake.
Inawezekana wanajua ujinga wote na waliolibuni .
Jaji wa zamani Augustine Ramadhani aliwahi kusema hivi.
Kuwa Kesi zote huwa zinaendeshwa ndani ya Mahakama na nje ya Mahakama.
Maana yake ni kwamba wakati Kesi inaendelea mahakamani huku mitaani pia watu hufuatilia,hujadili,hutoa ushahidi,huchambua,hupinga,hukubali,husikiliza na kuona kama haki inatendeka ama haitendeki.
Kwa sababu huku mitaani kuna mashuhuda ambao hawakuenda mahakamani kuwa mashahidi lakini wanajua mambo yote.wanajua kila kitu.
Kwa hiyo hukumu itakayo tolewa watajua kama ni hukumu ya haki ama ya uonevu.
Ndio maana utasikia watu wengi wakisema ama Kesi imeamuliwa kwa haki ama kwa uonevu.
Kwa sababu wanaifuatilia kila kitu na kuna baadhi wanajua ukweli.
Kesi za kisiasa hasa za Wapinzani dhidi ya serikali ya CCM.
Kesi za kisiasa hasa za Wapinzani dhidi ya serikali mara nyingi huwa zinaamuliwa kwa uonevu na mara nyingi maamuzi huwa hayatokani na maamuzi huru.
Ipo mifano.
Kesi ya mgombea binafsi iliyofunguliwa na Mtikila,
Kesi za kupinga matokeo ya Urais.
N.k.
Hawa mabalozi wa West kila baada ya Kesi ya Mbowe wanapewa ufafanuzi kuhusu mwenendo wa Kesi.
Serikali ya Samia imeonesha kutaka kurudisha mahusiano ya kimataifa tofauti na yule "gangwe".
Na mama anasafiri kwelikweli kutaka serikali yake ipewe heshima yake kimataifa,sasa Hawa wa magharibi wao wanatazama Sana demokrasia na haki za binadamu.
Je kama Mbowe akihukumiwa unafikiri watakaa kimya tuu.
Unafikiri kwenda kwao mahakamani kuna ashiria nini?
Wananchi wataipokeaje hukumu ya Mahakama kama Mbowe atafungwa?
Unajua kuwa kuna Wana CCM wanakerwa Sana na Kesi hii?
Unajua kuna viongozi wa baadhi ya vyombo na taasisi wanakerwa na Kesi hii?
Kama Mbowe akifungwa kwa kulazimisha, Unafikiri ni nini kitatokea.?