Pole sana. Haijalishi dini yako ila Jina la Yesu Kristo linaponya. Fuatiza maneno haya. Mungu nakuja mbele zako kuomba toba kwa kiapo ambacho niliingia bila kukushirikisha wewe, Mungu ninaomba unisamehe kwa kufanya kiapo amabcho ni kinyume na matakwa yako. Mungu natubu hii dhambi ya kiapo kwani ni kinyume na yale uyatakayo wewe kama yalivyo mapenzi yako juu yangu. Mungu ninatubu na dhambi zingine zote ambazo Mungu nilifanya kwa kutenda au hisia ambazo ziliniwekea kifungo cha viapo vingine. Mungu ninaomba toba kwa niaba ya kijana ambaye tuliingia mahusiano na akatamka maneno ya kunifunga kwa kiapo, naomba Mungu msamaha kwa niaba yake. Mungu wangu Baba Yangu naomba kuvunja maneno na viapo vyote tulivyovitamka na kijana (taja jina), nina nyunyizia damu ya Yesu Kristo, ikatangue maneno na viapo vyote ambavyo tulivutamka. Nina nyunyizia damu ya Yeau Kristo, damu ya Agano jipya kwenye kauli na maneno ambayo kijana (taja jina) aliyatamka, kuanzia sasa maneno yake yakose nguvu na damu ya Yesu Kristo ikayayeyushe yote nibaki na baraka zako Mungu ulizoniumbia. Naomba hayo yote ktk jina la Yesu Kristo, Amina.
Ukiyafuatisha hayo maneno, na unaweza kuongezea kadri unavyoona basi nte dadhicho kiapo hakitafanya kazi kabisa na utakuwa huru.