Kesi ya Mbowe: Wapelelezi wanatakiwa kumsaidia Rais kuithibitishia dunia Mbowe ni Gaidi na sio kucheza na majaji wetu pekee itatuweka kubaya

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Ukweli mchungu NI kuwa toka mama arudi ameingia kwenye dira za kimataifa za diplomasia. Ameenda ughaibuni na amekuja na Zawadi kibao.
Inchi inarudi kwenye furaha. Mama anajaribu kuonesha kuwa nchi inarudi kwenye utawala wa sheria. Tena Sheria zinazotenda haki. Sio Sheria hizi za juzi juzi za mitandao zilizolalamikiwa ndio ziondoke na mwanasiasa mashuhuri itaonesha wazi kuwa ilipangwa. Mmsaidie kwenye Hilo. Kupitia mahakama, Mandela alifungwa. Nyerere kwenye harakati alifungwa, Mugabe alifungwa lkn haki ilikuja kupatikana.

Tukifosi ushaidi finyu hukumu yetu kesho itabaki kuwa kumbukumbu kubwa duniani. Leo mahakamani dunia nzima ipo kufatilia kesi ya Mbowe kupitia mabalozi wao. Siku ya hukumu nakala za hukumu hiyo, ushaidi na kilakitu vitachukuliwa na kuchambuliwa dunia nzima. Kupitia hukumu hiyo dunia itajua Ubora wa mahakama zetu.

Mi si mwanasheria lkn mh!
1. kwa kiongozi "jambazi" aliyetaka kudhuliwa(kwa mujibu wa kibatala).
2. Kwa ushaidi wa kubambikia watu kesi kwa mashaidi muhimu
3. Kwa maelezo ya kudhuru viongozi(wengi) Ila mpaka leo anayetajwa NI kiongozi 1.
4. Kwa ushaidi wa maneno ya wasiri. Kwanini wasiri wasije wenyewe waelezee Hali alisi.
5. Kwa sprey isiyokuwepo.
6. Kwa vilipuzi pisto 1 na risasi 3.

Njooni na ushaidi mzito Mbowe asitoboe. Muwe siliasi. Msitupeleke vikwazoni Kama Zimbabwe.
 
Mpaka Sasa hivi tunaona sarakasi tu hakuna ushahidi au shahidi kulinganisha hayo makosa wanauotuhumiwa nayo watuhumiwa. Tunaona mpaka Sasa hakuna upelelezi wenye vidhibitisho kabla ya watuhumiwa kukamatwa zaidi ni hearsays (Hadithi) kutoka kwa Bwn Urio bila physical supportive evidence ie fingerprint, DNA,voice, written & video records kwaajili ya ku-link kesi
 
Ushahidi UPI huo?

Hawana lolote hawa.

Labda ungesema na kuwaambia wauondoe ujinga wao huo mahakamani na wamwachie ndugu Mbowe na wenzake huru wasiwapotezee muda wao kwa kuwaweka kizuizini isivyo halali...

Aidha ungewaambia na Polisi waache kufanywa daraja la wanasiasa ili kufikia malengo yao ya kisiasa kiasi cha kulazimika kuzikanyaga sheria na kutumia madaraka yao vibaya ili kuonea watu wasiowapenda, wanaodhani ni kikwazo cha maslahi yao..!
 
Nchi yetu inadhalilishwa na kikundi cha watu wasiofika hata 100
 
Nchi yetu inadhalilishwa na kikundi cha watu wasiofika hata 100
Hapa ndio umuhimu wa kuwapunguzia polisi baadhi ya majukumu ie upelelezi ianzishwe mamlaka inayojitegemea kwa ajili ya upelelezi tu pia ofisi ya mwendesha mashtaka itolewe kabisa polisi, polisi wao wabaki na kulinda raia &mali za raia na kukamata wahalifu tu
 
Mashahidi hawwna ushahidi....ajabu sana
 
Polisi anayesemekana ndio aliye wapekua watuhumiwa na kuwakuta na bastola na kete ndio huyo huyo kafukuzwa kazi kwa kutaka kumbambikia mzee mmoja meno ya tembo.

Shahidi wa upekuzi ni mama muuza pombe ya mbege ambaye kila amuuziaye tangu asubuhi lazima aonje yeye Kwanza.
Vitu vingine vya kijinga sana
 
hapa umechemsha, we Mhaya wangu! Utawala wa sheria kwa vipi amonesha? Haki ipi , ya Tozo?
 
Sijui tutafika lini tunakokwenda kama Nchi tupo busy na kesi ya kutengenezwa na Sabaya,Jumanne na huyo mtoto wa IGP mstaafu..Gaidi kweli atapewa hata kopo la maji mahamani si siraha hiyo ili apate siraha halisi..watoeni hao mnaidharirisha Tanzania na watu wake...
 
Ukweli mchungu NI kuwa toka mama arudi ameingia kwenye dira za kimataifa za diplomasia. Ameenda ughaibuni na amekuja na Zawadi kibao.
Inchi inarudi kwenye furaha...
Hapo ndipo inapotokea haja ya sheria zinazohusiana na mambo ya upelelezi na uchunguzi kufanyiwa maboresho ili kutambua uwepo wa "ombudsman" ambaye anakuwa mchunguzi huru katika kesi kama hii ya ugaidi.

Aina ya mashaidi na hata ushahidi unaoletwa na upande wa mashtaka una dosari nyingi za kisheria na zenye kutiliwa mashaka.
 
Mkuu hivi wale mabalozi waliokuwa wanahudhuria mahakamani kushuhudia kesi bado wanahudhuria? Kama siwaoni wala kuwasikia!
 
TISS ndio wamepanga huu utopolo , mama kapewa matango poli akayabugia , majaji wakaelekezwa na wamekubali bila kujali aibu inayowakabili
Sio aibu pekee bali na laana itakayowatafuna wao na vizazi vyao ikiwa watazidi kupinda haki kwa maslahi ya kisiasa.
 
Kinachonifikirisha ni kwa nini mtuhumiwa wa kosa kubwa kama hili aliachwa huru wakati washirika wake wamekamatwa! Hivi hakujua kuwa washirika wake wamekwisha kamatwa na dili limebunguluka?

Kwa nini alikuwa anaenda nchi za nje na kurudi alijiamini nini? Au walikuwepo washirika wakubwa zaidi waliokuwa wanampa ujasiri na asichukue hatua yeyote kujilinda?

Kwa nini alipewa nafasi kwenye sherehe kule Mwanza kuongea mbele ya Rais? Ngoja nisubiri mashahidi wengine pengine nitapata jibu, la sivyo kwangu ni ngumu kumeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…