PostGE2025 Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea Februari 9 hadi Machi 6, 2026

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
​

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano, Brenda Rupia ametoa taarifa hii iliyotolewa na
Gaston Galubindi, Mkurungenzi wa Sheria CHADEMA Taifa, kuhusu Kesi ya Uhaini ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA);

Chadema inawafahamisha kwamba kesi ya uhaini dhidi ya Mhe Lissu, Criminal session case No. 19605/2025 imepangwa kuendelea Mahakama kuu, Kanda ya Dar Es Salaam kuanzia tarehe 09 February 2026 hadi tarehe 06 March 2026.

Ikumbukwe kwamba kesi hiyo inasikilizwa na Majaji watatu, Mhe Jaji D. Ndunguru, Mhe Jaji J. Karayemaha na Mhe Jaji Kiwonde.

Tayari Mhe Lissu jana alipokea taarifa rasmi kutoka kwa Naibu Msajili wa Mahakama kuu.

​
Soma:
 
lisu akiwa na kesi hua nafuu sana kwa watumishi mana siku huyoyoma sana ila nihatari kwa wanaokaribia kustaafu na hawana wala boma mafao yatoke wamalizie
 

Kesi imefikia patamu. Je Tutaamini kuwa haki itatendeka katika muhimili huu wa Mahakama hii huru ya Tanzania chini ya Jaji Mkuu George Masaju?

Picha maktaba: Jaji mkuu George Masaju akihoji maelekezo toka juu

Je Mahakama yetu itajibanisha kuwa ni huru tofauti na ile ambayo Nelson Mandela na wenziwe walisimama mbele ya Mahakama iliyokuwa chini ya utawala gandamizi wa wachache ulioamini katika kubagua raia wa Afrika ya Kusini.

KESI IMEFIKA PATAMU, SASA DUNIA YOTE ILIYOKUWA HAIFAHAMU YA SASA YA UTAWALA WA SAMIA YATAANIKWA NA KUFAHAMIKA KINAGA UBAGA

Picha maktaba: Jaji mkuu George Masaju

Kesi hii ya Tundu Lissu itakuwa ktk vitabu kama kesi ya serikali ya makaburu dhidi ya Nelson Mandela. Kesi hii itasomwa ktk historia baada ya CCM kungolewa kutoka madarakani

Ifahamike katika mabano neno 'mahakama' ni kuwa CCM inataka kuburuza Mahakama zitumike vibaya pamoja na mfumo wa kusimamia / kuchunguza haki jinai (criminal justice system) nzima

Lakini imani yetu itapinwa baada ya kusikia hotuba kibao za jaji mkuu justice George Masaju kuwa Mahakama ni mhimili huru na itatenda haki na kukataa mbinyo wa aina yoyote ile toka upande wowote.

Historia inasema makaburu waliokuwa ktk serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini iliona waAfrika raia wengine waliokuwa wanadai kuwa watu-uhuru, kutaka demokrasia shirikishi na Marndeleo ya watu wote walikuwa ni hatari na wangeweza kuchelewesha maendeleo ya vitu kama madaraja, reli, flyovers pamoja ni miradi mingine mikubwa iliyokuwa ya mfano barani Afrika.

Madai hayo ya serikali ya kibaguzi ya wachache Afrika ya Kusini ya Makaburu miaka hii yanarudiwa na CCM miaka hii ya 2021 - 2026. Na CCM pamoja na serikali yake kudai wapinzani ni watu hatari wasio na uzalendo na wasioitakia Tanzania maendeleo.

Soma utetezi wa Nelson Mandela alipofikishwa mbele ya korti na utetezi huo wa Nelson Mandela kuenziwa na watu wote duniani na taasisi kubwa za kimataifa na vyuo vikuu vijana kufunguliwa macho juu ya tawala kandamizi za kibaguzi, katili na vinazokandamiza utu wa watu na haki zao kwa kisingizio cha kujenga uchumi, madaraja, flyovers, mabwawa ya umeme n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…