Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Kesi Namba Cc 32444/24 inayomkabili Saleh Ayoub (39), Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres iliyopo Mbezi Africana, mkazi wa Dar es salaam, anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi mwenye umri wa Miaka 11 imetajwa Mei 27, 2025 na kuahirishwa mpaka Juni 19, 2025.
Kesi hiyo ambayo iliendelea siku hiyo kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kutoa utetezi wake ilishindwa pia kusikilizwa katika hatua hiyo Mei 21, 2025 kutokana na sababu iliyoelezwa kwamba Wakili wa Mshtakiwa hakuwepo.
Hutua ya mshtakiwa kuanza kutoa ushahidi ilifikiwa baada ya upande wa Jamhuri kufunga ushahidi wao kwa kuleta mashahidi wanne kati ya sita pamoja na kielelezo kimoja kama ilivyoelezwa awali.
Itakumbukwa, mshtakiwa huyo alipandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza siku moja baada ya Mdau wa Jamiiforums.com kuhoji Walimu wa Shule ya Green Acres (Dar) wanaotuhumiwa kulawiti na kuwadhalilisha Wanafunzi, wanalindwa na nani?
Mei 27, 2025 Kesi ilitajwa ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Shule na Watu wawili waliruhusiwa kuingia Mahakamani lakini Mama wa Mtoto alipoingia aliambiwa hatakiwi.
Baada ya hapo Wakili Mkuu wa Jamhuri alikaa na Mama Mtoto kwenye chumba cha Mawakili na kumueleza ni haki yake kuwepo wakati kesi ikiendelea kwa kuwa anamuwakilisha mtoto wake ambaye ndiye muathirika katika shauri hilo.
Pia soma:
~ Daktari aliyemfanyia vipimo Mwanafunzi anayedaiwa kulawitiwa na Mwalimu wake, asema "Nilimkuta ameharibika sana"
~ Kesi inayomkabili Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayedaiwa kumlawiti mtoto yaahirishwa hadi Machi 24, 2025
~ Watu 6 kutoa ushahidi Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Green Acres anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake
~ Ushahidi wa Kesi ya Mwalimu wa Green Acres, Saleh Ayoub anayetuhumiwa kumlawiti Mwanafunzi wake kuanza kutolewa Februari 6, 2025
~ Kesi ya Mwalimu wa Shule ya Msingi Green Acres anayetuhumiwa kulawiti Mwanafunzi yaahirishwa Mwezi mzima, Hakimu apata udhuru