GE2025 Kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Septemba 10, 2025, Jamhuri kujibu mapingamizi

GE2025 Kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Septemba 10, 2025, Jamhuri kujibu mapingamizi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Kesi inayomkabili Tundu Lissu inatarajiwa kuendelea tena leo Septemba 10, 2025, ikiwa ni siku ya Tatu mfululizo, ambapo upande wa Jamhuri utaendelea kujibu mapingamizi yaliyowekwa na mshtakiwa ambaye anajitetea mwenyewe.

Lissu aliweka mapingamizi kiwa Mahakama Kuu aina mamlaka ya kusikiliza kusikiliza shauri kutoka kulalamikia mchakato wa committal court kwamba ulikuwa na dosari kwa kutofuata sheria.

Lissu tayari amewasilisha hoja zake kuhusu mapingamizi aliyoweka, sasa upande wa Jamhuri unangojewa kukamilisha utetezi wao kabla ya Lissu kutoa mjumuisho wa hoja zitakazokuwa zimewasilisha ili Mahakama iweze kutoa uamuzi.

Ikumbukwe Lissu alifikishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya mchakato wa kusomewa shtaka pamoja na maelezo ya shtaka, hata hivyo aliweka mapingamizi hayo ikiwemo kuhoji utofauti wa nyaraka aliyopoewa akiwa Gerezani kutofautiana na waliyonayo upande wa Jamhuri, ambapo anadai aliyonayo ina mapungufu.

1757482808906.png


#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
 
Back
Top Bottom