Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Naomba usiseme kwa sauti watoto wao watasikia.Polisi wetu linapokuja swala la pesa am sorry to say wanakuwa hawana tofauti na upigaji mwingine
Wanachukua hadi hati ya kiwanja, pikipiki???Kingai aneuchuna tu utafikiri hakukwapua pesa za makomandoo
Hivi karibuni kuna mama mmoja mfanyabiashara huko maeneo ya Tegeta nadhani alilalamika kuwa walichukua mgodoro yake ya biashara, alipoambiwa akayachukue alipewa magodoro chakavu yaliyotumika. Gari likiwekwa yadi yao litatoka na magurudumu chakavu na betri iliyochoka.Pesa wameshakwapua hao wakirudisha hapo ni kesi kwao itabidi wauchune tuu kama hawajui kitu hapo hata hiyo habari ya kuvunja nyumba kwa Adamoo wanaweza kumruka hata Mkuu wa Polisi Chalinze kuwa hawakwenda na ishu hiyo ni yake...
Huenda wamekwenda kuvihakiki kwa ajili ya sensa ya watu na makazi.Umesahau hati ya kiwanja na kadi ya pikipiki mali za Adamoo na mkewe. Sijui hata walivipeleka wapi hivyo vitu?!
Mbele ya pesa nikama kundi la fisi kwa hawa vijana wa SirroPolisi wetu linapokuja swala la pesa am sorry to say wanakuwa hawana tofauti na upigaji mwingine
Kaliona hilo ndio maana akasema kwa maandishi. HahahaahNaomba usiseme kwa sauti watoto wao watasikia.
Walishajarib kunifanyia huo uhuni. Nikaahtaki kwa mkuu wa upepelez... walirudisha chap na mnuno juu.Hilo ni ngumu aisee kama tu ukikabidhi Smart kaunta ukiwa selo ukitoka unapewa kitochi ukitaka kucomplain unatishiwa kurudishwa selo,ndo watarudisha hivyo.
DAI la Katiba mpya linaletaje vilio na manung'uniko kwa wengine? Ni kwa CCM na wachumia tumbo kama "katelephone" na "lion cha mwene"? Maana hao ndio miongoni mwa wasiotaka kabisa kusikia habari za Katiba mpya.Hili likesi nalo DPP alifute tu, halina maana wala maslahi yeyote kwa Taifa kwa sasa! Kama ni mambo ya katiba mpya yanahusika basi wakae chini na bwana Mwamba waongee ni jinsi gani linaweza likashughulikiwa hilo bila kuligawa taifa or kuleta vilio na manung'uniko kwa wengine..
Si miongoni wa mliotoa hukumu kabla ya kesi kuwa ni gaidi na hakubambikiwa pamoja na wengine,halafu unasema unaipenda Tanzania.Ipi?Hili likesi nalo DPP alifute tu, halina maana wala maslahi yeyote kwa Taifa kwa sasa! Kama ni mambo ya katiba mpya yanahusika basi wakae chini na bwana Mwamba waongee ni jinsi gani linaweza likashughulikiwa hilo bila kuligawa taifa or kuleta vilio na manung'uniko kwa wengine..
Taifa halijajigawaHili likesi nalo DPP alifute tu, halina maana wala maslahi yeyote kwa Taifa kwa sasa! Kama ni mambo ya katiba mpya yanahusika basi wakae chini na bwana Mwamba waongee ni jinsi gani linaweza likashughulikiwa hilo bila kuligawa taifa or kuleta vilio na manung'uniko kwa wengine..
Pesa ni kitu kingine kwa Polisi wetu na viongozi wetu hawa huwa wanachanganyikiwa.Mashahidi wa mwisho walikuwa wake wa watuhumiwa, kubwa lililoonekana kwenye kesi ni polisi kuchukua pesa na vitu ambavyo havihusiani na kesi kwani havikuwasilishwa mahakamani kama ushahidi. Maadam wake wa washitakiwa wamefahamika ingekuwa jamno jema mahakama iamuru wakina mama hao ambao nawaona kwa sasa ni kama wajane wapewe pesa zilizochukuliwa toka kwa waume zao ili ziwasaidie kimaisha.
Nawasilisha.