PostGE2025 Kesi ya Uhaini inayowakabili vijana 3 yapigwa tena kalenda hadi Machi 16

PostGE2025 Kesi ya Uhaini inayowakabili vijana 3 yapigwa tena kalenda hadi Machi 16

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kesi mbili (2) tofauti zinazowakabili vijana watatu (3) wanaodaiwa kuvunja, wizi na kukutwa na mali zinazodhaniwa kuwa ni za wizi zimetajwa leo Mahakamani hapo kwaajili ya kutolewa uamuzi

Hata hivyo uamuzi wa kesi zote umeshindwa kutolewa, badala yake zimehairishwa hadi Machi 16.2026 ambapo imeelezwa kuwa sababu zilizopelekea kukwama kutolewa uamuzi ni kufuatia Hakimu Mkazi Mkuu Hassan Makube anayesikiliza kesi zote kutowepo Ofisini leo (amepata dharura),

Hata hivyo, vijana hao wameendelea kusota gerezani kutokana na kesi nyingine inayohusu mashtaka ya uhaini inayowakabili, na walifikishwa Mahakamani hapo kwa mara ya kwanza kusomewa mashtaka hayo (ya uhaini) Novemba 2025 wakidaiwa kuhusika na maandamano yaliyozaa vurugu zilizotokea Nchini Oktoba 29.2025 (Siku ya Uchaguzi Mkuu) na siku zilizofuata, vurugu zilizopelekea uharibifu wa mali za umma na binafsi, na vifo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa kwenye viunga vya Mahakama hiyo, Wakili wa utetezi Maduhu Willium kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC amemuomba Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) kuharakisha upelelezi wa mashtaka ya uhaini ili washtakiwa wafikishwe Mahakama Kuu kwaajili ya kusikilizwa kesi hiyo, au wafutiwe mashtaka yao

 
Back
Top Bottom