Alipoulizwa na mtangazaji wa Global kuhusu Zuchu kumnunulia gari, Khadija Kopa alisema kuna kuzaa na kunya na yeye ni miongoni mwa watu walio zaa, maneno hayo yametafsiliwa tofauti na watu wameenda mbali zaidi wakidai bi Khadija amewatukana wanawake wenzake ambao wamezaa watoto lakini hawajawapa magari na pengine nyumba kuwa hawakuzaa bali walikunya na watoto hao ni mavi wanatakiwa watupwe.
Hii kauli naomba tumkumbushe na yeye
Nini maoni yako?
========= Mtangazaji: Na hii gari nadhani ndio aliyokununulia Zuchu
Khadija Kopa: Eeeh, ndiyo
Mtangazaji: Hii ndio fahari ya mtoto, unalizungumziaje pia?
Khadija Kopa: Kuna kuzaa na kuna kunya, ukinya unatupa mavi yote yanaondoka, anaetaka mbolea pengine yamshinde kuyabeba lakini kuna kuzaa, mtoto hata akiwa anacho kidogo anakuona, sio lazima akupe gari lakini anacho kidogo anakuona sio lazima akupe gari lakini hata kidogo.
Kapata laki mbili basi ishirini ya mama, huko ndio kuzaa na nawaombea wazazi wenzangu wote mwenyezi Mungu awajaalie watoto wao wawe na imani na waweze kuwasaidia wazee wao na wazee wa wenzao InshaAllah.
Yuko sahihi tu mbona kakosea wapi?? Kuna watoto wanashika pesa na hawakumbuki wazazi wao full kusema hawana hela wakija JF wanajisifu kuhudumia malaya kwa kila kitu.
Mbona yupo sawa tu, ushu kazungumzia chochote kidogo, hapa kamaanisha mtoto kumkumbuka mzazi haijalishi kwa kiasi gani, hajasema sisi watoto tusio na vipato ni mavi, ila wasiowajali wazazi wao ni mavi.[emoji1]
Hata ukiwa unaotea kielfu 5 si mbaya kumkumbuka mama hata sayona ya jero, ishu sio kiasi unachotoa, ishu ni kutoa kwa moyo wako wa dhati(mapenzi), na hili jambo ndio linalomfurahisha mungu.
Sasa jipime mwenyewe we ni mavi au mtoto uliyezaliwa na mama.
Huyu mama si ni mwimbaji maarufu wa taarabu a.k.a mipasho; sasa watu wanalalalmikia nini tena kwenye majibu yake? Au walitaka ajibu kama Profesa wa uchumi?