Kesi ya Mirathi ya Dkt. Likwelile: Vicky Kamata ashindwa, mahakama yasema ndoa yao haikuwa halali

Je kama hatuja divorce lakini mke wangu akaolewa na mtu mwingine na mimi nikao mke wangu ana haki ya kudai mali zangu ambazo nimechuma baada ya yeye kuondoka?
 
Kuwa na uwezo wa kufoji na kufoji ni vitu viwili tofauti. Kwa ndoa nyingi huwa cheti kikishatolewa inatakiwa uende kufuatilia je wafungishaji wamekisajili rita? Huwa si utomatic umefunga na umesajili hapohapo. Pia kama kitu toka kwa muuzaji kiliandikwa jina fulani ni rahisi kufuatilia mlolongo wa fomu namba 30 ya ardhi.
 
Then huyo mzee according to mwenendo wa kesi alifunga ndoa ya kiserikali na baadae akaenda kuibariki kanisani. Ndoa ya kiserikali je ina limit ya idadi ya wake?
 
Je kama hatuja divorce lakini mke wangu akaolewa na mtu mwingine na mimi nikao mke wangu ana haki ya kudai mali zangu ambazo nimechuma baada ya yeye kuondoka?
Hapana, hawezi kudai. Labda kama umeendeleza kutokana na mali za ndoa. Kwa sababu kwenye mgwanyo wa mali. Lazima Kwanza mali ziwe za ndoa na kuwe na uthibitisho kuwa mhusika amechangia kwenye upatikanaji wake. Na anachopata ni kulingana na mchango wake katika kuipata mali hiyo!
 
Then huyo mzee according to mwenendo wa kesi alifunga ndoa ya kiserikali na baadae akaenda kuibariki kanisani. Ndoa ya kiserikali je ina limit ya idadi ya wake?
Ndoa ya serikali Kwa Hali ya kawaida ni ndoa ya mke mmoja mune mmoja. Lakini inaruhusu kuongeza mke, Kama wakati wa kufunga mume uliweka wazi kuwa itakuwa potential monogomous. Yaani ni ndoa ya mke mmoja ambayo huko mbeleni inategemewa kuongeza mke!
 
Ndoa ya serikali Kwa Hali ya kawaida ni ndoa ya mke mmoja mune mmoja. Lakini inaruhusu kuongeza mke, Kama wakati wa kufunga mume uliweka wazi kuwa itakuwa potential monogomous. Yaani ni ndoa ya mke mmoja ambayo huko mbeleni inategemewa kuongeza mke!
Ahsante, nimepitia hapo kwenye sheria nikaona. Kwa hapo vipo vitu viky atapoteza maana sheria tanzania haitambui concubine. Ila kuna vitu naamini kashiriki kuvinunua. Pia watoto wakipata hivyo vitu wavitumie na kuviendesha kwa hekima kubwa. Vitu vilivyopiganiwa mahakamani vina vingi ndani yake. Mungu awayangulie.
 
Umenikumbusha mbali alitikisa ndoa ya Amina Chifupa huyu, hadi Amina alikuwa hapigi wimbo wake kwenye kipindi🤣
 
Inasikitisha sana.

Pole sana Isaack kwa unachopitia.

Haya tuliyajua mapema.
 
Mbunge msitaafu wa viti maalum ambaye baadae alifunga ndoa na katibu mkuu wa fedha enzi za Kikwete ,Vick Kamata amekwaa kisiki baada ya mahakama kutupa madai yake ya kutaka yeye ndiyo awe msimamizi wa miraithi ya mali za marehemu Likwelile.
Mahakama imempa haki zote mtoto mkubwa wa kiume wa marehemu Likwelile.

 
Wanaume mambo Kama haya ndo yanatufanya tusite kujitoa 100 kwenye familia, mnabaki mnalaumu hamjui mishahara yetu inaenda wapi.

Hivi kweli ujanani nijitoe tufanye maendeleo, sivai vizuri, human hair na dish dash za Dubai nazionea insta, najikaza tuinvest Kwa ajili ya watoto.....inafika utuuzimani unababaishwa na madako ndoa inakuwa haieleweki, halafu ukifariki mtu anaanza kusumbua hivi kubeba Mali za watoto, tena zenye jasho la mke wa awali....kisa alikata viuno sijui miaka 6 au 7, tena alikukuta welloff...

Serikali iendelee kuwapa waganga vibali, tutarogana sana Yani....Hukumu ya haki itajulikana kwa Mungu, hapa duniani tutaokoteshana sana makopo manina....
 
Kimenisikitisha hicho Kingereza kilichopo kwenye hukumu.

Dah, Tanzania tuna safari ndefu sana ya kwenda. Ikiwa judge ndio hivyo, judegement si itatupiliwa mbali mahakama ya rufaa kwa lugha tu hiyo.
We bibi Judegement ni nini... ? Sema judgment bwana ... unakosoa kumbe nawewe zao la memkwa huna lolote.
 
Tatizo alitaka kujipatia vyote kama mke wa marehemu wakati marehemu alikua na mahawara saba wenye watoto plus watoto halali wa ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…