Imebidi kujiridhisha mambo kadhaa kwanza:
Amesikika shahidi #5 kwenye kesi hii akijitambulisha kama Fred Kapala (lawyer) japo TLS anasomeka kama Fred Kapara:
View attachment 1996270
Ikumbukwe pia Fred Kapara aliwahi ibuka pia kwenye case almaarufu ya kujiteka kwake bwana Abdul Nondo kama shahidi upande wa mashtaka kutokea Tigo kama hivi hivi.
Fred Kapara anataka mahakama imwamini kuwa hakuwahi kumsikia Freeman Aikael Mbowe popote pale duniani.
Shahidi huyu wa kimkakati tokea Tigo anadai pamoja na kuwapo watu wengine katika legal department hapo Tigo, yeye ndiye aliyepokea barua yenye ombi la kufuatilia nyendo za namba ya Mheshimiwa Mbowe kutokea polisi.
Kwamba pia yeye ndiye aliyelifanyia kazi ombi hilo. Ndiye aliwasilisha maelezo polisi na ndiye aliye kinara leo mahakamani kumkaanga Mh. Mbowe.
Kwa mtaji huu, Fred Kapara ndiye legal team na legal team ndiye yeye pale Tigo.
Kwamba zilitakiwa taarifa za usajili na za miamala ya pesa kutokea kwenye simu hiyo ya Tigo kwa kipindi cha tokea Jun 1 - Jun 31, 2020.
Kama mchezo wa kuigiza vile:
1.June ina siku 30.
2. Mbowe alishambuliwa na watu wasiojulikana 8 Jun 2020 na akaendelea kuwa out of action kwa muda mrefu.
3. Yeye alipeleka taarifa zote alizoweza kupata kuhusu namba hiyo ya Mheshimiwa Mbowe zikiwamo ambazo hakuulizwa.
4. Hapakuwa na kigezo chochote kisheria au kimaadili kilichozingatiwa kwenye utoaji wa taarifa hizo.
Shahidi ambaye kimsingi ni mwana sheria kaonyesha wazi kuwa hana ujuzi wowote na masuala ya kiusalama, kiulinzi wala kiufundi wa mitambo ya mawasiliano.
Pamoja na kupoteza muda mwingi kujaribu kuyaongelea mambo ya kiufundi, shahidi alihitimisha kwa kudai:
1. Ali print kutokea kwenye screen server 😁😁.
2. Shahidi hakuwahi kusikia uwapo DB2 software ambazo leo ni literally obsolete na akafanywa kukubali kuwa ndiyo latest.
3. Shahidi hakuwahi kusikia kuhusu program habari ya mujini ya udukuzi kwenye telecommunications Industry leo ya "Pegasus" wala uwezo wake.
4. Shahidi hajui SQL ni nini. Anafanywa kuamini ni software yenye version.
5. Shahidi hajui kuwa Ernest and Young hawajihusishi na security systems za telecommunications.
6. Hajui kuwa hakuna jargon LINU katika IT.
7. Hajui maana ya server wala aina zake.
8. Anasema Tigo wako secure kwa sababu wana Cisco, kuna firewall na switch ya Huawei.
9. Nk nk
Shahidi kaipotezea mahakama muda mwingi kupitia mambo ya kitalaamu asiyokuwa na ujuzi nayo.
Kwamba Mbowe alituma pesa kwa simu kipindi hicho? Kwani kosa kutuma pesa?
Ikumbukwe pia alicho print anaweza print mtu mwingine yeyote katika format hiyo hiyo bila kuhusianisha na server za Tigo.
Nini thamani ya ushahidi kama huu?