Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa kesho Ijumaa, Julai 3, 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania itakayosikiza jijini Dar es Salaam maombi ya marejeo Na. 7440840/2026 yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) dhidi ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Tundu Antipas Lissu
Kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA, maombi hayo yatasikilizwa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, ambao ni Jaji Mwarija, Jaji Muruke na Jaji Khamis.
Chama hicho kimesema usikilizwaji wa shauri hilo unatarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi, na kimewaalika wananchi, wanachama, wafuasi pamoja na wadau wa demokrasia kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Naamini hapatakuwepo simu za kupokelewa na majaji wala hairisho la ghafla
Polisi nao wawe sehemu ya kufuatilia kesi na siyo kuzuia wafuatiliaji wa kesi