Kesi ya Mbowe: Umuhimu wa Ushahidi wa CPL. Abdallah ni Upi?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Umesikika ushahidi wa Cpl. Hafidh Abdallah (shahidi #3) kutokea Police Forensic Bureau, Dar es Salaam.

Shahidi anadai alipokea bastola moja, risasi tatu na barua yenye maelekezo kutokea office ya DCI.

Kwenye taarifa yake rasmi shahidi anasema:

IMG_20211030_090340_053.jpg

Yaani ameshiriki kwenye kukagua na kutambua silaha za moto, milipuko, maganda ya risasi, risasi zilizo tumika na vifaa vya kufanyia kazi vijavyo dhaniwa kutumika kwenye matukio ya uhalifu kwa miaka 10 sasa."

Hata hivyo shahidi akawasilisha mahakamani peke yake bastola 1, risasi 1, maganda 2, na risasi 2 zilizotumika pamoja na ripoti yake.

Shahidi huyu:

1. Hana barua iliyotoka kwa DCI yenye kuonyesha alipewa nini na alitakiwa kufanya nini?

2. Orodha ya vitu alivyofanyia utambuzi na ukaguzi ni kubwa kuliko aliyowasilisha mahakamani.

3. Shahidi haonyeshi nyaraka yoyote kwanini alikabidhiwa risasi 3 naye kawasilisha risasi 1.

4. Shahidi haonyeshi popote ushahidi wake unahusiana vipi na mshitakiwa yeyote.

Hata kama hukumu zinatolewa kwa kuzingatia maelezo ya upande wa mashtaka peke yake:

Kesi ya Mbowe: Ushahidi upande wa Mashtaka unapochukuliwa kuwa ndiyo Dhahiri

Ni nini thamani ya ushahidi wa Cpl. Hafidh Abdallah Mohammed?
 
Ripoti inataja "TERROLIST"; kuna American English, Australian English, Nigerian English; ifike mahali Tanzanian English itambuliwe rasmi na iingie kwenye Kamusi. Maneno mengi aliyotamka "shujaa" yangeweza kuingiamo na sisi tukawa na ka-kiingledha ketu! Nasema uongo ndugu zanguni?

Kingai aliita hiyo ni curable mistake 😁😁
 
Ngoja waje wajuzi wa haya mambo. Mimi nafuatilia kupata ujasiri wa kuuliza maswali na kufikiri kwa kina

Title na aya ya kwanza vinahusika:

IMG_20211029_201139_121.jpg

Within the curable errors za ACP Kingai, wakili msomi Malya ana hoja nzito:

"Yawezekana shahidi na exhibits zake ni kwa ajili kesi nyingine, siyo hii."

Ndiyo maana utopolo wote aliokuja nao, haumhusu mtu yeyote kwenye kesi hii.
 
Umesikika ushahidi wa Cpl. Hafidh Abdallah (shahidi #3) kutokea Police Forensic Bureau, Dar es Salaam.

Shahidi anadai alipokea bastola moja, risasi tatu na barua yenye maelekezo kutokea office ya DCI.

Kwenye taarifa yake rasmi shahidi anasema:

View attachment 1991648

Yaani ameshiriki kwenye kukagua na kutambua silaha za moto, milipuko, maganda ya risasi, risasi zilizo tumika na vifaa vya kufanyia kazi vijavyo dhaniwa kutumika kwenye matukio ya uhalifu kwa miaka 10 sasa."

Hata hivyo shahidi akawasilisha mahakamani peke yake bastola 1, risasi 1, maganda 2, na risasi 2 zilizotumika pamoja na ripoti yake.

Shahidi huyu:

1. Hana barua iliyotoka kwa DCI yenye kuonyesha alipewa nini na alitakiwa kufanya nini?

2. Orodha ya vitu alivyofanyia utambuzi na ukaguzi ni kubwa kuliko aliyowasilisha mahakamani.

3. Shahidi haonyeshi nyaraka yoyote kwanini alikabidhiwa risasi 3 naye kawasilisha risasi 1.

4. Shahidi haonyeshi popote ushahidi wake unahusiana vipi na mshitakiwa yeyote.

Hata kama hukumu zinatolewa kwa kuzingatia maelezo ya upande wa mashtaka peke yake:

Kesi ya Mbowe: Ushahidi upande wa Mashtaka unapochukuliwa kuwa ndiyo Dhahiri

Ni nini thamani ya ushahidi wa Cpl. Hafidh Abdallah Mohammed?
Upande wa mashtaka wanajaribu kunogesha tamthilia yao ili isizidi kupoteza mvuto
 
Title na aya ya kwanza vinahusika:
....
... Aya ya Kwanza; kwa miaka 10 amekuwa mtaalamu wa utambuzi wa zana zilizohisiwa kutumika kwenye uhalifu ingawa namna alivyoandika inaweza pia kutafsiriwa as if amekuwa mtaalamu wa zana zilizotumika kwenye uhalifu kwa miaka 10. Huyu inaelekea kwenye somo la "Sentence Structure" hakuwa darasani huyu!

Kwa ripoti muhimu kama hii (ya ugaidi) huwezi kujiandikia andikia tu! Kila herufi, kila neno, kila sentensi, kila paragraph lazima vioane na vijenge context yenye mashiko; isiyoacha utata wa aina yoyote ile. Walishindwa kum-consult editor mtaalamu akawasaidia ku-edit? Au editor naye ndio hivyo?
 
Ni nini thamani ya ushahidi wa Cpl. Hafidh Abdallah Mohammed?
Vuta subira. Umuhimu wake utauona muda utakapofika. Bado mashaidi 20 upande wa serikali. Mambo ya ku connect dots ni wachache tunayoyaweza ila hairuhusiwi kujadili maswala ambayo yako mahakamani.
 
... Aya ya Kwanza; kwa miaka 10 amekuwa mtaalamu wa utambuzi wa zana zilizohisiwa kutumika kwenye uhalifu ingawa namna alivyoandika inaweza pia kutafsiriwa as if amekuwa mtaalamu wa zana zilizotumika kwenye uhalifu kwa miaka 10. Huyu inaelekea kwenye somo la "Sentence Structure" hakuwa darasani huyu!

Kwa ripoti muhimu kama hii (ya ugaidi) huwezi kujiandikia andikia tu! Kila herufi, kila neno, kila sentensi, kila paragraph lazima vioane na vijenge context yenye mashiko; isiyoacha utata wa aina yoyote ile. Walishindwa kum-consult editor mtaalamu akawasaidia ku-edit? Au editor naye ndio hivyo?

Mkuu Simbachawene alisema required maximum qualifications for police applicants ni Division IV (not less than 30 points):

Waziri Simbachawene, nadhani umeshapata jibu kuwa Jeshi la Polisi siyo "dumping site" ya" failures"

Tutegemee nini zaidi kwenye mazingira hayo 😁😁?
 
Hakuna sheria inayozuia kujadiliwa kwa mambo yaliyo mahakamani, ni propoganda ya wanasiasa na wanahabari uchwara tu wanapotaka kukwepa kuzungumzia jambo.
Vuta subira. Umuhimu wake utauona muda utakapofika. Bado mashaidi 20 upande wa serikali. Mambo ya ku connect dots ni wachache tunayoyaweza ila hairuhusiwi kujadili maswala ambayo yako mahakamani.
 
Hakuna sheria inayozuia kujadiliwa kwa mambo yaliyo mahakamani, ni propoganda ya wanasiasa na wanahabari uchwara tu wanapotaka kukwepa kuzungumzia jambo.
Hao wanasiasa ndiyo watunga sheria. Mawakili na wanasheria wengine ni wasomi tu wa hizo sheria zilizotungwa na wanasiasa kama akina Msukuma.

Utata unakuja pale hao waliosoma hizo sheria zilizotungwa na akina Msukuma, wanapojiita wao ndiyo wasomi na wahimili wakuu wasiopaswa kuingiliwa na hao wakina Msukuma wanaotunga hizo sheria na sheria mama aka katiba.
 
Back
Top Bottom