Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Tundu Lissu leo, Alhamisi Septemba 24.2026 anaendelea kuwasilisha 'Final Submission' zake Mahakamani katika kesi ya uhaini inayomkabili, zoezi aliloanza nalo hapo jana
LISSU ambaye anajitetetea mwenyewe kwenye kesi hiyo, inayosikilizwa 'mfululizo' kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam mbele ya jopo la Majaji watatu (3) wakiongozwa na Jaji Dastan Ndunguru, endapo atakamilisha zoezi hilo mapema, basi upande wa Serikali (Jamhuri) nao watafanya zoezi hilo wakitumia muda uliosalia kuelekea kesho, ambapo kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa na Mahakama ndio itakuwa siku ya mwisho ya usikilizwaji wa kesi hiyo,
Ikumbukwe kuwa, hatua hii ya pande zote mbili (3) yaani upande wa Mashtaka (Serikali/Jamhuri) na ule wa mshtakiwa Tundu Lissu kuwasilisha 'Final Submission' inakuja kufuatia pande zote kukamilisha kutoa ushahidi wake, ambapo Jamhuri ilifunga ushahidi wake baada ya kuwaleta Mahakamani mashahidi 17, wakati upande wa utetezi uliwaleta Mahakamani mashahidi watano (5) wakiongozwa na mshtakiwa mwenyewe.
Baada ya usikilizwaji wa kesi hiyo kumaliza, hatua itakayokuwa inasubiriwa na pande zote mbili (2) na wadau wengine wa ndani na nje ya Nchi wanaofuatilia kwa karibu KESI hiyo ni kuona uamuzi utakaotolewa na Mahakama.
====
LIVE UPDATES | MATUKIO KUTOKA MAHAKAMANI - Sept. 24, 2026
Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu Mkuu, John Mnyika tayari wapo ndani ya chumba cha Mahakama Kuu, kufuatilia kesi ya Tundu Lissu ambaye ameiambia Mahakama wanaostahili kunyongwa wapo mtaani waliouwa ndugu zetu Tarehe 29.10.2025.
Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Boniface Jacob amewasili Mahakamani
TUNDU LISSU AWASILI MAHAKAMANI KUKAMILISHA MAJUMUISHO, KESI YA UHAINI INAYOMKABILI
Mahakama imeanza, kaa tayari kwa ajili ya kukujuza nini kinaendelea kwenye majumuisho ya leo ambapo Septemba 34, 2026 tuliishia Sehemu ya 446 na leo tubaendelea na;
Sehemu ya 447
Majaji wameingia Mahakamani na Mhe. Tundu Lissu nae ameingia Mahakamani na kupokewa kwa makofi mengi hapa.
Amepiga kinyaturu na ndugu zake waliopo hapa Mahakamani, amesema NINA KWETU NA NILIAGA VIZURI.
Anasimama Ajuaye na kuwataja wenzake anaoshirikiana nao na kusema wako tayari kuendelea.
Majaji wanateta kidogo pale juu kidogo na kumuuliza Mshitakiwa kama yuko tayari. Mh. Lissu nae anajibu niko tayari Waheshimiwa majaji akiwa amekaa na anaandika andika pale kizimbani.
Jaji Ndunguru tuendeleee sasa.
Mhe. Lissu anaanza.
Waheshimiwa Majaji nikumbushwe nilipoishia.
Uliishia pale kwenye kesi ya Mbowe.
Sasa Wahehsimiwa Majaji naomba kabla sijasema kuhusu ushahidi naomba niseme kitu muhimu ambacho Mahakama hii ilisema kwenye kesi ya Freeman Aikael Mbowe.
Madhara ya kutofafanua essential elements ambazo zimetajwa kwenye sheria wakati unaandaa hati ya Mashitaka. Ni muhimu hiki nitakachokisoma kiingie kwenye rekodi sawasawa.
Kama nilivyosema Mahakama Hii ilikuwa inajadili kushindwa kwa upande wa Mashitaka ku disclose essential particulars za lawful authority kwamba maana yake ni nini hizo mamlaka halali.
Ukurasa wa 53 wa Hukumu kwenye hiyo kesi ya Freeman Aikael Mbowe ilisema statute must give fair notice or warning to those subject to them. They must guard against arbitrary and discriminatory enforcement and they must not unreasonably guard people .....
Zilinde watu dhidi ya matumizi holela mamlaka ndio sheri zinapaswa kufanya kazi hiyo.
Muhimu zaidi Mahakama hii ilisema yafuatayo; Such statute must be intepreted strictly under the overbread doctrine. Lazima zitafsiriwe kwa umakini mkubwa ili kulinda haki za watu.
Over bread dotrine if the statute is broadly written that it deter free speech then it can be strucked out on its face because of its chill effect. Even if it also prohibit acts that may legitimately be forbidden.
Kama sheria imeandikwa haina limit na inanyima watu haki yao ya kusema Hii Doctrine inasema Mahakama inaweza kuifuta.
Hii overbread maana yake iko kwenye Blacks Law Dictionary 7th Edition.
Mahakama hii kwenye kesi ya Freeman Mbowe ilimalizia kwa kucite Isdory Patrice kwa kusema maneno yafuatayo ukurasa wa 58. The failure to name lawful authority targeted by the utterances prejudiced the first accused in his defence and denies the Court an objective criterion upon which it can evaluate if the the words in question were calculated to achieve the act of conduct said to seditions. In view of the aforesaid the charge was defective.
Nairudia tena. Anarudia tena kusoma Mahakama Kuu ilichosema kwenye kesi ya Mbowe kama ilivyo hapo juu.
Kwa kifupi.. Hati ya Mashitaka inayosema alichochea umma. Umma ni watu wote wa Tanzania Bara, wageni wasio wageni, watoto wachanga. Kila mtu aliyepo Tanzania bara ni umma. Hayo maneno yasipofafanuliwa hakuna namna ya kujitetea. Kwahiyo Mtuhumiwa hawezi kujitetea.
Leo unaambiwa wa Mtwara, kesho kutwa wa Nanyumbu ndo maana Mahakama inasema lazima yafafanuliwe na yasipofafanuliwa hati ya mashitaka ni batili.
Maneno yaliyopo kwenye hati ya mashitaka kwenye shitaka langu imeingiza neno umma halipo kwenye sheria na pili halijalifafanua. Kwasababu hiyo ni hati ya mashitaka batili.
Waheshimiwa Majaji baada ya kusema hivyo nijibu swali nililoliacha jana. Je ushahidi unasemaje?
Ukiachana na kuwa legally defective je ushahidi nao pia unasema nini?
Sehemu ya 448
Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Hapa Nazungumzia ushahidi unaohusu nia ya kuchochea umma iliyoletwa na hawa walionishitaki.
Nia ya kuchochea umma kuzuia Uchaguzi mkuu wa mwaka jana kwanza nilishasema nia yenyewe haipo kisheria hiyo ya kuzuia uchaguzi nitaelezea baadae.
Sasa jambo la kwanza.
Katika mashahidi 17 wa Mashitaka waliokuja kutoa ushahidi ni mashahidi wanne tu ambao walitoa ushahidi kuhusiana na suala hili.
Mashahidi hao ni PW1 George Bagyemu; PW2 John Kaaya, PW16 Amin Mahambana PW 17 aliyepewa jina la gizani la P.
Hao ndio walitoa ushahidi juu ya nia ya kuchochea umma kuzuia uchaguzi mkuu.
Jambo la Pili.
Watatu kati ya hao mashahidi wanne ni Mapolisi, mmoja tu PW17 ndio hakuwa polisi.
Jambo la tatu.
Watatu kati ya hao wanne hawakuwepo kwenye huo Mkutano, hakuhudhuria na mmoja tu PW 17 ndio alikuwepo kwenye Mkutano.
PW 17 ni shahidi pekee ambae ni eye witness katika mashahidi wote 17 aliyeona na kusikia yaliyotokea kwenye Mkutano. Wengine wote sio eye witnesses, wameona mitandaoni.
Hayo mambo matatu ni muhimu kama nitakavyoonesha shortly.
Huyo PW 17 sio tu aliona na kusikia ndo aliyerusha Matangazo. For now it suffices to say PW 17 ni mwandishi wa habari aliyesema kuwa alirusha matangazo kwenye mtandao wa Jambo TV.
Waheshimiwa Majaji kesi ya Upande wa Mashitaka imejengwa kwenye nini?
Kesi yao imejengwa kwenye ushahidi wa PW 1, PW 2 na PW 16. Hao Mapolisi ambao hawakuwepo kwenye mkutano. The theory of the case is built on their Evidence, what is this theory of the case.?
Dhana ya kesi hii ni kwamba Mimi mshitakiwa nilichochea umma kwa kuzungumza maneno yale yapo kwenye hati ya mashitaka kwa lengo la kuitishia Serikali kwasababu moja tu. Serikali ndio inasimamia Sheria za nchi na kwasababu Uchaguzi upo kwa mujibu wa sheria basi niliitishia serikali.
Hiyo ndio dhana yao. That is their theory. Ukiuvuruga Uchaguzi unakuwa umeitishia serikali. That is entire basis of this case.
Hiyo nadharia imetokana na ushahidi wa hawa Mapolisi watatu.
Tuanze na PW 1 George Bagyemu Waheshimiwa Majaji PW 1 ndie aliyepewa taarifa kwamba kuna video ina maneno ya kijinai na alipewa taarifa na PW 2. Tar. 04/04 siku moja baada ya ule mkutano.
Kwenye ushahidi wake PW1 alisema nini juu ya nia ya kuichochea serikali. Ukurasa 146 wa rekodi. Anazungumzia kilichomfanya aamini kuna nia ya uhaini.
The factors which led me to conclude it was a treason offence is
"The accused words that atahamasisha uasi, atavuruga sana, atazuia uchaguzi, atakinukisha sana sana, atakinukisha vibaya sana"
Hicho ndio kilimfanya askari Polisi George Bagyemu kusema ule ni uhaini.
Kwa maoni yake akasema pia These words were communicated with the intention of threatening the Executive.
Akaendelea kusema I say so because the election is held as per constitution and the law.
Akaendelea kusema The Executive Enforces the Law. He intimidated the Executive for the purpose of violating the Law which it enforces.
Kesi yote ipo hapo.
Mtakumbuka kwamba PW 1 was subjected to weathering cross Examination.
Kwenye Cross Examination PW 1 alisema kwamba sio kusema alikiri kwamba kwenye hayo maneno hakuna neno SERIKALI wala hakuna Serikali ya JMT, Wala Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Hakuna Rais wa JMT Samia, wala Makamu wa Rais, Isdory Mpango, wala Mkuu wa Mkoa Chalamila na zaidi ya hayo hakuna maneno Halmashauri ya Jiji Dar es salaam Temeke au Ubungo.
Na kwa maneno yake alisema no desgnation of any Executive leader mentioned by the treason words kwahiyo hiyo serikali wanayosema ilitishiwa hiyo Serikali yenyewe haipo na viongozi hawapo.
PW 1 licha kusema Serikali haipo lakini alisisitiza words to EXECUTIVE was intended to be intimidated.
Alisema yafuatayo kwenye ukurasa wa 166 wa record when a person says kukinukisha sana he commits Treason.
Sehemu ya 449
Lissu anaendelea kufanya mawasiliano yake ya mwisho (Final submission)
Anasema Shahidi huyo akaendelea kusema the words kukinukisha sanasana, vibaya sana are not provided in section 39(2)(d) of Penal Code lakini uchaguzi unasimamiwa na Sheria kwahiyo ni kosa.
Amekubali maneno hayo hayapo kwenye kifungu kinachotengeneza kosa la Uhaini na ukiyasema tu umefanya kosa la Uhaini.
Huo ndio ushahidi mnaoshawishiwa mtoe hukumu ya Kunyongwa? Huo ndio ushahidi wa Uhaini.? Ushahidi wa kunyonga mtu. hawana hata aibu.
Jaji sasa mshitakiwa huko usiende sana
Mhe. Lissu anajibu Perfectly ligitimately mimi kuumizwa na maneno haya kwamba nimekaa ndani kwa mambo haya. Acha niseme.
Anaendelea.
The evidence on record suggest once PW 1 complained ghat words was treasonous kila mtu hadi mawakili wa serikali akili zao zikawekwa mfukoni na wakaamini kila kitu kuwa yale maneno ni uhaini. Hawakuwahi kufikiria vinginevyo.
Alipoamua kuwa huu ni Uhaini hakuna kitu chochote ambacho kingebadili mawazo yake.
Mfano unamuhusu alipoulizwa PW 17 aliyekuwa shahidi wa kuona na kusikia wala hakuona tatizo lolote la kihaini wala kikosaji huyu PW 1 alisema yafuatayo;
Ukurasa wa 169 alisema hivi it is true that in his statement P ndio PW 17 said you were discussing challenges facing you in your constituency he were also said you were airing up your police of no refomrs no election. I read his statement and decided to open up the treason case. It was me who ordered the open up of the file of treason case.
Ni kweli P alisema mlikuwa mnajadili sera yenu ya no reforms nimesoma maelezo yake na nikaamua kufungua kesi ya Uhaini. Ni mimi ndie niliyeamua kufungua file la Uhaini baada ya kupitia ushahidi wote. Kielelezo D16 ndio maelezo ya PW 17. Hayo maelezo hayajasema kulikuwa na kosa lolote.
Huyu Polisi amesoma maelezo ya shahidi wake na kwa vile alishaamua kuwa ni uhaini huu akasema fungua file la Uhaini. Nothing was going to change him. Alipoulizwa baada ya mimi kumuhoji sana. Katuga alimure examine.
Kwamba unasemaje kuhusu hayo maneno yanaweza kuicover serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa vile alishasema serikali haipo sasa ukurasa wa 176 majibu yake yakawa hivi.
The words quoted contexually reffred to Executive. Kwa muktadha wake sio yanasema ila muktadha.
Muktadha ni intepretation, akaendelea kurudia ile Mantra yale maneno unasema kila siku Baba yetu uliye mbinguni.
Kwamba Serikali inasimamia Sheria na uchaguzi unaendeshwa kwa katiba.
Election is held as per law and Constitution and the Executive is the only arm enforces the law. The word Executive exists.
Kwenye maneno tunayolalamikia hayapo lakini yapo. Contexually. Na baadae tukaambiwa constructive. Kisichokuwepo kinaletwa.
Huo ni ushahidi wa PW 1. Na aliposema hayo huo ndio ukawa msimamo wa kila Polisi aliyekuja hapa kutoa ushahidi.
Pw1 testimony set the tone for the three other police witness. For the two sio three.
Yeye PW 1 aliposema kwamba maneno yale ya uhaini kila polisi alisema hivyo hivyo. Ushahidi wao ulifanana kama sare zao za Polisi.
PW 2 alisema hivi, I construed the words tutaenda kuzuia uchaguzi kwasababu tunasema tutaenda kuhamaisha uasi as contain elememt of criminality because th election is conducted according to the constitution and the law.
Therefore kuharibu uchaguzi obstruction without comply to the law manifest the intention to intimidate the Executive which is the principle enforcer of the law and maintainer of peace...
Hayo maneno kwamba uchaguzi unaendeshwa kwa katiba na Serikali ndio inasimamia sheria ni maneno yaleyale kutoka kwa George Bagyemu. Ukurasa wa 183 uko hivyo.
Kwasababu ilishakuwa artice of faith huyo PW 2 kwenye cross examination PW 2 hakubadilika ndio yakawa majibu yake kwamba ni uhaini kwasababu uchaguzi upo kikatiba na serikali inasimamia kwahiyo umeitisha.
Sehemu ya 450 inafuata hapa....