Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 143,138
- 288,731
Hii kesi itakuwa Mubashara, kwahiyo kila mmoja atajionea Mwenyewe hoja kabambe.
Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea Mwenyewe
Tundu Lissu amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu
Hivi ndivyo Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu alivyofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar Es Salaam kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.
Makamu mwenyekiti wa CHADEMA bara John Heche pamoja na katibu wa cha hicho John Mnyika pia amefika Mahakamani.
Lissu agoma kesi yake kuahirishwa
Mtumuhiwa wa kesi y uhaini, Tundu Lissu amegoma kesi ya uhaini inayomkabili isiahirishwe kwa sababu yoyote ile amesema hakuna sababu yoyote ya msingi yakuahirishwa kwa kesi hiyo.
Maombi ya Mshitakiwa yametekelezwa
Mshitakiwa katika kesi ya Uhaini Tundu Lissu amesema baada ya kuomba, badhii ya mahitaji yake akiwa mahakamani ameanza kupatiwa nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja na anapata hewa safi, kuonana na mawakili wake na pia aliletewa Padri kwaajili ya maombi lakini Tundu Lissu amesema licha ya haya yote sio sababu ya yeye kuendelea kubaki Gerezani.
Mshitakiwa Lissu kuhusu Msajili wa vyama vya siasa
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu ameiambia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa hana mamlaka ya kukizuia Chama hicho kushiriki shughuli za siasa kwenye mwaka wa uchaguzi.
Mbali na hilo pia Lissu ameiomba mahakama hiyo kuwa kama upelelezi ama ushahidi haujakamilika basi aachiwe huru kwa sababu mara ya mwisho waliambiwa upelelezi umekamilika na jalada lipo wa DPP.
Lissu ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franko Kiswaga wakati lilipotajwa shauri la uhaini ambapo ilitarajiwa upande wa Jamhuri kutoa taarifa juu ya uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kama kesi hiyo iende Mahakama Kuu ama lah.
Lissu alisema kuwa anaiomba mahakama hiyo isiahirishe kesi kwa sababu hakuna sababu ya msingi, kwani mara ya mwisho waliambiwa upelelezi umekamilika na wangepewa taarifa ya uamuzi.
Hakimu kasema ni kweli hoja za Tundu Lissu zinaeleweka lakini hana kifungu Cha kuamua dhidi ya malalamiko ya mtuhumiwa, mahakama haiwezi kumuamrisha DPP afute kesi au apeleke kesi kwenye mahakama kuu, hivyo basi hakimu akaipa jamhuri siku 14 Tena ndipo watakapokutana yaani tarehe 15.07.2025.