Kheri James na Vincent Mashinji kupewa Ukuu wa Wilaya ni demotion

Kheri James na Vincent Mashinji kupewa Ukuu wa Wilaya ni demotion

Milion I 2 ampe dj kabisa mbona ndoto za mchana kweupe
Mzee usikurupuke, milioni 12,NYUMBA milioni 7,GARI viieite,na mengine mengi.

HALAFU una upeo mdogo sana Mbowe ndiye anatoa mshahara au ni maamuzi ya chama .Acheni akili za makali*n hazina tija wala hazisaidii chochote.
 
Wote wawili ni demotion ya kiwango kikubwa.

Kiuhalisia, James amekwishaondolewa kwenye nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM. Kuwa mkuu wa wilaya, ni kuwa mtendaji wa Serikali kila siku. Sasa hawezi kutoka ofisini kwenda kwenye shughuli za cha bila ya kuruhusiwa na Mkuu wa Mkoa. Imetafutwa namna ya kumdhibiti.

Huyu Mama Samia, ni mjuzi hasa. Ukiwa na akili ndogo, unaweza kuondolewa kwenye uongozi huku ukishangilia kwa furaha kubwa, ukiamini umepanda.
SSH anajitahidi kuunda CCM mpya yenye watu anaowataka Ila kuhuhalisia anachofanya anakimaliza chama,wanaoingizwa CCM walio wapya ni mzigo kwa chama na matokeo yake atayaona uchaguzi mkuu 2025
 
Uteuzi wa komredi Kheri James Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa (UVCCM) na Dr. Mashinji kuwa wakuu wa wilaya hii ni demotion( Kushushwa Vyeo), kwani hawa walikuwa viongozi wa juu na sasa wanakwenda kuwajibika kwa wakuu wa mikoa Amos Makala Dar es Salaam na Alli Hapi, Mara.

Kwa nafasi walizokuwa nazo awali walikuwa wanaingia kwenye vikao vikuu vya chama vyenye kutoa maamuzi mazito ya chama kama Kamati Kuu za vyama vyao na walikuwa wanaongoza wilaya na mikoa. Mama kumpa James u-DC wa Ubungo ni kuonyesha hataki kufanya naye kazi ndani ya chama na anataka mtu mwingine kwenye umoja wa vijana.

Mimi sijui JF kuna watu wana akili gani mfano kama wewe uliotuma huu uzi ni upuuuzi mtupu. Hivi nani kati ya hawa wawili kapata demotion? Hakuna mtu hata mmoja. Labda hujui maana ya neno demotion hivyo ni bora tukaeleweshana maana ya neno demotion kisha tuendelee na mada yetu. ( A demotion is a compulsory reduction in an employee's rank or job title within the organizational hierarchy of a company public service department, or other body, unless there is no reduction in pay.) Yani mi maamuzi ya lazima yakumshusha cheo mtumishi ndani ya mfumo wa taasisi.

1. Dr Mashinji - Tuongelee kashushwa cheo kipi ndani ya Serikali ya Tanzania?? Huyu alikuwa katinu mkuu wa Chadema na sasa ameteuliwa Mkuu wa Wilaya wa Serikali ya CCM. Kifupi Serikali mamlaka haijafanya reference yoyote kulingana na nafasi aliyokuwa nayo Chadema ila wameona ni msomi asie na kazi na fursa ikapatikama akapewa kazi. Hivyo hajashushwa cheo chochote bali kapata ajira Serikalini.

2. Kheri James - Huyu alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM nafasi ambayo aligombea na akapata ndani ya CCM. Sasa mamlaka imemuona na amepewa nafasi ya UDC ndani ya Serikali. Sasa hapa demotion iko wapi kati ya UVCCM na UDC.

Kumbuka demotion siyo kitu cha hiari bali ni lazima hivyo basi James hata angemaliza muda wake wa uwenyekiti TAIFA halafu akagombea uwenyekiti CCM Mkoa wowote bado isingekuwa demotion kwani ni maamuzi yake. Demotion ni pale ambapo katibu mkuu Taifa aliyoko madarakani akatolewa na kupelekwa KK mkoa hiyo ndio demotion au Chalamila angetolewa u RC wa Mwanza kwenda DC Nyamagana hapo ingekuwa demotion.

Asante
 
Mwakani wenyekiti wake ulikuwa unafika mwisho. Pia ataendelea kuvaa kofia mbili hadi mwakani
 
Uteuzi wa komredi Kheri James Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa (UVCCM) na Dr. Mashinji kuwa wakuu wa wilaya hii ni demotion( Kushushwa Vyeo), kwani hawa walikuwa viongozi wa juu na sasa wanakwenda kuwajibika kwa wakuu wa mikoa Amos Makala Dar es Salaam na Alli Hapi, Mara.

Kwa nafasi walizokuwa nazo awali walikuwa wanaingia kwenye vikao vikuu vya chama vyenye kutoa maamuzi mazito ya chama kama Kamati Kuu za vyama vyao na walikuwa wanaongoza wilaya na mikoa. Mama kumpa James u-DC wa Ubungo ni kuonyesha hataki kufanya naye kazi ndani ya chama na anataka mtu mwingine kwenye umoja wa vijana.
Mkuu hao ndo wanaondolewa kwenye mfumo wa kistaarabu.

Wapatukaji wote wa nyakati zile wanaondolewa kwa mfumo wa kiutu uzima kama huu,huyu anasogezwa nje ya ulingo.
 
Simple logic haitaji analysis ya ajabu kwa level ya Mashinji mtu alyekuwa anapata kipato cha 12m/- per month leo unapata 4m unaona sawa ni ajabu kweli? naona wewe ni Tomaso huamini mpka uumshike Yesu. Kipato chake kimeshuka kimepanda. Fursa hiyo ni sawa na Machopabga, Mwalukuzi amtu aliyekuwa na level ya Chongola,Je chongola ameshuka au kapanda cheo?
 
Kama unafuatilia siasa, Nchimbi akiwa mkiti UVCCM aliwahi kuteuliwa kuwa DC wa Bunda na maisha yakaendelea.

Rashid Mfaume Kawawa amewahi kuwa waziri mkuu, ila baadae akaja kuwa waziri asie na wizara maalum.
Kwenye siasa hasa za uteuzi, waingereza wanasema they "serve the pleasure" ya mamlaka ya uteuzi.

The serve at her excellency pleasure.

Kila la heri kwa Dr. Mashinji, Kheri James na wengine wote mliopata imani ya Rais kumwakilisha katika wilaya mlizopangiwa.

F
 
Boss ya Uvccm ameonekana kwenye mkeka wa udc ambao mama amebet June hii.Nimefika Lumumba, vijana wanalaumu uteuzi huu, wapo wanaosema amewekwa kwenye cheo Sawa na wale waliokuwa wakimuita boss,unawekwa cheo kimoja Sawa na mchopenga aliyekuwa anakuita boss, huku ukiwa boss wa vijana taifa.
Vijana wanaponda VYEO vya kuteuliwa ukikosea unafukuzwa so kinamshushia hadhi.Sasa hii inakuaje ni Kweli Heri James kwa cheo alichokuwanacho kimemshushia heshima au kwa kuwa rais kamteua.
 
Heri James
Doto James
Furaha James

Masalia ya mwendazake ndiyo yanapukutishwa.
Utasubiri sana wote wale wataendelea kuchapa kazi.Wanaelimu na uwezo wa kuongozi .Wewe endelea na kuhubiri ukabila.
 
Boss ya Uvccm ameonekana kwenye mkeka wa udc ambao mama amebet June hii.Nimefika Lumumba, vijana wanalaumu uteuzi huu, wapo wanaosema amewekwa kwenye cheo Sawa na wale waliokuwa wakimuita boss,unawekwa cheo kimoja Sawa na mchopenga aliyekuwa anakuita boss, huku ukiwa boss wa vijana taifa.
Vijana wanaponda VYEO vya kuteuliwa ukikosea unafukuzwa so kinamshushia hadhi.Sasa hii inakuaje ni Kweli Heri James kwa cheo alichokuwanacho kimemshushia heshima au kwa kuwa rais kamteua.
Kwanza vijana hao wanafaa washukuru mamlaka ya uteuzi japo kwa kumuachia nafasi hiyo,kwani hata hiyo nikupewa nafasi ya kujirekebisha kwa mapungufu ya awali.
 
Simple logic haitaji analysis ya ajabu kwa level ya Mashinji mtu alyekuwa anapata kipato cha 12m/- per month leo unapata 4m unaona sawa ni ajabu kweli? naona wewe ni Tomaso huamini mpka uumshike Yesu. Kipato chake kimeshuka kimepanda. Fursa hiyo ni sawa na Machopabga, Mwalukuzi amtu aliyekuwa na level ya Chongola,Je chongola ameshuka au kapanda cheo?

Kwahiyo Mashinji ameteuliwa kuwa DC akitokea Ukatibu Mkuu Chadema??? Mashinji kaondoka Chadema tokea January 2020 hivyo hiyo M12 hajaipata kwa mwaka mmoja na nusu. Hivyo tukubaliane Mashinji hakuwa na kazi ya kuajiriwa kwenye kupindi hiki na ndio sasa kaipata yenye huo mshahara wa m4. Ukiniambiwa sijui katoka kwenye mshahara wa m12 kwenda m4 mimi sikueleweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Boss ya Uvccm ameonekana kwenye mkeka wa udc ambao mama amebet June hii.Nimefika Lumumba, vijana wanalaumu uteuzi huu, wapo wanaosema amewekwa kwenye cheo Sawa na wale waliokuwa wakimuita boss,unawekwa cheo kimoja Sawa na mchopenga aliyekuwa anakuita boss, huku ukiwa boss wa vijana taifa.
Vijana wanaponda VYEO vya kuteuliwa ukikosea unafukuzwa so kinamshushia hadhi.Sasa hii inakuaje ni Kweli Heri James kwa cheo alichokuwanacho kimemshushia heshima au kwa kuwa rais kamteua.
Hiyo ni promotion kubwa sn
 
Kuna wakati tukumbuke kila mtu na mtuwe na pia msukuma kula urojo akikosa chakula kingine ni ushujaa.
 
Back
Top Bottom