Kesi ya wabunge 19 wa viti maalum waliofukuzwa CHADEMA, Wakili Kibatala aanza kuwahoji mahakamani

Kesi ya wabunge 19 wa viti maalum waliofukuzwa CHADEMA, Wakili Kibatala aanza kuwahoji mahakamani

NA MKUU WA GEREZA ALIYEMTOA MTUHUMIWA USIKU WA MANANE KUKIWA NA GIZA NENE
 
Hata mimi imenishangaza kidogo juu ya CHADEMA nao walivyoichukulia hii kesi iendeshwe kimya kimya!

Hata hapa JF ni kama inakuja kinyemela vile, tofauti kabisa na hali iliyozoeleka kwa jambo kama hili.

Sijui, pengine ni katika mipang iliyokubaliwa kwenye mazungumzo ya "maridhiano", maanake naona mabadiliko makubwa sana jinsi CHADEMA inavyofanya mambo yake siku hizi.

CHADEMA wameanza kuwa controlled na serikali. Wajifunze kwa Raila madhara ya kujiungamanisha na serikali.
 
Dar es Salaam. Kesi ya wabunge wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya chama chao hicho cha zamani imeanza kuunguruma mahakamani, baada ya kukwama mara tatu.

Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, imeanza kusikilizwa leo Ijumaa Oktoba 7, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha, ambapo mawakili wa Chadema wameanza kuwahoji walalamikaji hao kuhusiana na malalamiko yao.

Hatua ya kuwahoji baadhi ya walalamikaji inatokana na maombi ya mawakili wa Chadema wanaoongozwa na Peter Kibatala ambao waliomba siku ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo wapewe nafasi ya kuwahoji walalamikaji wanane kati yao, akiwemo Mdee na wenzake saba.

Mbali na Mdee wengine walioitwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga na Cecila Pareso.

Wa kwanza kuwekwa kikaangoni leo Ijumaa ni Tendega, aliyekuwa katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), ambaye amehojiwa na Wakili Kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa Chadema.

Katika mahojiano hayo, Kibatala anamuuliza kuhusiana na madai au malalamiko yake kama alivyoyaweka katika kiapo chake, pamoja na mambo mengine akidai kufukuzwa uanachama bila kufuata utaratibu kwa kutokupewa haki ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakati Wakili Kibatala akimhoji Tendega kuhusiana na madai yake hayo, katika majibu mengine amekuwa akidai hajui huku mengine akikiri kuwa hajawasilisha mahakamani ushahidi hususani vilelezo kuthibitisha madai yake hayo.

Lakini pia amehojiwa kuhusiana na taratibu za ushughulikiaji matatizo ya wanachama wanaotuhumiwa ukiukwaji wa taratibu kanuni na katiba ya chama.

Pamoja na mambo mengine, wanalalamikia kuitwa kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu kwa njia ya WhatAsapp lakini alipopewa Katiba ya Chadema inatambua matumuzi ya tehema kama moja ya njia za mawasiliano.

Pia, amekiri hakuwahi kuandija barua kuwataka Katibu Mkuu, John Mnyika na mwenyekiti, Freeman Mbowe wasishiri kikao cha Baraza Kuu walikokata rufaa kupinga uamuzi wa kamati kuu kwa madai walioa kauli za kuwahujumu hata kabla ya vikao.

Kutokana na mahojiano hayo, shauri hilo limeahirishwa kwa saa moja kwa ajili ya maandalizi ya mahakama kuangalia vilelezo vya ‘flash disketi’ mbili kusikilizwa kauli walizozizungumza Mnyika na Mbowe ambazo wanazilalamikia.

Chanzo: Mwananchi
Ni kupenda tu kesi ili mawakili wapige hela. Hii kesi sio kesi. Uamuzi wa chama kuwafukuza uawachama wanachama wake ni haki isiyostahili kuhojiwa kirahisi.
 
Ingekuwa hivyo ingekuwa poa sana .Wanaoweza kufanya hivyo ni mahakama za wakenya huku kwetu ni ngumu mno .sijui majaji wetu wanaogopa nini ?
Ili waendeleze michongo yao gizani katika Dunia ya TEHAMA na Utandawazi.Hawa watu wamechoka mbaya,spana zipigwe na ikiwa nyeupe ama nyeusi tusisite kunena.
Mwisho wa yote ni upatikanaji wa Katiba Mpya ya Wananchi wenyenchi yao-Tanganyika na Zanzibar ndipo tuungane kupata Jamhuri ya Muungano.
Vinginevyo patachimbika hivi punde.
 
Je hii kesi haiwezi ikaoneshwa moja kwa moja kutoka mahakamani? Je kuna watu waliruhusiwa kufuatilia mahakamani!

katafute ugali wa wanao mkuu,kibatala anatafuta ugalia,mdee na wenzie wanatafuta ugali.

endelea kuishi kwa ushabiki.
 
Hii Kesi Wakenya wanafuatilia kwa karibu sana!
Acha kukurupuka hovyo kama ilivyo kawaida ya chawa wanapokuwa kikaangoni bila ushahidi wowote.

Jaji Mkuu wetu mstaafu alitambulishwa rasmi akihudhuria na kufuatilia yaliyokuwa yakiendelea mahakamani Kenya.

Sasa na wewe tutajie Mkenya ambaye anahudhuria rasmi na kufuatilia kwa karibu yanayojiri mahakamani kwetu.
 
katafute ugali wa wanao mkuu,kibatala anatafuta ugalia,mdee na wenzie wanatafuta ugali.

endelea kuishi kwa ushabiki.
Wewe hujui huyo unayemjibu kipumbavu hapo anauwezo wa kukulisha wewe, mke na wanao wote maisha yenu yote?

Hopeless kabisa.
 
Wewe hujui huyo unayemjibu kipumbavu hapo anauwezo wa kukulisha wewe, mke na wanao wote maisha yenu yote?

Hopeless kabisa.
sawa sawa mkuu,
lakini nasisitiza katafutie wanao ugali.
 
katafute ugali wa wanao mkuu,kibatala anatafuta ugalia,mdee na wenzie wanatafuta ugali.

endelea kuishi kwa ushabiki.

Yeye ugali tayari anao, sasa hivi anamtafutia Kibatala ugali, au unakonda?
 
sawa sawa mkuu,
lakini nasisitiza katafutie wanao ugali.
Tofauti na huyo uliyemjibu mwanzo, upande wangu nitakupa wewe kazi ya kunipikia ugali kila ninapouhitaji, maana naona ndicho kitu kilichokaa akilini mwako zaidi ya kitu kingine.
 
Tofauti na huyo uliyemjibu mwanzo, upande wangu nitakupa wewe kazi ya kunipikia ugali kila ninapouhitaji, maana naona ndicho kitu kilichokaa akilini mwako zaidi ya kitu kingine.
mimi kukupikia mpaka uwe nao huo ugali.

lakini umemjibia kama mkewe au chawa wake????
 
Back
Top Bottom