Kesi ya Mbowe: Yanayoendelea ni taswira ya Uongozi tulionao

Kesi ya Mbowe: Yanayoendelea ni taswira ya Uongozi tulionao

Naomba kutangaza mgongano wa maslahi. Mimi ni miongoni mwa watu wakubwa tu serikalini. Katika kesi hii kuna moja ya kielelezo (exhibit) jaji huyu alikikataa kwa madai kuwa shahidi alikipata kwa nia za panya kutoka kwenye masjala ya mahakama.

Haijulikani mpaka leo ni nani alikiiba toka kwenye masjala au maktaba ya mahakama na kumpa yule shahidi. Baada ya kukikataa kile kielelezo hakimu huyu ametishiwa kupoteza kazi muda wowote au la ameambiwa atahamishiwa Tandahimba.

Sielewi Tandahimba kuna nini kibaya cha kumtishia mtu kupelekwa huko. Taratibu za mahakama zipo wazi kwamba ama umekitumia au hujakitumia huruhusiwi kupanda kizimbani na kitu chochote zaidi ya nyaraka za mahakama unazozikuta pale ikiwemo vitabu vya dini.

Huyu shahidi aliingia na majibu ya maswali atakayoulizwa na upande wa mawakili wa serikali. Huyo Jaji yupo upande wa mwajiri wake ambaye ni serikali. Hapo alipo anajua alivyokoromewa kwa kukataa kile kielelezo.

Mwanzo hakujua kuwa hii kesi ina maslahi ya serikali kuhalalisha kufungwa kwa Mbowe. Ndiyo maana Mama alitamka wazi kabisa kwamba Mbowe ni gaidi na washirika wake walishafungwa kitambo. Kwamba alikuwa anasubiriwa yeye tu.
 
Naomba kutangaza mgongano wa maslahi. Mimi ni miongoni mwa watu wakubwa tu serikalini. Katika kesi hii kuna moja ya kielelezo (exhibit) jaji huyu alikikataa kwa madai kuwa shahidi alikipata kwa nia za panya kutoka kwenye masjala ya mahakama...
Duh! Hatari sana.
 
Naomba kutangaza mgongano wa maslahi. Mimi ni miongoni mwa watu wakubwa tu serikalini. Katika kesi hii kuna moja ya kielelezo (exhibit) jaji huyu alikikataa kwa madai kuwa shahidi alikipata kwa nia za panya kutoka kwenye masjala ya mahakama...

Kwa mtizamo huu. Kesi hii labda kama ina maamuzi kamili mkononi tayari. Kama ni hivyo:

1. Ya nini basi kuendelea na kesi hii, si wasome hukumu tu?
2. Ya nini Mawakili wa utetezi kuendelea kumvumilia jaji huyu kuendelea na kesi kwa namna hii?
3. Kwanini mawakili utetezi wasichukue hatua kali zaidi zikiwamo kuitaka mahakama kushurutisha ushahidi wa namna yoyote kuletwa hata kutoka kwa yeyote wanayemtaka yakiwamo makampuni ya simu?
 
Nimewaza tuuu; Kama pingamizi zote za utetezi zingekubaliwa automatically, kesi ingekuwa imekwisha.
Kwa umoja wao, hawataruhusu Hilo mapema ivi.
Ni ndoto tuuuu
 
Nimewaza tuuu; Kama pingamizi zote za utetezi zingekubaliwa automatically, kesi ingekuwa imekwisha.
Kwa umoja wao, hawataruhusu Hilo mapema ivi.
Ni ndoto tuuuu

Kiuhalisia si ilikuwa sheria na haki? Kinyume cha hapo hakuna umuhimu tena au vipi?
 
Naskia na leo jaji amekataa pingamizi la utetezi, huko ndiko akili zao wote serikalini zilipohamia, tukipigwa na wajanja wa nishati hata hawana habari.

Hii kesi natangulia mahakama ya rufani kuisubiri, huko mahakama kuu kinachoendelea kwa sasa ni kupotezeana muda tu.

kwani wale maafisa wa unarozi wao wanasemaje!!![emoji2][emoji2][emoji2]

mkuu ccm inawachosha na inajua kama mnapenda sana kushindana.
 
Alisikika Jaji Mkuu kwenye hafla ya kuapishwa Jaji Siyani:

"Hukumu zenu zizingatie mitizamo ya mihimili mingine."

Tulipo sasa tumemalizana na shahidi ambaye ushahidi wake umepokelewa kama ulivyo. Hii ni pamoja na kukutwa akiwa na maandiko ya chabo yaliyo batili kizimbani.

Huyu ni shahidi anayethibitisha kupokea exhibit (detention register) kutokea mahakamani bila ya yeye kuiomba wala kusaini popote (hali ya kustaabisha).

Exhibit hii anayosema ilikoma kutumika kutokea 12 August 2020, ni yenye kusajili mahabusu kwa jinsi wanavyokuja na kutoka.

Hata hivyo pamoja na kuthibitisha kuwa entries zake hupaswa kufuatana (sequentially) kwa tarehe, kunaonekana:

#392 - Mohammed Ling'wenya 12/8/2020

Wakati entries nyingi nyingine kwa mfano:

#114 kuna mtuhumiwa aliingia 30/7/2021
#156 kuna mtuhumiwa aliingia 3/8/2021

Nk, nk.

Nini maana ya mivurugano hii kutokea kwenye dola, katikati ya haki za watu?

Kwanini njia za kisayansi zilizopo mikononi mwa serikali hazitumiki kuufichua ukweli na kuacha haki kutamalaki?

Au ni kwamba tuna uongozi tu uliodhamiria kuwanyang'anya watu haki zao pasipokuwa na uhalali wowote?

Umoja gani wa taifa lipi unaoweza kutumainiwa wapi katika hali kama hizi?
Mkataba wa bagamoyo tayari baadaye mkataba bado
Umeme wa maji ghari, umeme wa gas ghari
Mgao wa maji na umeme, tumekamata mchina anaiba maji mgao umeisha
 
Mkataba wa bagamoyo tayari baadaye mkataba bado
Umeme wa maji ghari, umeme wa gas ghari
Mgao wa maji na umeme, tumekamata mchina anaiba maji mgao umeisha

Shahidi aliyepeleka watuhumiwa Mbweni anasema hajawahi kufika huko. Waungwana wanasema - na bado!
 
Back
Top Bottom