Kuambiwa umejenga uwanja kijijini ndio matusi?kuiba michango ya wahanga ndio matusi?kweli kijani kuna vihiyo kwelikweli [emoji3]
Weka hapa list ya matusi aliyotukanwa rais wenu
Chama Chochote kinachoendekeza Ukabila hakifai kabisa .
Kuna mgombea anayeendekeza Siasa za ukabila na udini kwenye Taifa hili.
Ukiwajaza watu wa nyumbani kwako kwenye kila idara ni jambo la khatari sana kwenye Taifa lenye Katiba ya kifalme mana ndugu wanakua na Uchungu na mfalme sio kwa sababu ni mfalme bali kwa sababu ni ndugu wa damu.
Ndio maana madikteta wote wana kawaida ya kutumia Ukabila au Udini kuwanyazisha wapinzani wao.
Yani Dikteta yeyote ili afanikiwe kuwaangamiza wapinzani wake ni lazima aangalie kama ana nguvu ya kikabila basi anawajaza watu wa kabila lake kwenye vyombo vya dola ili aweze kutekeleza mbinu zake za kuwateketeza wapinzani wake kwa kuwapoteza ama kwa kuwaua kwa risasi au kwa namna nyingine.
Katiba yetu haifai kabisa kuwa na kiongozi anayejinasibu kikabila au kidini mana ni Katiba yetu inampa mkuu wa nchi mamlaka makubwa sana .
Kwa Mfano Kheri hata akiamua kutembea barabarani na Panga na kumkata kata kata yeyote asiyemtaka au anayeona ni adui wa ndugu yake ,hakuna mtu atakayeweza kumkamata na kumfunga kamba au hata pingu kwa hofu ya Ndugu Mfalme kama atakaa kimya bila kulaani kitendo hicho.
Akifikishwa mahakamani napo mahakimu wataogopa kutoa hukumu ya kumnyonga kumhofia mfalme.
Itatumila kila Mbinu na inawezekana mtu anayekatwa panga na kufa anaweza kusingiziwa kuwa alijarubu kumdhuru ndugu kama huyo wa mfalme. Aliposhindwa aliamua kujiua mwenyewe. Hofu ya wasimamia haki kuigusa familia ya Mfalme ni kubwa sana mana Katiba inampa mamlaka yote ya duniani mfalme.
Mfano RC yule alipokua anakwenda kujaribu kuwamaliza watangazaji wa TV fulani .Waziri alipojarubu kujua ukweli wa uvamizi ule alitimuliwa na kutishiwa kwa Bastola.
Watu wengine wote walikaa kimya.
Hivyo wale wanaoambiwa kuwa wanamtukana mgombea ambaye ni ndugu wa Bwana Kheri wawe makini mana sio tu anapata jeuri ya kufanya chochote kwa yeyote lakini pia hatanii wala haongei kisiasa bali kifamilia . Yaani Kheri anaona ndugu yake amepoteza mvuto ghafla baada ya wananchi kuonyeshwa upande wa pili wa shilingi.
Tuepuke kujaza ndugu kwenye ofisi za umma hasa zenye kusimamia haki sawa kwa wote.
Maendeleo ni kwa wale walionichagua tu.Wengine mtajuata .