GE2025 Kesi ya Uhaini inayomkabili Lissu kuendelea leo kwa kusikilizwa mfululizo hadi Oktoba 24, 2025

GE2025 Kesi ya Uhaini inayomkabili Lissu kuendelea leo kwa kusikilizwa mfululizo hadi Oktoba 24, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Kesi ya uhaini, Jamhuri dhidi ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu A. Lissu inatarajiwa kusikilizwa mfululizo kuanzia Jumatatu, saa 4 asubuhi 06.10.2025 hadi 24.10.2025 na kuendelea kuanzia 03.11.2025 hadi 12.11.2025.

Kesi itasikilizwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, Ukumbi Na. 1. Maandalizi yamekamilika. Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu A.M Lissu yupo imara kimwili na kiakili

Kama ambavyo mnafahamu, Tundu A.M Lissu katika shauri hili anajitetea mwenyewe, hivyo amejiandaa vizuri sana kushughulika na mashahidi wa kificho wa Jamhuri katika kesi hii – gizani.

Tunaanza kusikiliza mashahidi upande wa Jamhuri na vielelezo vyao ikiwepo ‘flash’ yenye uhaini. Upande wa Jamhuri una mashahidi 30 na vielelezo 11. Tupo tayari kusikiliza ushahidi.

NB; Tundu A.M Lissu alieleza Mahakama iwaelekeze Mawakili wa Serikali, mashahidi wao waelezwe kwamba wasipoteze muda wa Mahakama katika kuthibitisha sauti na picha zake, NI YEYE.

Update

Kupitia ukurasa wa X wa Chadema wanadai baadhi wananchi waliofika kufuatilia kesi wamepigwa.

FB_IMG_1759727197745.jpg


Fuatilia mwenendo wa Utetezi

 
Wamuachie tu, maana kina capitaine tesha wamejaza ombwe aliloliacha, ngoma inogile
 
Nchi hii inamauzauza mengi sana, wamepanga mtililiko wa siku nyingi kama kunamambo mengi ya kuongea vile ni upuuzi mtupu.
 
Kila la heri Tundu Lissu
Upo unaonewa na Deep state, hao mafisadi siku zao zinahesabika
 
Back
Top Bottom