Mlaleo,
Kuna historia nakuwekea hapa usome kisha tunaweza tukaendelea na mjadala:
Ndjabu...
Ondoa tu hayo matusi hayana maana lakini yote uliyoandika ni muhimu.
Obsession honestly...
Hakika kisa cha akina Sykes ni kisa mimi kimenikamata sana.
Achilia ule udugu lakini siku niliposoma kitabu, ''Modern Tanzanians,'' kitabu alichohariri John Iliffe na kusoma, ''The Townsman: The Life of Kleist Sykes,'' sura iliyoandikwa na mjukuu wa Kleist Sykes, Aisha ''Daisy'' Sykes Buruku historia hii ilikamata fikra zangu (Modern Tanzanians, (ed), East African Publishing House, Nairobi, 1973).
Nakumbuka kama vile jana nilikuwa katika Maktaba ya Taifa, Arusha ndipo nilipokikuta kitabu hiki.
Utafiti wangu wa kutaka kujua mengi ulianza siku ile.
Nikawauliza hawa ndugu zangu juu ya kitabu cha Iliffe.
Wakanifahamisha kuwa babu yao, Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949 alikuwa ameandika ''kitabu,'' ambacho alimwachia mwanae Abdul Sykes.
Kwa hakika hakikuwa kitabu bali mswada wa kitabu.
Mwanae Abdu Sykes, Daisy alipoingia Chuo Kikuu cha Afrika ya Mashariki mwaka wa 1967 kusoma Elimu na Historia ndipo alipokutana na John Iliffe na huyu mwalimu wake baada ya kufahamu historia ya akina Sykes na yeye kama mimi akakumbwa na hii ''obsession,'' akataka kujua mengi vipi walifika Tanganyika kutoka Afrika ya Kusini.
Hapo ndipo Daisy akawa anachukua nyaraka zilizokuwa katika familia na kumuonyesha Iliffe pamoja na mswada wa kitabu alichoandika babu yake.
Kutokana na nyaraka hizi Iliffe akaandika paper hii: '‘The Role of the African Association in the formation and Realisation of Territorial Conciousness in
Tanzania.’ Mimeo, Universityof East Africa Social Sciences Conference,'' 1968.
Iliffe kapatwa na homa ya ''obsession,'' ya akina Sykes anataka kujua mengi zaidi Daisy akipewa ''assignment,'' anakwenda kwa baba yake anauliza anapewa maelezo na ushahidi wa nyaraka.
Iliffe kila akielezwa hili ndani linazuka jingine akataka kujua ilikuwaje Abdul Sykes akawa General Secretary wa Dar es Salaam Dockworkers Union mwaka wa 1948.
Iliffe akapewa maelezo na nyaraka akaandika paper hii:‘A History of Dockworkers of Dar es Salaam’ TNR, Dar es Salaam, 71, 1970.
Iliffe kama mimi miaka mingi baadae akawa Sykes, Sykes na Sykes.
Sijui kwa nini Iliffe hakuandika historia ya TANU kwa ukamilifu wake wala hakuwa na shauku ya kukutana na Abdul Sykes, baba wa mwanafunzi wake hodari Aisha ''Daisy,' Sykes ambae kamsaidia sana kuijua historia ya African Association na TANU.
Mohamed Said na yeye kwa kumsoma Iliffe gonjwa la Sykes likamkumba.
Mimi nikaamua kufanya kile Iliffe hakufanya nacho ni kuandika maisha ya Abdul Sykes lakini nikaamua pia kuweka mguu wangu pale unyayo wa Iliffe ulipokanyaga.
Hapa ndipo ilipoaanza safari yangu iliyonifikisha hadi Imhambane kijiji kinachoitwa Kwa Likunyi alipotoka Sykes Mbuwane kuelekea Laurenco Marquis akiwa ameongozana na Chief Mohosh na Wazulu wengine kupanda manowari ya Wajerumani kuja Pangani kuanza vita na Abushiri bin Salim na Mtwa Mkwawa mwishoni mwa miaka ya 1880.
Huyu Chief Mohosh ndiye akaja kujulikana kama Affande Plantan Tanganyika akiwa mkuu wa Germany Constabulary.
Prof. Emmanuel Achiempong wa Harvard na yeye gonjwa la Sykes likamkumba akaniandikia mwaka wa 2008 kuniomba anijumuishe katika mradi wa Dictionary of African Biography (DAB) anataka niandike mchango wa Kleist Sykes katika historia ya Afrika.
Mradi huu ulijumisha waandishi na watafiti takriban 500 kutoka kila pembe ya dunia.
Oxford University Press, New York wamechapa volumes sita ya kazi hii.
Bwana Ndja
Yako mengi lakini kwa leo tuuishie hapa sitaki kuwachosha wasomaji.
Saigon haijapata kufifia hata siku moja kuanzia ilipoundwa mwaka wa 1967 nami nikiwa mmoja wa waasisi.
Wastani wa umri wetu ulikuwa miaka 15 na huu ndiyo ulikuwa umri wangu mimi.
Baada ya kuwa sasa tumekuwa watu wazima hatuwezi tena kucheza mpira Saigon imebakia kuwa Barza maarufu sana ya Wanamji wa Dar es Salaam.
Saigon ina kalenda mbili muhimu sana ya mwaka kitu ambacho hata vilabu vikubwa havijaweza kufanya.
Kila mwaka Saigon inafanya khitma ya kuwarehemu wanachama wenzetu waliotangulia mbele ya haki, ndugu na jamaa na masheikh wetu na jina la kwanza kutajwa huwa la Sheikh Hassan bin Ameir.
Saigon kila mwaka Mwezi wa Ramadhani tunafuturisha.
Huu mpango wa futari alianzishamarehemu Iddi Simba kwa kuwaalika viongozi wa Saigon nyumbani kwake kwa ajili ya futari kisha akaleta wazo kuwa itakuwa bora zaidi ikiwa futari hii itafanyika club kwa wanachama wote na Waislam kwa ujumla.
Wazo hili liliafikiwa na yeye mwenyewe ndiye aliyekuwa akigharamia futari kila mwaka hadi alipofariki.
Katika shughuli hizi zote wageni wa heshima wanakuwa viongozi wakubwa wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Lakini kubwa linalojenga nguvu Saigon ni ule uwezo wake wa kuweza kuwavutia wanachama wapya wa kila aina bila ya kujali dini wala kabila zao au ni wazawa wa Dar es Salaam au kwengineko.
Tunamuomba Allah ajaalie mapenzi haya yadumu hadi siku ya mwisho.
Nakuwekea picha ya Ally Sykes akiwa na Sheikh Issa Aussi wazee ambao wamekuwa pamoja na baba yangu katika mitaa ya Dar es Salaam.
Nakuweka pia picha ya Iddi Simba katika khitma yake ya mwisho kuhudhuria mwaka jana.
Kulia ni Ally Sykes na pembeni yake ni Sheikh Issa Ausi picha hii nimewapiga mimi kwenye Khitma ya Saigon mwaka wa 2010.
Wote kwa sasa ni marehemu.
Hii ni klabu hapa Dar es salaam ambayo kila Rais wa Tanzania alikuwa member (sina hakika kama huyu wa sasa, Magufuli naye ni member) Wazee wetu na walikuwa members toka miaka hiyo sisi tunakua ya 1980's (wengine tumekuja kuiona baada ya kuhamia Kariakoo Mtaa wa sikukuu). Mohammed Said tunaomba...