Kesi ya Mbowe Serikali imeingia kwenye mtego huu iuepuke mapema

Jirani feki
Feki!!! ,IPO siku nitakuumbua!Ulijisahau siku moja ukaandika kitu kuhusu CHADEMA yale maongezi ulikuwa unayaongea na yule mchumia tumbo mwenzio wa Gazeti la Uhuru ndo nikakugundua vizuri.

Ni hivi achana na kazi hii ya laana Endelea na uhudumu wako wa Afya.Yaliyokupata ni makubwa Sheria za Jamii forumu haziruhusu otherwise ningekuumbua vizuri na CCM wenzako wangejifunza kitu Na kuachana na kazi za kujikomba Kama wewe.

Nina uhakika Kwa yaliyo kupata huwezi tena kuwa active Kama zamani kila uzi unao mhusu JPM IPO.Kula ulicho kipanda
 
HAKUKAMATWA KWA SABABU YA KONGAMANO LA KATIBA ONDOA UPOTOSHAJI
Ila kwa sababu gani? Ugaidi? Ujambazi? Uchochezi?

Kama unadhani ni hivyo, basi wewe ni miongoni mwa watu wenye fikra duni na za masafa mafupi sana yanayoishia chini ya magoti yako...!!
 
Kumbuka hakuwepo Tanzania kwa kipindi kirefu tu.toka wale wenzake wakamatwe

Huu ujinga ndio mnatamani wananchi wauamini. Kwa bahati mbaya mnatumia mbinu za kizee mno, matokeo yake mashahidi wa jamuhuri wanaongea utoto wa ajabu huko mahakamani. Ukifuatilia hiyo kesi na ushahidi unaotolewa na serikali, huwezi shangaa ukisikia wazungu wanatuita manyani.
 
Kumbuka hakuwepo Tanzania kwa kipindi kirefu tu.toka wale wenzake wakamatwe
Wakati akienda dubai na mamlaka zinamruhusu alikuwa gaidi ama alikuwa bado? Wakati anafiwa na kaka ake Chief hangaya anampa Salam za rambirambi alikuwa gaidi au alikuwa bado? Apange ugaidi jambo linalogharimu mataifa miaka na miaka wamwachie tu mwaka mzima eti wanafanya uchunguzi, uchunguzi walokuja kufanya ndo huo wa pistol moja na risasi tatu ndiyo vitafanya matukio yale yoooote
 
Kuna ng'ombe humu wanaamini Mbowe ni gaidi aliyepanga mipango na mpika chai wa sabaya ili kuangusha serikali na kumdhuru Raisi wao sabaya aliyefungwa miaka 30 kwa ujambazi
 
Kimsingi nahisi alikamatwa kwa sababu ya tozo, waliona anatibua makusanyo. Siku zote walitulia nini kiliwasukuma sasa?
 
.
 
Kaka waliyo iandaa hii kesi ,,lengo kubwa na madhumuni yao ni kumuangusha mama.Najua watamfunga kwa ubavu,,kwa juu juu tu ukiangalia,mpaka sasa haijatajwa wala kudhihirika au viashiria vya mbowe kuwa alikuwa anataka kufanya ugaidi,kilichopo ni silaha kushikwa kwa mshitakiwa mbali na mbowe.Ndio maana Kingai alisema wamemshika na risasi sijui tatu,,Mahita anasema mbili,,,mtaalamu wa kukagua,anatuletea risasi moja na maganda mawili,,Loo,,,kaka Mama wanataka wamuangushe,,mie binafsi yangu,ninavyo mpenda mama,,inaniuma sana,wanamuaminisha kitu ambacho hakipo, NGOJA TUONE NI UPI MWISHO WA HII KESI.
 
Ni kweli kesi hii ni ya kutunga. Lakini CCM haiwezi kuifuta kesi regardless the athari zake kwa sababu kwa sasa CCM inaongozwa na dhamira kuu tatu:
1. Kuendelea kushika madaraka kwa namna yoyote, iwe kuua, kuteka, kupora uchaguzi, kufunga etc
2. Kutesa watu physically, socially, spiritually etc
3. Kufilisi watu
So Mbowe huenda akafungwa, na kuangalia motive ya serikali yote utaona wamepanga kumfunga Mbowe. CCM haijali athari halimradi inatawala.
 
Ukweli ni kwamba suala la katiba mpya haliepukiki ni sawa na kulisogeza tu tatzo mbele iwe leo, kesho ama kesho kutwa katiba lazima itakuja tu, kudeal na mbowe bila akili kubwa ni ujinga na kwa msimamo wa mbowe wajue siku akitoka tu ataanzia pale pale alipoishia
 
mboe anavuna alicho kipanda kwa mikono yake mwenyewe.
hili ndio tatizo la kung'ang'ania nafasi ya uenyekiti kwa muda mrefu, matokeo yake alijisahau na kuanza kujifanyia mambo anayo yataka yy mwenyewe.
 
Kwani mbowe kaanza kulilia katiba mpya lini na wakina adamoo wamekamatwa lini?
 
mboe anavuna alicho kipanda kwa mikono yake mwenyewe.
hili ndio tatizo la kung'ang'ania nafasi ya uenyekiti kwa muda mrefu, matokeo yake alijisahau na kuanza kujifanyia mambo anayo yataka yy mwenyewe.
Wewe wakala wa shetani taja hayo mambo ambayo kajifanyia mwenyewe.
 
--" Mara hii Mbowe huchomoki-- Tunakupiga ugaidi"--ACP Kingai
These idiots are taking this country for granted am sure!
Kuna mavijana fulani hapa mtaani wana shida sana kila wakati wanatetea dola ovu! Juzi nimewaambia afadhali wafe tu wote tuanze upya kumentor vijana wanaojitambua!
Bila hivyo hii nchi iko njiani kwenda gulioni!
 
Umewaamini walioliweka hivyo. Kwa nini usiongeze na za kwako na ukajaribu kulifikiri ukawa na majibu ya kwako, kuliko kuaminishwa na watu wenye maslahi yao ya kisiasa!!??
 
Umewaamini walioliweka hivyo. Kwa nini usiongeze na za kwako na ukajaribu kulifikiri ukawa na majibu ya kwako, kuliko kuaminishwa na watu wenye maslahi yao ya kisiasa!!??
(Members sympathy)search..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…