Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Zanzibar, Khadija Nassoro Abdi, amewataka vijana na wananchi kwa ujumla kuwa makini na kile alichodai kuwa ni jitihada za baadhi ya watu na vyama kutumia hoja za Katiba pamoja na madai ya ubaguzi kati ya wananchi wa Zanzibar na Bara kwa lengo la kuwagawa Watanzania.
Amesema hayo leo Agosti 1, 2026, akiwa akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Tarafa ya Pawaga, Jimbo la Ismani mkoani Iringa, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.
Khadija amesema baadhi ya watu na vyama vimekuwa vikigusia masuala ya Katiba pamoja na kuibua hoja zinazohusisha tofauti kati ya Zanzibar na Bara, akidai kuwa hatua hiyo inalenga kuwachanganya wananchi na kuvuruga umoja uliopo
Pua soma: Mbunge Mohamed Ali: Kama kuwatetea vijana wa Zanzibar kutavunja Muungano basi acha uvunjike