Wewe mpuuzi eti nawe unajiita Dr. Akili...huu udokta wenu huko CCM ni sawa na uhayawani! Kuna tusi zaidi ya kuwatishia raia wasio na hatia kwamba utawapiga wao, mama zao, shangazi zao na dada zao, huu si uhuni tu?
Hebu msikilize huyu mwingine anasema nini kuhusu kuwapelekea watu maendeleo...
Je wanaowakilishwa na wapinzani hawalipi kodi?
Mbona mgombea wenu anawatisha wananchi kwamba hawatajengewa barabara kama watachagua wagombea kutoka upinzani?
Shangazi zao na dada zao uwapige halafu kodi zao ukusanye lakini maendeleo uzuie huku wote ni Watanzania, kweli!