GE2025 Kesi ya Said Issa dhidi ya CHADEMA yaahirishwa hadi Septemba 10, 2025; nyaraka za mali na fedha zaombwa Mahakamani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kesi ya madai namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho imeendelea tena leo, Alhamisi Agosti 28.2025 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam

Kesi hiyo inayosikilizwa chini ya Jaji Hamidu Mwanga ilipangwa kuanza kusikilizwa rasmi leo, hata hivyo Mahakama imelazimika kuhairisha hadi Septemba 10 mwaka huu kutokana na maombi yaliyowasilishwa na wadai Mahakamani hapo

Awali, wakiwa Mahakamani hapo, Wakili Shaban Marijani anayewakilisha upande wa wadai ameieleza Mahakama kuwa mnamo Agosti 26 mwaka huu wateja wake wametuma maombi maalum upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) wakiomba kupatiwa nyaraka kadhaa walizozitaja kuwa ni muhimu kulingana na muktadha wa shauri husika

Ametaja nyaraka hizo kuwa ni pamoja na Taarifa za mali za chama, Ripoti ya ukaguzi wa mahesabu, Muhtasari na ajenda za vikao vya Bodi ya Wadhamini, Kamati Kuu ya chama, Kamati maalum ya Kamati Kuu Zanzibar, Sekretarieti ya chama Taifa, Sekretarieti maalum ya Zanzibar, Taarifa za Benki na zinazohusiana na fedha kwa ujumla wake, ambapo nyaraka zote hizo ni zile za kuanzia mwaka 2019 hadi 2024

Upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) kupitia kwa wakili wake Hekima Mwasipu umethibitisha kupokea maombi hayo, hata hivyo wameomba siku saba (7) za kujibu hoja hizo, huku upande wa wadai nao wakiomba siku tano (5) za kupitia majibu ya wadaiwa, maombi ambayo yamekubaliwa na Mahakama

Akitangaza hairisho la kesi hiyo Jaji Hamidu Mwanga amesema kwa kawaida Mahakama haiwezi kuendelea kusikiliza kesi ya msingi bila kuanza kusikiliza na kufanya maamuzi ya maombi madogo yaliyofunguliwa, hivyo baada ya Mahakama kusikiliza na kutolea maamuzi maombi hayo hapo Septemba 10.2025, tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya msingi itatajwa

Katika shauri hilo leo upande wa wadai umewakilishwa na Mawakili watatu (3) wakiwemo Shaban Marijani na Gido Semfukwe, huku upande utetezi ukiwakilishwa na Mawakili wanne (4) akiwemo Dkt. Rugemeleza Nshala, Hekima Mwasipu na Deogratias Mahinyila.

1756380793966.png

Attachments

  • VIDEO-Aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2.mp4
    25.7 MB
Nimegundua akina Said wapo kupoteza muda tu, hakuna jingine.

..kila kesi inapoahirishwa, kabla kesi haijaitwa tena, upande wa wadai unawasilisha ombi la dharura. Huo ndio mtindo wanaotumia kuchelewesha shauri.
 
Wajibu wa Mahakama ni kutenda haki, kwetu Mahakama inachelewesha haki.
 
Ccm hawaezi siasa za hoja. Hawawezi labda kwa kutegemea polisi .
One walivyomwaga polisi wenye silaha huko nje kisa wanazindua KAMPENI!
Yaani unazindua kampeni kisha unapeleka magari ya washawasha kuwatisha hao wapiga KURA?
CCM ni majangili tupu
 
CCM CHAMA CHA MAJAMBAZI
 
Kesi ya madai namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho imeendelea tena leo, Alhamisi Agosti 28.2025 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam

Kesi hiyo inayosikilizwa chini ya Jaji Hamidu Mwanga ilipangwa kuanza kusikilizwa rasmi leo, hata hivyo Mahakama imelazimika kuhairisha hadi Septemba 10 mwaka huu kutokana na maombi yaliyowasilishwa na wadai Mahakamani hapo

Awali, wakiwa Mahakamani hapo, Wakili Shaban Marijani anayewakilisha upande wa wadai ameieleza Mahakama kuwa mnamo Agosti 26 mwaka huu wateja wake wametuma maombi maalum upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) wakiomba kupatiwa nyaraka kadhaa walizozitaja kuwa ni muhimu kulingana na muktadha wa shauri husika

Ametaja nyaraka hizo kuwa ni pamoja na Taarifa za mali za chama, Ripoti ya ukaguzi wa mahesabu, Muhtasari na ajenda za vikao vya Bodi ya Wadhamini, Kamati Kuu ya chama, Kamati maalum ya Kamati Kuu Zanzibar, Sekretarieti ya chama Taifa, Sekretarieti maalum ya Zanzibar, Taarifa za Benki na zinazohusiana na fedha kwa ujumla wake, ambapo nyaraka zote hizo ni zile za kuanzia mwaka 2019 hadi 2024

Upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) kupitia kwa wakili wake Hekima Mwasipu umethibitisha kupokea maombi hayo, hata hivyo wameomba siku saba (7) za kujibu hoja hizo, huku upande wa wadai nao wakiomba siku tano (5) za kupitia majibu ya wadaiwa, maombi ambayo yamekubaliwa na Mahakama

Akitangaza hairisho la kesi hiyo Jaji Hamidu Mwanga amesema kwa kawaida Mahakama haiwezi kuendelea kusikiliza kesi ya msingi bila kuanza kusikiliza na kufanya maamuzi ya maombi madogo yaliyofunguliwa, hivyo baada ya Mahakama kusikiliza na kutolea maamuzi maombi hayo hapo Septemba 10.2025, tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya msingi itatajwa

Katika shauri hilo leo upande wa wadai umewakilishwa na Mawakili watatu (3) wakiwemo Shaban Marijani na Gido Semfukwe, huku upande utetezi ukiwakilishwa na Mawakili wanne (4) akiwemo Dkt. Rugemeleza Nshala, Hekima Mwasipu na Deogratias Mahinyila.

Hawana ushahidi wanasubiri wapewe nyaraka ndiyo waangalie matatizo!!!!
 
Hapana vipi kawe singasinga na rostam Azizi umewaona hapo???
Jana kadinali kaenda Chamwino kuonana na Bi Mdashi lkn Mahakamani anawatuma nyie waimba kwaya yeye kiguu na njia Ikulu. Kamtosa Lissu
 
..kila kesi inapoahirishwa, kabla kesi haijaitwa tena, upande wa wadai unawasilisha ombi la dharura. Huo ndio mtindo wanaotumia kuchelewesha shauri.
Mtu akikukaba kabali, anakuwa na nafasi ya kukudunda tu anavyotaka mwenyewe.
CHADEMA wamekabwa kabali mbaya sana hii; na kwa kuwa wasimamizzi na waendesha kesi nao wanazo 'interest' zao ndani ya kesi hii, usishangae kuona inachukuwa hata miaka kumalizika

Maana ya yote haya ni kwamba Zanzibar wanayo 'veto' power ya kuamua mstakabali wa hivi vyama vya upinzani.
Interests za mamilioni ya waTanzania zinazowakilishwa na CHADEMA zinazimwa na kundi dogo kabisa la watu.

Zanzibar kuna wanachama wangapi wa CHADEMA. Inawezekana kabisa hata elfu tano hawafiki.

Lakini mahakama haiwezi kuyaangalia haya mambo kwa mlango huo!

Sijui katiba ya CHADEMA inazungumzia ugawanaji wa mali za chama kwa uwaiano gani; au kuna maelekezo ya Msajili wa vyama inayosimamia maswala haya?
 
Back
Top Bottom