PreGE2025 Kesi ya uhaini inaweza kuchukua miaka mitatu mpaka minne, hii ya Lissu inaweza kufika 2029

PreGE2025 Kesi ya uhaini inaweza kuchukua miaka mitatu mpaka minne, hii ya Lissu inaweza kufika 2029

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Haijalishi Lissu atakaa miaka mingapi jela.

Hata Mandela alikaa jela miaka 27 lakini haikuzuia Afrika Kusini kupata Uhuru.

Mfungeni hata Lissu maisha ila Mungu lazima aiokomboe Tanzania dhidi ya udhalimu wenu.
Lissu keshaona hamjielewi, kaamua Kula hela za Abdul ajitie kuvuruga amani akimbie uchaguzi kujifanya mhaini awaache na unyumbu wenu. Baada ya uchaguzi anaachiwa anaenda zake ubelgiji.
 
Haijalishi Lissu atakaa miaka mingapi jela.

Hata Mandela alikaa jela miaka 27 lakini haikuzuia Afrika Kusini kupata Uhuru.

Mfungeni hata Lissu maisha ila Mungu lazima aiokomboe Tanzania dhidi ya udhalimu wenu.
Mzeee haki haipatikani Kwa maneno Africa
 
Hatakaa muda mrefu mahabusu ikizidi sana miaka minne
 
Enzi za Mwalimu sio kwamba kulikuwa hamna Mawakili wenye uwezo, watu waliogopa Mkono wa chuma. Wewe unawajua Mawakili maarufu, bongo hii kuna Mawakili ni alumnus wa Harvard and Stanford Law schools, wapo bongo hii, usitishe watu kwa "exposure" yako finye juu ya Mawakili na Uwakili.
Nani huyo?
Pia wenda ulihadithiwa, ule wa Mwalimu ulikuwa uhaini kweli wa silaha na watu walikufa, yalikuwa sio masihara wala mzaha wala sio siasa, yalikuwa ni Maasi ya Vita na Mchonga kweli alitingwa. 😁

Kuhusu muda: Kwani Lissu akiwekwa kizuizini mpaka 2030, harakati zitaisha?.
 
Kwahiyo policcm na mahakama ccm hicho ndio mmekaa mkajadili mkaona Lissu akikamatwa na kubambikiwa kesi ndio no reform no election itakufa?

Mnaweza kumuua mtu ila fikra zake bado zikaishi na wakazaliwa wengine zaidi.

Magufuli alijinasibu ataufuta upinzani , ila hadi leo hii yeye ndio hayupo policcm wanacheza ngoma za Chadema kwenye mikutano na kutumia nguvu nyingi kwa watu wasio hata na fimbo mkononi zaidi ya simu na scarf.
 
Yes ni Kesi ya kubumba same kama ile ya Ugaidi wa Mh. Mbowe ambao mwisho wake aibu kwa CCM baada ya kushindwa kuthibitisha huku wakiwa wametumia mabilkion ya hela za watanzania maskini kwa kesi hiyo.

Werevu tulijua ule mziki wa No reform CCM haiwezi kuuhimili- wameona wapumue kidogo kwa kumuweka Lissu ndani.

CCM kila siku tunasema ni chama ambacho kishapoteza uelekeo kwa wananchi. Sasa mziki wa Mbinga tu wakaonana ohooo huyu Lissu hakamatiki tumuweke ndani kwanza tupumue.
 
Kesi za uhaini ni kesi ngumu sana, na huchukua muda mrefu kumalizika. Hii inaweza kufika hata 2029. Na hapa sioni mawakili wa kiwango cha Lakha aliyesimamia kesi ya uhaini enzi ya Nyerere.

Soma Pia: Tundu Lissu ashtakiwa kwa Uhaini, arudishwa rumande, kesi yake kusikilizwa Aprili 24, 2025

Siasa sio kibali cha kuvunja sheria
ichukue hata miaka 100 lakini ukweli ni kwamba hakuna UCHAGUZI TANZANIA BALI KUNA UCHAFUZI. Na ccm hakiwezi kujibu hoja za washindani wake. chama hiki kinategemea dola tu basi
Bado tunangoja tuambiwe DUKA LA VIRUSI VYA EBOLA NA MPOX tukanunue huko. makala atuambie na bei yake
 
Unadhani historia itakukumbuka kwa haya? Au alimradi unatimiza matakwa ya mabwana zako(your lords)
 
Tutaendelea kuutembelea huu uzi na tutajua atakayecheka mwishoni .

Maana dalili zipo tutaambiwa watu wako fit wanachapa kazi kumbe hata ofisini hawapo tena.

Hakuna kuukimbia uzi.
 
Dk. Slaa aliomba poo ndio ikaisha, mahakama ya chini ikijikoroga tunapeleka notice of appeal, faili linakaa parking kwa miezi kadhaa
Roho mbaya puo zetu wote zimeinama chini,mtu alisema akiwa Belgium je Nina hakikishiwa siasa huru na salama.wakasema.haina.shida.sasa.mnaweka.kizuizini gerezani ili iweje wakati alisema naomba mnihakikishie usalama.
Hapa kinachofuata Bora kuomba sick sheet kwenda kuchekiwa risasi yetu kiunoni,mtu ana risasi kiunoni hata soni hamuoni kumweka korokoroni.
 
Roho mbaya puo zetu wote zimeinama chini,mtu.alisema.akiwa.Belgium je Nina hakikishiwa siasa huru na salama.wakasema.haina.shida.sasa.mnaweka.kizuizini gerezani ili iweje wakati alisema naomba mnihakikishie usalama.
Hapa kinachofuata Bora kuomba sick sheet kwenda kuchekiwa risasi yetu kiunoni,mtu ana risasi kiunoni hata soni hamuoni kumweka korokoroni.
Alisema anakuja kuanzisha uasi kwa kuunda vikosi vya kutumia silaha, alivuka mstari wa amani
 
Tutaendelea kuutembelea huu uzi na tutajua atakayecheka mwishoni .

Maana dalili zipo tutaambiwa watu wako fit wanachapa kazi kumbe hata ofisini hawapo tena.

Hakuna kuukimbia uzi.
Karibu sana tumshikishe adabu huyo jamaa
 
Hakuna Uhaini humo bali ni uhuni wa CCM - Lissu atatoka mapema tu kabla hata ya July.
 
Back
Top Bottom