Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu iliyoahirishwa kupisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, inarejea leo Jumatatu, Novemba 10, 2025.
Kesi hiyo inayosikilizwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Iringa, Dunstan Ndunguru akishirikiana na James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, ilianza kusikilizwa ushahidi Oktoba 6 mpaka 24, 2025.
Ilipangwa kuendelea baada ya kumalizika uchaguzi huo Oktoba 29, 2025, kwa siku 10 za kazi, kuanzia Novemba 3 mpaka 12, 2025.
Hata hivyo, Novemba 3 kesi haikuendelea kutoka na athari za uchaguzi huo, kufuatia maandamano katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam na katika mikoa mingine, hali iliyoilazimu Serikali kusimamisha shughuli mbalimbali zikiwamo za kiofisi.
==
Tayari kaka wa Lissu, Wakili Msomi Alute Mughwai Lissu amefika Mahakamani ili kufuatilia shauri linalomkabili ndugu yake ambaye kwa sasa anasimama kujitetea mwenyewe.