GE2025 Kesi ya Said Issa dhidi ya CHADEMA yaahirishwa hadi Septemba 10, 2025; nyaraka za mali na fedha zaombwa Mahakamani

GE2025 Kesi ya Said Issa dhidi ya CHADEMA yaahirishwa hadi Septemba 10, 2025; nyaraka za mali na fedha zaombwa Mahakamani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kesi ya madai namba 8323/2025 iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho imeendelea tena leo, Alhamisi Agosti 28.2025 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam

Kesi hiyo inayosikilizwa chini ya Jaji Hamidu Mwanga ilipangwa kuanza kusikilizwa rasmi leo, hata hivyo Mahakama imelazimika kuhairisha hadi Septemba 10 mwaka huu kutokana na maombi yaliyowasilishwa na wadai Mahakamani hapo

Awali, wakiwa Mahakamani hapo, Wakili Shaban Marijani anayewakilisha upande wa wadai ameieleza Mahakama kuwa mnamo Agosti 26 mwaka huu wateja wake wametuma maombi maalum upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) wakiomba kupatiwa nyaraka kadhaa walizozitaja kuwa ni muhimu kulingana na muktadha wa shauri husika

Ametaja nyaraka hizo kuwa ni pamoja na Taarifa za mali za chama, Ripoti ya ukaguzi wa mahesabu, Muhtasari na ajenda za vikao vya Bodi ya Wadhamini, Kamati Kuu ya chama, Kamati maalum ya Kamati Kuu Zanzibar, Sekretarieti ya chama Taifa, Sekretarieti maalum ya Zanzibar, Taarifa za Benki na zinazohusiana na fedha kwa ujumla wake, ambapo nyaraka zote hizo ni zile za kuanzia mwaka 2019 hadi 2024

Upande wa wadaiwa (Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA) kupitia kwa wakili wake Hekima Mwasipu umethibitisha kupokea maombi hayo, hata hivyo wameomba siku saba (7) za kujibu hoja hizo, huku upande wa wadai nao wakiomba siku tano (5) za kupitia majibu ya wadaiwa, maombi ambayo yamekubaliwa na Mahakama

Akitangaza hairisho la kesi hiyo Jaji Hamidu Mwanga amesema kwa kawaida Mahakama haiwezi kuendelea kusikiliza kesi ya msingi bila kuanza kusikiliza na kufanya maamuzi ya maombi madogo yaliyofunguliwa, hivyo baada ya Mahakama kusikiliza na kutolea maamuzi maombi hayo hapo Septemba 10.2025, tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya msingi itatajwa

Katika shauri hilo leo upande wa wadai umewakilishwa na Mawakili watatu (3) wakiwemo Shaban Marijani na Gido Semfukwe, huku upande utetezi ukiwakilishwa na Mawakili wanne (4) akiwemo Dkt. Rugemeleza Nshala, Hekima Mwasipu na Deogratias Mahinyila.

Itasomwa Hadi baada ya Uchaguzi Mkuu 🤣🤣
 
Alafu anajiita muislamu swafi kabisa katika kuitetea haki 😏
Nchi yetu haitaki tu kuyatazama haya maswala katika uhalisia wake. We are all in denial; sijui kwa faida ya nani.
Ukweli ni kwamba tupo kwenye mapambano ya kidini tayari.

Tuseme bayana, au tujifanye hatulijui hilo, hakuna kinachoondoa ukweli huo.
 
Back
Top Bottom