PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Klabu ya Singida Black Stars imemsimamisha kazi miezi mitatu kiungo wake Khalid Aucho raia wa Uganda kwa utovu wa nidhamu na utoro kazini.
Uamuzi huo umetolewa Februari 27, 2026 na Kamati ya Nidhamu ya klabu hiyo.
“Khalid Aucho ameadhibiwa kwa utovu wa nidhamu na utoro kazini hivyo amesimamishwa kazi kwa miezi mitatu” Imeeleza taarifa ya Kamati ya Nidhamu Singida BS
Katika hatua nyingine klabu hiyo imemsimamisha kazi miezi mitatu golikipa Amas Obasogie ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za upangaji wa matokeo.
Singida Black Stars imewakumbusha wachezaji na watumishi wake wote kuzingatia nidhamu, uwajibikaji na heshima kwa klabu.