Kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu kuendelea kesho Julai 3, 2026

Kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu kuendelea kesho Julai 3, 2026

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Wakuu,

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa kesho Ijumaa, Julai 3, 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania itakayosikiza jijini Dar es Salaam maombi ya marejeo Na. 7440840/2026 yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Antipas Lissu

Soma Pia: Kesi ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu iliyopangwa kusikilizwa Juni 11, 2026 yaahirishwa hadi Julai 6, 2026

Kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA, maombi hayo yatasikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, ambao ni Jaji Mwarija, Jaji Muruke na Jaji Khamis.

Chama hicho kimesema usikilizwaji wa shauri hilo unatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, na kimewaalika wananchi, wanachama, wafuasi pamoja na wadau wa demokrasia kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

1782996229124.png


​
 
Naamini hapatakuwepo simu za kupokelewa na majaji wala hairisho la ghafla
Polisi nao wawe sehemu ya kufuatilia kesi na siyo kuzuia wafuatiliaji wa kesi
 
Back
Top Bottom