Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Kiranga,
Nina namna yangu ya kuandika na kuhadhiri tofauti sana na watu wengine.
Mimi hupenda kuandika na kueleza yale ambayo wengi hawajui.
Haya kwa kawaida hushikwa na watu kuliko tarehe ya kuzaliwa, ana watoto wangapi na maelezo mfano ya hayo.
Nimeanza kumueleza Iddi Simba akiwa mazikoni nyumbani kwa Bi. Mruguru bint Mussa mama yake Ally Sykes kakaa kwenye jamvi na Ally Sykes na Zuberi Mtemvu.
Ally Sykes analaumu nchi imeharibika hakuna mchele wala mafuta ya kupikia.
Zuberi Mtemvu anamjibu kwa kejeli kuwa asilalamike hayo kayataka mwenyewe.
Ally Sykes akamjibu anauliza, "Nyie Congress kumbe hatukuwamaliza bado mpo."
Ally Sykes, Abdul Sykes na Julius Nyerere walikuwa TANU na Mtemvu chama chake Congress.
Kufika hapa nikamleta Iddi Simba kupitia kinywa cha Mtemvu alipomuuliza Ally Sykes, "Huyu Nani?"
"Humjui huyu?" Ally Sykes kashangaa.
"Huyu ni Iddi Simba."
Hii ndiyo staili yangu na wengi wanaipenda.
Baada ya hapo nikaja Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Muslim School aliposoma Iddi Simba nk.
Hapo ndiko nikaingia katika tarikh ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lini ilianzishwa (1933), madhumuni yake na kwa nini wanafunzi wa shule hii walikuja kuwa mstari wa mbele dhidi ya ukoloni.
Hii ndiyo namna yangu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app