Khadija Abdi: Wanatukoroga mara wanasema katiba, hicho tunachoambiwa kule wabara wanabaguliwa siyo kweli

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Your browser is not able to display this video.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Tanzania (UWT) Zanzibar, Khadija Nassoro Abdi, amewataka vijana na wananchi kwa ujumla kuwa makini na kile alichodai kuwa ni jitihada za baadhi ya watu na vyama kutumia hoja za Katiba pamoja na madai ya ubaguzi kati ya wananchi wa Zanzibar na Bara kwa lengo la kuwagawa Watanzania.

Amesema hayo leo Agosti 1, 2026, akiwa akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Tarafa ya Pawaga, Jimbo la Ismani mkoani Iringa, wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani humo.

Khadija amesema baadhi ya watu na vyama vimekuwa vikigusia masuala ya Katiba pamoja na kuibua hoja zinazohusisha tofauti kati ya Zanzibar na Bara, akidai kuwa hatua hiyo inalenga kuwachanganya wananchi na kuvuruga umoja uliopo

Pua soma: Mbunge Mohamed Ali: Kama kuwatetea vijana wa Zanzibar kutavunja Muungano basi acha uvunjike
 
Ulitegemea CCM aseme Nini Zaidi ya porojo?. Makamu wa Rais amesema tupambanie Katiba Mpya halafu huyu mdada anaiponda.
 
mambo yana enda speed.. leo wazenji hawaitaki katiba mpya, wanaona iliyopo ina wa favor.. Kosa kubwa alilofanya huyu anaye andaliwa kuwa mtakatifu Nyerere ni kuiachia Zanzibar, ilitakiwa mara baada ya kuungana ni ku unganisah kila kitu, yaani zanzibar iwe mkoa wa Tanzania. kufikia leo tungekuwa tusha changinyikana hakuna tena ukabila ubara na ukisiwani
 

Hivi hawa CCM mbona kama vile walio wengi huko wana upeo mdogo sana. Hivi wanapodai kuwa watu wamepeleka familia zao nje anamaanisha akina nani ...!!? Lissu na Lema au ni akina nani hao?

Naona ni wakati sasa tuanze kuorodhesha viongozi ambao familia zao ziko nje tuone. Maana nasikia kuwa Nzungu familia yake yote iko Belgium na tena wanaishi kule kwa status ya Ukimbizi.
 
Walitunga Katiba yao, ya Zanzibar tu.
Inayosema Zanzibar ni Nchi kimili, yenye wimbo wa Taifa, bendera yao na Rais wao.

Wawaache Watanganyika nao waandike ya kwao, yenye manufaa kwa Watanganyika.
 
Kipi kina nafuu, mwenye familia nje au mwenye akaunti ya fedha za wizi na rushwa nje ya nchi..
 
Mzanzibari mna nchi yenu na serikali yenu chini ya rais wenu, mambo yote ya bara hayawahusu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…