Khadija Kopa: Kuna kuzaa na kunya, mtoto hata akiwa anacho kidogo anakuona

Mama Salma kikwete
Mama dangote
Na hadija kopa

Hao wanawake kwenye kuongea kama unasikiliza redio basi unazima maana wanaongeaga vitu vya ajabu sana kuongea mbele za watu ni mtihani sana kwao.
 
Riziki inatoka kwa Mungu ila inapitia kwenye mikono ya binadamu kuja kwako. Haishuki kama mvua Bali inapita kwenye mikono ya watu, kumbe basi ISHI NA WATU VIZURI
 
Khadija kamsifia bint yake lakini komenti zinawaponda watoto wa kiume tu
 


Labda neno "kunya" alilotumia ndilo lenye ukakasi tu lakini mantiki ya alichokisema ni swadaqta.🤣
 
Hajakosea kabisa,tunawasahau sana wazazi
 
Kuna kuzaa na kuya?[emoji23] mbona hivi viwili vinatoka matundu tofauti sasa[emoji23]
 
Kuna kuzaa na kuya?[emoji23] mbona hivi viwili vinatoka matundu tofauti sasa[emoji23]


Na wewe umeanza sasa!!!, angalia usiwe wewe ndie utukanaye kwani tunaweza kusema yeye kaongea msemo kwamba kuna "kunya na kuzaa", kwani unasemaje juu ya methali/mseno wa "nyani haoni kundu lake??" 🤣--- je hilo ni tusi??
 
Namuunga mkono KHADIJA, wewe kama hujali mzazi wako kutwa kucha Kitambaa cheupe na milupo una faida gani kwa mzazi?
Kuna wazazi wengine hawakuwajali watoto wao yaani walipowazaa kwao ikawa habari kwisha, hakuna cha malezi wala support yeyote, hawa pia tunawaweka kwenye kundi gani?
 
Ujumbe mzuri tatizo lugha.
Huwa nawashangaa wanaotumia neno kunya kwenye audience ya watu au kwenye mahojiano. Neno kunya halina tafsida. Angetumia busara kutumia maneno kujisaidia haja kubwa badala ya kunya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…