Mchezaji wa simba sports club akihisi coacher hatampanga kwenye mechi anaweza kwenda mahakamani kuzuia mechi isichezwe kwasababu ya hisia kuwa hatapangwa na atapata loss kwa washabiki wake, na fedha ya mechi ya siku.
Jaji atasaidia wengi sana kwenye vyama vya siasa wana hisi vikao vikikaa hawawezi kutendewa haki. Itakuwaje kwenye kura za maoni ambapo kuna wengi huwa wanakatwa majina na vyama vyao, Je hukumu hii si italeta kasheshe kwenye utendaji wa kila siku wa vyama vya siasa, makampuni, na taasisi mbalimbali?
Kesi hii ni kesi ya kipuuzi kabisa kuwahi kufunguliwa kwenye uwanja wa sheria? Sioni ni jinsi gani Jaji wa mahakama kuu atatoa hukumu kwa hisia. Sheria ni pamoja na material evidence, huwezi kuwa na hisia ukashinda kesi.
Kesi hii hata kama ina mkono wa Ikulu labda jaji awe mwehu kabisa. Kweli unazuia kikao cha chama kisikae eti unahisi utafukuzwa chama? Unazuia usijadiliwa kwa hisia utanyang'anywa kadi? Ni vipi mahakama inazuia chama kisisimamie maadili na sheria, kanuni na kanuni zake. Je Ni lazima kuwa mwanachama wa chama fulani is it enforceable by law kuwepo kwenye siasa? Kweli hii ni sababu ya kwenda mahakamani? Kwanini usisubiri ufukuzwe ndio uende mahakamni.
Posho, mshahara, ajira ndio vinapiganiwa sasa. Wasiwasi wangu ni kuwa wakili wa ZZK amemwingiza ZZK choo cha kike bila ya zito kujijua. Ajira Hapa TZ ngumu, Zito katangaza dau kubwa wakili kasema twende mzigo. Ushauri wa kisheria haujazingatiwa zaidi ya panic na kukurupuka.
Naamini kesi hii itatupwa.