Nchi nyingine, Jaji ni nafasi ya heshima, lakini kwetu hapa, kuwa jaji ni sawa sawa na Polisi, msajili wa vyama vya siasa, mwenyekiti/mkurugenzi wa Tume ya uchaguzi, wakurugenzi wa Wilaya. Wote, hakuna mwenye weledi, wanafanya kazi kama tarishi, wanasubiria amri ya mwenyekiti wa CCM.
Kwa sasa hizo ni nafasi, kwa kiasi kikubwa ni alama ya ibilisi. Mpaka sasa, hakuna hata mmoja aliyeonesha kwa vitendo kuwa hataki ushirika na ibilisi. Hakuna aliyeonesha kuwa anataka kuwa mtumwa wa weledi wake, kama ambavyo watu wenye akili na weledi hupenda kuwa. Hawa wa kwetu wameamua kuwa watumwa wa CCM, na CCM ina ushirika wa kudumu na inilisi. By implication, nao wameamua kuishi kwenye ndoa na ibilisi. Siku zote ibilisi, lazima mwishowe akupeleke kwenye majuto.