Khitma ya Saigon club ya Iddi Simba msikiti wa Mtoro




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaandika hitma ya Iddi Simba inayotaja watu wengine kuliko inavyomtaja Iddi Simba, kwa namna ambayo inaweza kutafsirika kuwa umetumia msiba wa Iddi Simba kueneza siasa zaidi ya kuhitimisha maisha ya Iddi Simba.

Hata kama unaandika siasa, ingekuwa bora ukaandika siasa za maisha ya Iddi Simba zaidi, kafanya nini, kasema nini, lini, maisha yake yalikuwaje.

Sasa wewe unaandika siasa zako za kila siku, unachomeka jina la Iddi Simba sehemu moja au mbili, halafu unasema hiyo ni hitma ya Iddi Simba?

Hiyo ni hitma ya Iddi Simba au siasa za kila siku zinazotumia jina la Iddi Simba na wasaa wa msiba wake kujitangaza tu?

Hitma yako imeelezea siasa na majina ya watu wengine kuliko maisha ya Iddi Simba.

Hapo hujamtendea haki Iddi Simba, hujautendea haki usomi wako wa historia wala hizo siasa zako za Uislamu.

Umejionesha wewe ni opportunist tu.

Kama vulture, yule ndege anayesubiri wenziwe wafe yeye apate mlo bila kujali itifaki za mazishi.

You are a vulture

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga,
Hiyo ndiyo namna yangu ninapoeleza historia.

Huwa nakwenda mbali zaidi na kuyakusanya mambo mengi ya nyakati zile kisha humtumbukiza ndani muhusika mkuu.

Kwa staili hii nimepata wasomaji wengi ambao wakiona makala yangu hawawezi kuipita lazima watasimama na kuangalia nimeleta kipi kipya?

Hizo ''name calling,'' hazinihagaishi ila kwa kitu kimoja.

Nakuonea huruma jinsi kalamu yangu inavyochoma moyo wako.

Ulitaka nimuandike Iddi Simba peke yake kama vile hakuwa amezungukwa na watu na mie nikiwa mmoja wa watu hao.
 
Hapa umemuongelea hayati Idd Simba( Mwenye enzi Mungu amrehemu) au habari za dini za miaka ya 80?

Nimeshindwa kukuelewa

Sent using Jamii Forums mobile app

Uncle Ben,
Hivyo ulivyoeleza ndivyo nilivyokusudia.

Nimeandika siasa kama alivyozikuta Iddi Simba aliporudi Tanzania.

Rais alikuwa Mzee Ali Hassan Mwinyi na kulikuwa na matatizo mengi ndani ya chama chake na serikali kiasi ya kuwa magazeti ya chama na serikali yakimwandika vibaya nk. nk.

Naamini sasa umenielewa la ikiwa bado niulize nami In Shaa Allah nitajitahidi kukufahamisha kadri ya uwezo wangu.
 
Kubali, hujamtendea haki marehemu Iddi Simba. Umetumia jina/kifo chake kama uchochoro wa kusambazia propaganda zako. Kwa watu waliostaarabika hiyo si sawa na haikubaliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kubali, hujamtendea haki marehemu Iddi Simba. Umetumia jina/kifo chake kama uchochoro wa kusambazia propaganda zako. Kwa watu waliostaarabika hiyo si sawa na haikubaliki.

Sent using Jamii Forums mobile app
Trace...
Mimi sina uwezo wa kukuzuia kuamini kile utakacho.

Hii ni nchi huru na inathamini uhuru wa fikra na kukinzana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujaweza kuwa na uwezo wa kunichoma moyo.

Unichome moyo kwa kamasi hizi chafu ambazo unapenga halafu hata kujifuta hujui?

Do not flatter yourself.

Na kuandika habari za maisha ya Iddi Simba zilizomzunguka Iddi Simba wala si kuandika habari za Iddi Simba peke yake.

Lakini pia si kuandika habari za siasa zako tupu, ukambandika Iddi Simba sehemu moja au mbili, halafu ukasema hiyo ni hitima ya Iddi Simba.

Kama unamjua Iddi Simba andika habari zake.

Kama humjui, acha kujishaua kuandika habari za watu usiowajua.

Na zaidi, acha kutumia misiba ya watu maarufu kueneza habari za siasa zako.

Kwa watu tunaosoma kwa kituo tunakuona hamnazo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga,
Nasema nafsi yako inataabika kwa kuwa unaandika huku umeghadhibika.

Nasema umekasirika kwa kuwa unaishambulia haiba yangu.

Nimekuwa nikikutana na watu wa mfano wa wewe kwa miaka mingi kwa ajili ya kalamu yangu na wote mnafanana na kinachokunganisheni ni hasira zilizomo vifuani mwenu kila mnaponisoma.

Matumizi ya maneno ya matusi dhidi yangu yako dhahiri katika uandishi wako.

Wala mimi siwezi kuwa hamnazo kwa kiwango chochote utakachotumia.

Iddi Simba tunafahamiana vizuri na alikuwa mzugumzaji wangu sana.

Dar es Salaam hii mimi nitunie misiba ya watu...

Nifanye hivyo kwa kutafuta kitu gani?
Flattering?

Hapa kwetu Dar es Salaam au mji mwingine?
 
Pumbaavu huna hata aibu! Umechukulia kifo cha Muislamu mwenzako ambaye hamkuwa naye karibu kihivyo alipokuwa hai kama fursa tu ya kueneza siasa zako za kibaguzi za udini.

Taratibu jamaa yangu; tujadiliane kwa staha.
 
Taratibu jamaa yangu; tujadiliane kwa staha.
Mfiaukweli,
Ndugu yetu amehamaki jinsi nilivyomweleza Iddi Simba kwa kumuunganisha na historia ya Dar es Salaam na watu wake.

Hii ni moja ya ibra ya historia hii hata kama itakuwa ndani ya taazia wapo watu wanatamani kama historia hii isingelikuwapo.

Matokeo yake ndiyo haya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam. Nami ningependa kujua historia ya St. Joseph's School aka Forodhani, shule yangu ya msingi enzi za baada ya uhuru hadi mwisho wa miaka ya 80 wakati wa Nyerere na Ujamaa.

Kiwanja hiki walipewa Wamisionari wa kikatoloki na Sultan wa Zanzibar Majid, kama Kanisa kuu la Bagamoyo na minara miwili Zanzibar


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Sio sahihi..
Historia ya mtu husimuliwa na watu aliowagusa kwa namna moja ama nyingine bila kujali ni ndugu ama wanafamilia. Ulishasikia wanafamilia wanamzungumzia Mkapa zaidi ya watu aliowagusa au kufanya nao kazi.
Jipambanue, hadhira bado ni pana sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwana...
Jana nimeletewa taarifa ya msiba wa mmoja wa ndugu zangu.

Msiba huu ukanikumbusha mengi basi nikaandika taazia fupi.

Naiweka hapo chini taazia hiyo ili wale ambao wanataabishwa na staili ya uandishi wangu wapate rejea nyingine:

''Nikifahamiana na na Bi. Sharifa toka miaka ya 1970s yeye na rafiki yake Bi. Mgeni ambaye alishatangulia mbele ya haki miaka mingi iliyopita.

Bibi yangu Bi. Mwatum bint Mgeni nyumba yake ilikuwa Mtaa wa Sekenke si mbali na kwao Bi. Sharifa.

Namkumbuka Bi. Sharifa siku hizo ni msichana mdogo yeye na shoga yake Bi. Mgeni wakija kusali Fajr msikiti wa Mtambani ule wa zamani wakiongozana na Liumbi Abdallah kijana umri wao ambae mimi alikuwa rafiki yangu sana.

Katika miaka hii ya karibuni niliwahi kufika nyumbani kwa Sheikh Kalala Mikocheni baada ya miaka mingi nikaonana na Bi. Sharifa.

Bi. Sharifa alifurahi sana kuniona baada ya yeye na mumewe kuhamia Marekani.

Miaka mingi sana ilikuwa imepita na nilimfahamisha kuwa nilikuja Washington na nilikuwa Maryland lakini muda haukutosha kuwapitia ndugu na jamaa wote na hiyo ndiyo sababu sikuwatembelea kwao.

Taarifa hii ya msiba imenirudisha nyuma sana kunikumbusha Bi. Sharifa na rafiki yake Bi. Mgeni na Imam wetu aliyekuwa akitusalisha Fajr marehemu Sheikh Mwagavumbi kwenye ule msikiti mdogo wa Mtambani.

Nimemkumbuka pia na Mzee Hassan mnadi sala ambae akitoka kwake Kinondoni Shamba njia nzima akielekea msikitini ananadi, "Salaa, Salaa..." hadi anafika msikitini.

Siku hizo kulikuwa hakuna "loud speakers," na Mzee Hassan alifanya kazi hii ya kunadi sala na kuadhini hadi alipofariki.

Kwa kweli historia ya Bi. Sharifa imenirudia upya na wakati ule kasichana kadogo kajitanda khanga na shoga yake Bi. Mgeni wanakuja msikitini kusali Fajr, kitendo hiki hakikunielemea kama hivi sasa nikitazama nyuma na kuhisi athari yake.

Kaka Kalala nina hakika hili litamshangaza kujua kuwa mimi nimemuona yeye kwa mara ya kwanza nilipokwenda kumuona Bi. Sharifa hospitali alikolazwa ilikuwa ndiyo kwanza siku za mwanzo kamuoa Bi. Sharifa.

Kabla ya hapo nikilisikia tu jina la Kalala sikupata kukutananae.

Baadae nikasikia Sharifa na mumewe wamehamia Marekani.

Sikupata kumuona Bi. Sharifa hadi waliporudi Tanzania.

Allah ampe kauli thabit dada yetu na amjazie pale palipopungua.
Amin.''
 
Mkuu, umemuelezea vizuri sana huyu mzee... ni Vulture haswaa! Tapeli na laghai la kidini! Anapindua pindua historia za marehemu kwa malengo yake ya utapeli wa kidini!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakuelewa Mzee wangu
 
Mkuu, umemuelezea vizuri sana huyu mzee... ni Vulture haswaa! Tapeli na laghai la kidini! Anapindua pindua historia za marehemu kwa malengo yake ya utapeli wa kidini!

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzizi,
Nimesomeshwa ilm ya minakasha yaani majadiliano na Sheikh Haruna na alikuwa akitueleza kuwa ukiona mtu anakuja na matusi elewa umeshamshinda kwani mwenye hoja ataleta hoja hawezi kubadili hoja kwa kutukana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…